Nape ajikanyaga DW kuhusu kufungia Mawio na kuzuia matangazo ya bunge live

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Akihojiwa na DW amesema ni kweli sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ni mbovu na inapelekwa bungeni kuibadilisha. Alipoulizwa kwamba kama amekiri sheria hiyo ni mbovu ikiwa itafutwa na maamzi ya kulifungia Mawio yatabatilishwa kwa vile yalifanyika kwa kutumia sheria mbovu? Akasema sheria hata kama ni mbovu lazima iheshimike hivyo maamzi yatabaki pale pale.

Kuhusu bunge kurushwa live Nape amesema watumishi wa serikali walikuwa wakiiba muda wa kazi kutazama bunge. Alipoulizwa kwa nini hatua za kiutendaji zisichukuliwe badala ya kusitisha matangazo na kwa nini mwanzoni alisingizia gharama. Akajibu kwamba suala hilo si la serikali bali bunge "Kwanza hili suala si la serikali, bunge liliona ni kuna redio 125 nchi hii na wote hawawezi kuleta mitambo yao hapa hivyo wakatengeneza studio ambayo redio zote zinaweza kupata matangazo" alisema.

Alipobanwa kwamba kwa nini redio na Tv zilizo na uwezo wa kurusha moja kwa moja zilizuiliwa? Akajibu, mbona South Africa wanafanya hivyo na hakuna malalamiko? "Nchi nyingine kama South Africa inaonyesha masaa 8 live na baada ya hapo wanarekodi huko mbona hawalalamiki?
 
Hakunaga kitu nisichopenda maishani mwangu kama kuniambia mbona fulani anafanya..........naweza kumkata kibao mtoa hiyo kauli.......haya ss kama mfano wa kuigwa ni south Africa, basi tuige pia rais wao anavyohangaika na mashtaka mahakamani.
Acha zako wewe, hapo kafananisha tu na wala si kuiga kama unavyosema, mbona huwa mnalingalisha na kutamani uchumi wa china au kenya?
 
Hahah! Ni kweli mleta mada upo sawa! Alipokuwa anabanwa na hoja nzito anajibu majibu mepesi sana tena majibu yenyewe yapo nje ya anacho ulizwa! Nimeona aibu sana hadi ikanilazim nipunguze sauti ya radio! Nape angefaa awe msemaji wa simba aendane na speed ya Jerry Muro!
 
Akihojiwa na DW amesema ni kweli sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ni mbovu na inapelekwa bungeni kuibadilisha. Alipoulizwa kwamba kama amekiri sheria hiyo ni mbovu ikiwa itafutwa na maamzi ya kulifungia Mawio yatabatilishwa kwa vile yalifanyika kwa kutumia sheria mbovu? Akasema sheria hata kama ni mbovu lazima iheshimike hivyo maamzi yatabaki pale pale.

Kuhusu bunge kurushwa live Nape amesema watumishi wa serikali walikuwa wakiiba muda wa kazi kutazama bunge. Alipoulizwa kwa nini hatua za kiutendaji zisichukuliwe badala ya kusitisha matangazo na kwa nini mwanzoni alisingizia gharama. Akajibu kwamba suala hilo si la serikali bali bunge "Kwanza hili suala si la serikali, bunge liliona ni kuna redio 125 nchi hii na wote hawawezi kuleta mitambo yao hapa hivyo wakatengeneza studio ambayo redio zote zinaweza kupata matangazo" alisema.

Alipobanwa kwamba kwa nini redio na Tv zilizo na uwezo wa kurusha moja kwa moja zilizuiliwa? Akajibu, mbona South Africa wanafanya hivyo na hakuna malalamiko? "Nchi nyingine kama South Africa inaonyesha masaa 8 live na baada ya hapo wanarekodi huko mbona hawalalamiki?
Basi na sisi watuonyeshe live kwa masaa nane live kama wasouth. Hicho cheo alichopewa nape kimemzidi.
 
Hakunaga kitu nisichopenda maishani mwangu kama kuniambia mbona fulani anafanya..........naweza kumkata kibao mtoa hiyo kauli.......haya ss kama mfano wa kuigwa ni south Africa, basi tuige pia rais wao anavyohangaika na mashtaka mahakamani.
Mimi pia nachukia Sana mtu anayefanya comparison za kijinga, mwenye akili hawezi kusema hivyo.
 
Hakunaga kitu nisichopenda maishani mwangu kama kuniambia mbona fulani anafanya..........naweza kumkata kibao mtoa hiyo kauli.......haya ss kama mfano wa kuigwa ni south Africa, basi tuige pia rais wao anavyohangaika na mashtaka mahakamani.

Hoja mfu kabisa. Kwa hiyo kama una njaa na huna uwezo wa kununua chakula na jirani yako anaishi vizuri kwa kuwa ni shoga basi na wewe utaamua kuwa shoga?
 
Nchi hii kuna tatizo. Nape alituangaisha akiwa msemaji wa ccm....tukaona ubwege wake....tukaona upuuzi wa kila aina ikiwemo kutaka kuitumbukiza nchi ktk vita kwa 'goli la mkono'.....kwa upuuzi huo hakuna hata aliyewaza Nape kupata ubunge to jimbo la mtera. Bahati mbaya leo ni mbunge na waziri....kubalini haina yote ya ufidhuri atakaowafanyia...hata hakiwatuna na kuwabiga mpeni shavu apige....hamkujua tabia yake?...hamkujus ubabe wake na kiburi chake...hati mnamsikiliza Dw....hawspe majibu gani msiyojua kutoka kwa 'Nape
 
Back
Top Bottom