CCM chalia rafu za makada, mahasimu
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeeleza kubaini kundi la watu waliojipanga ambao wanafanya kila jitihada ili kuhakikisha chama hicho kinasambaratika na kwamba siku chache zijazo kitawataja kwa majina hadharani.
Kadhalika, chama hicho kimesema hakuna mgogoro miongoni mwa viongozi wa juu wa CCM na kwamba kinachosemwa mitaani ni sehemu ya propaganda zinazoenezwa na kundi la watu hao.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipozungumza na waandishi wa habari na kwamba anawajua kwa majina watu hao wanaojitahidi kupandikiza fitina na kuwataka waache mara moja kufanya hivyo vinginevyo muda wowote atawataja kwa majina.
Mafisadi je? Hawafahamu kwa majina? mbona miezi mitatu sasa inakuwa miaka mitatu? Muda utakapowadia hata hao anaowaahidi kuwataja hatotimiza ahadi hiyo kwani bado wanadaiwa ahadi nyingi sana ambazo bado hawakuzitekeleza!!