Nape amjibu Lowassa kuhusu Ajira...!

Nilichokurupuka ni kipi? au kwasababu nimepingana na hoja ya kuwaita vijana bomu kila siku? Na kisa kasema flani? Lazima umtukane nape na kumwita mbumbumbu ndio siku yako iende?... Serikali imetoa takwimu za hali halisi ya ajira nchini, nikatakiwa kutoa maoni, nilichojibu kuwa serikali iko sahihi, hali ya ajira nchini kwa takwimu sio maneno ya barabarani, na hasa ukilinganisha na nchi hata za Afrika mashariki tu Tanzania ni bora kuliko zingine, umbumbumbu wa Nape uko wapi?

Nadhani ni vizuri pamoja na kutakiwa kutukana kila unapokuta jina la Nape, akili za kuambiwa changanya na zako....

Kwanza nimefurahishwa na utayari wako wa kutetea kile unachoamini. Kuhusu suala la ajira kwa vijana nadhani utakuwa ama kujamwelewa vyema waziri mkuu mjiuzulu Lowassa au kwa makusudi unabadili kile alichosema ili upate hoja za kumpinga. Hakuwaita vijana mabomu bali alisema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ndio bomu. Sio kweli pia kuwa Mh. Lowassa amekuwa akiwaita vijana mabomu kila siku kama unavyodai kwenye hoja yako.

Tukirudi kwenye ukweli wa mambo suala la ukosefu wa ajira kwa vijana lipo na kama alivyosema Mh. Lowassa ni bomu linalosubiri kulipuka. Ni kweli serikali na sekta mbalimbali wamekuwa wakiajiri vijana wanaomaliza masomo kwenye ngazi mbalimbali lakini kiwango cha ongezeko la vijana wanaohitaji ajira baada ya kumaliza masomo yao ni kikubwa kuliko kiwango cha ajira zinazotolewa nchini. Hii imesababisha ziada ya vijana wasiokuwa na ajira ambao idadi yao inaongezeka kila mwaka. Kwa lugha ya kimahesabu wakati ambapo ajira zinaongezeka "arithmetically" idadi ya vijana wanaohitaji ajira imekuwa ikiongezeka "geometrically" na kusababisha ongezeko la vijana wasioajiriwa.
 
hey hivi huyu nape anapinga mradi kaongea au halijui tatizo, mamshangaa manake ukweli anao moyoni mwake. Ila minachoamini Mungu ni hakimu wa mambo yote. Mheshimiwa lowasa endelea kusema ukweli wazidi kuumiza vichwa hawa, na wanachadema msichoke kututetea wananchi wenu. MAGAMBA tumieni akili kutatua matatizo na sio kuyakimbia matatizo kwa visingizio. Hv magamba wake zenu na watoto wakiwaambia matatizo yao mtaishia kulalamika na kuyakimbia matatizo?
 
Nape badala ya kujibu hoja ya msingi na kupendekeza hatua zipi serikali ya chama chake ichukue kumaliza tatizo la Ajira kwa Vijana,yeye anatuletea majibu ya kijinga kwa kumshambulia mleta hoja! Wakati unatoa majibu jihadhari kuingiza hisia za chuki binafsi. Wewe ni msemaji wa chama chako siyo familia yako ama genge lako ktk CCM.
 
Nilichokurupuka ni kipi? au kwasababu nimepingana na hoja ya kuwaita vijana bomu kila siku? Na kisa kasema flani? Lazima umtukane nape na kumwita mbumbumbu ndio siku yako iende?... Serikali imetoa takwimu za hali halisi ya ajira nchini, nikatakiwa kutoa maoni, nilichojibu kuwa serikali iko sahihi, hali ya ajira nchini kwa takwimu sio maneno ya barabarani, na hasa ukilinganisha na nchi hata za Afrika mashariki tu Tanzania ni bora kuliko zingine, umbumbumbu wa Nape uko wapi?

Nadhani ni vizuri pamoja na kutakiwa kutukana kila unapokuta jina la Nape, akili za kuambiwa changanya na zako....

Umemaliza kuharisha nikupatie maji..
 
Nape, you are right. Huyu EL ni Mbunge. Ana forum Bungeni. Mbona hatujamsikia akitoa maoni/mapendekezo yake katika hotuba ya Bajeti y mwaka jana? Aache ubabaishaji huyu EL!
 
Nape, you are right. Huyu EL ni Mbunge. Ana forum Bungeni. Mbona hatujamsikia akitoa maoni/mapendekezo yake katika hotuba ya Bajeti y mwaka jana? Aache ubabaishaji huyu EL!

Kwani ni mara ya kwanza EL kuzungumzia sula hili. Amezungumza mara nyingi ila mnatetea upuuzi kwani watu wangekuwa na ajira gharama mnazozitumia leo kuhonga ili mshinde uchaguzi zisingekuwepo. Angalia nchi kama haina Rais wala Waziri Mkuu mambo madogo tu ya madaktari yalichukua muda mrefu kutatuliwa wakati ilihitajika busara ndogo tu. Kwa kweli anayetetea CCM namuona kama mwendawazimu imechoka, ikae kushoto ili ione mabadiliko.
 
Nape ni mtu mdogo sana hana ubavu wa kupambana na Lowassa, alichosema Lowassa ni kweli vijana ambao hawana ajira ni bomu.
 
Unafiki wa Nape ni upi? Kama kusimamia msimo wangu kuwa rasilimali za nchi lazima zifaidishe watanzania walio wengi ni unafiki, nina furaha kuitwa mnafiki..... Kama kwa kusema watu waache ufisadi na ulafi wa madaraka ni unafiki jina hilo linanifaa sana.... Haya mengine ya Arumeru Mashariki, najua ni hasira za kushindwa kutakakowakuta, na najua itakuwa aibu kubwa kwa magwanda, si vibaya mkitanguliza hasira zenu kwangu maana mie ndo punching bag.....
nikuulize Kijana mwenzangu Nape. ktk mwaka huu wa fedha ni sekta zipi zaidi ya sekta ya Elimu, Afya na Kilimo zilizoajiri? ina hata ktk sekta za elimu na kilimo ni watu wengi walio achwa. -Kama ni sekta hizo tafsiri fupi ni kuwa watu wanao hitimu vyuoni ni watu wanao chukua masomo ya ualimu, afya na kilimo tu? je wako wapi wanaosomea biashara, uchumi, takwimu, sanaa, na kozi nyingine ambazo wadau watanisaidia..... Nape we na serikali yako mmekuwa mkiomba watu wenye experience ya angalau miaka 3-5, je huyo n kjana aliyemaliza masomo atapata nafasi hizo? Ajira zinapotangazwa bila kuwa na jina kama lako linaloishia Nnauye(baba ako) huwez kpata ajira au uandae zaidi ya 500,000 sa utazitoa wp? mnachoniuzi ni mnaporundikiana vyeo wkt hata hvyoni source ya ajira, mfano mkapa ni mwenyekiti wa bodi mbalimbali bado kiongozi mkubwa wa udom, mwinyi,msekwa na wengine wengi. je kwa kuwanyang'anya hvyo vyeo mngegenarate ajira kiac gan? we uliniuzi zaid ck yamdahalo uliposema bado tuko kwenye ujamaa na kujitegemea, tangu ck hyo cna hamu na ww, bado ukazunguka kpiga kelele unapinga ufisadi wkt lowasa kila ck anakuchezea na ww kazi yako ni kufuata mkia....kama ni uwongo hebu twambie kama uriridhia siyoi kuchaguliwa kugombea ubunge arumeru. mbona sa hv unaleta unafk kwamba tsubiri arumeru hk hata ww mwenyewe hkupend. NAPE We utakuwa chini ya EL hata kama utapewa uwenyekiti wa CCM, EL anahesabu ktk chama hamna cheo kama chako, hapo upo kama kivuli tu na hakueshimu kama kiongozi wake hata kdogo. na waandishi wa habari wameishakuona kama Vuvuzera ndo maana insh akiongea EL wanakuuliza ili wazidi kuproovejinsi ulivyo mnafiki.
 
Lowaananchi na kidogo afanikiwewe kuwahadaa wananchi,Yeye ni fisadi na atabaki kuwa fisadi na sio kiongozi wa mfano,anahujumu waumini pamja n viongozi wake.Ni kweli Kikwete haongozi vema na hiyo haimaanishi kuwa fisadi mwenza aweza kuwa rais bora! Hivi jamani Lowassa anapambana na nani?
 
Sisi wote ni watanzania na tunaipenda nchi yetu na mbaya zaidi tumeshiriki kuiweka serikali iliyopo madarakani kwa namna mbalimbali kwa kadri tulivyojaliwa, na kwa msingi huo ningeomba sana mawazili wetu waache kukurupuka kwa majibu easy ktk maswali magumu, issue ya vijana leo huna sababu ya kujitetea kwa kulinganisha kitakwimu na nchi zingine, issue ni kwa nini un-employment, wakati tuna ardhi ya kutosha, maliasili, na mbaya zaidi wasomi wengi tena kama ni wachumi basi waliobobea? au Nape wewe huoni ajabu ktk kipindi kama hiki ambapo tumeweza kuwa na madaktari wengi na ongezeko la magonjwa, madawa mengi na maradhi yasiyotibika? magorofa marefu mengi yanayojengwa wakati watanzania wengi ni wafupi (kipato). ningeomba Nape TUJITAHIDI kuwa wakweli inapobidi ili hata wenzetu waweze kuona na kutoa ushauri tatizo la ajira ni issue very sensitive, na kwa hiyo ni lazima politacians kama wewe muweze kuliadress, na si kutumia fursa hii kama mtaji kwenu hasa katka kipindi cha kampeni kwa kuwakusanya vijana (kutumika).
 
Lowaananchi na kidogo afanikiwewe kuwahadaa wananchi,Yeye ni fisadi na atabaki kuwa fisadi na sio kiongozi wa mfano,anahujumu waumini pamja n viongozi wake.Ni kweli Kikwete haongozi vema na hiyo haimaanishi kuwa fisadi mwenza aweza kuwa rais bora! Hivi jamani Lowassa anapambana na nani?

Andika upya ueleweke. Kwani nani amesema Lowassa awe Rais, mambo mengine muda ukifika utazungumza wenyewe. Mataraji ya nani anaweza kuwa rais ni baada ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa Chadema mwakani kama Mbowe ataridhia kuachia uenyekiti na Slaa kuacha Ukatibu hapo sasa utakuwa na mwelekeo halisi wa siasa za 2015.
 
U DC nachingwea ulitengeneza ajira kwa vijana?mikakati gani ulifanya?maji-kahama,udom,sekondari za kata lowasa ww jee?
 
Mbadala wa viwanda KILTEX,MWATEX,SUNGURATEX,MUTEX,KIUTA,URAFIKI,UFI,TRC,NATIONAL RADIO,TANG PACKERS upo wapi kwavijana?
 
hivi kuna tathmini yoyote kuhusu zile ahadi ya ajira milioni 1 kama sikoseikwa mwaka kama zimetimizwa kutoka ktk ilani ya chama twawala lowassa na nape wakiwemo
 
Nape ni mtu mdogo sana hana ubavu wa kupambana na Lowassa, alichosema Lowassa ni kweli vijana ambao hawana ajira ni bomu.

Mkuu ritz ni ww au mtu kaiba password yako! Unapingana na bosi wako. Kweli nguvu ya umma kiboko
 
hapa tunadanganyana tu...hii nchi imeshakua KINGDOM na rulers wetu kama tunavo wajua ni "BOYS TO MEN"yani "RO-KI-LO"...tusubiri tu vijana wetu wenye uchungu na nchi waje baadae walete mabadiliko,ila kwa sasa ni BOYS TO MEN tu ndo watawala....wazungu wanasemaga "THEY HAVE MONEY AND THE POWER"...
 
Back
Top Bottom