Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,484
- 4,821
Hivi ni 'kamdhulumu' ama 'hajatekeleza ahadi yake'?......Hii nimeipata kutoka kwenye fainali za Maisha plus kuwa Nape ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi msimu uliopita alitoa ahadi kwa Mshindi,ambayo mpaka leo anampiga chenga kumpa zawadi hiyo
. Kweli ahadi za Viongozi wa CCM hazitekelezeki.
Maelezo zaidi...
KWENYE FAINALI ZA MAISHA PLUS leo Tar 18/05/2014...
MASOUD KIPANYA alimuuliza "ile zawadi" uliyoahidiwa na mgeni rasmi wa mwaka jana ulishapewa! Dada aliomba kupitia TBC kuwa "Mh.Nape ile zawadi uliyoniahidi mbona hujaitekeleza! Nimesumbuka sana ofisini kwako nakuta gari lako ila wasaidizi wako wananiambia haupo" Tehe tehe teheeeee!!!
Nnape Nnauye; Ritz; Faiza Foxy.
Binafsi nimemsikia huyo binti sijamsikia akizungumza suala la kudhulumiwa, bali kakumbushia ahadi aliyopewa na Nape....Na sina uhakika kama ukomo wa kutoa hiyo zawadi ulikuwepo ama la....
Siasa zisitupumbaze tukakosa hata ufahamu wa kutofautisha maana ya kudhulumu na kutotekeleza ahadi kwa wakati....