....
katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape Nnauye apatwa na majanga mkoani Iringa baada ya kuanguka na kuteguka mkono wake wa kulia wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya msafara wa Kinana na Veteran mjini Iringa.
Tukio hilo limetokea mapema asubuhi ya leo na hivyo kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
Mwembetogwa mjini hapa Nape ambae alikuwa amefungwa mkono wake alisema amepatwa na tatizo hilo leo asubuhi baada ya kuanguka uwanjani japo mbali ya kuanguka alisema hajaweza kuacha kupanda jukwaani kuwaeleza wananchi wa Iringa mjini juu ya mbunge wao mchungaji Peter Msigwa( Chadema)
Kwani alisema ni lazima mbunge Msigwa aondoke katika jimbo hilo baada ya kushindwa kuwatumikia vema wananchi wa jimbo hilo na kuendelea kuwaletea mabalaa mbali mbali .
Nape pia ametumia nafasi hiyo kutaja ahadi lukuki za mbunge Msigwa ambazo alipata kuwaahidi wananchi pasipo kuzitekeleza katika jimbo hilo.
[07:19, 10/13/2014] Masengo: News; Moto mkali wateketeza soko kuu la wilayani urambo mkoa wa Tabora. Moto huu ulianza majira ya saa nne usiku na bado unaendelea hadi asubuhi hii. Mali za mabilioni kadhaa zateketea na moto huo yakiwemo maduka makubwa yaliyozunguka soko hilo. Chanzo cha moto huo ni itilafu ya umeme ambapo wilayani urambo umeme una kawaida ya kukatika na kurudi mara kwa mara. Aidha wilaya hii haina hata gari moja la zimamoto.
[07:36, 10/13/2014] : Halafu wamekazana oooh msigwa hajaleta maendeleo lazima aondoke! Jimbo la sita hilo amekaa miaka zaidi ya 30 akiwa mbunge wa urambo mpk Leo hakuna gari LA zima moto.
Kweli inaingia akilini?
[07:36, 10/13/2014] CDM Chinga President: ilani ya ccm inaubaguzi inapeleka zimamoto kwa msigwa harafu kwa sita hapewi kumbe dawa ya maendeleo ni kuchagua upinzani✅
[07:38, 10/13/2014] : Kwa hiyo nape alisema msigwa lazima aondoke kumbe nimejua wakuondoka Ni serikali ya ccm ndio haijaleta maendeleo. Na sio msigwa