Nape Ajikana

Nape Ajikana

LICHA ya tambo za kuwaondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baadhi ya vigogo wa chama hicho wenye tuhuma za ufisadi kwa kutumia falsafa ya kujivua gamba, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amekana mkakati huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Nape alisema suala la kuwafukuza uanachama wanachama wake wenye tuhuma za ufisadi si la msingi bali chama kinajikita kuweka miundombinu itakayozuia masuala hayo kutokea.

Alisema kuwa chama kimejikita kwenye mkakati wa kuzuia mambo mabaya yasiendelea kutokea ndani.
?Hili ni chama kubwa linakaribia kuwa na wanachama milioni sita?wanakuwapo watu wana hamu ya kutoa rushwa, kununua uongozi, wanakuwapo watu wana hamu ya kupora rasilimali za nchi...hii ni sawa na kumchoma moto kibaka, unamchoma leo lakini kesho anatokea mwingine,? alisema.

Nape aliongeza kuwa njia sahihi ni kuweka miundombinu ya kuhakikisha watuhumiwa hao hawafanikiwi kufanya mambo hayo. Kwamba mjadala mkubwa usijikite kwenye kufukuza.

?Kufukuza pia inaweza kuwa njia mojawapo lakini adhabu peke yake inatosha? Leo nchi inayoongoza kwa adhabu kali ya rushwa ni China, lakini bado wala rushwa wapo,? aliongeza.

Akizungumzia tuhuma za chama hicho kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya wapinzani kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi mkuu mwaka 2015, alisema madai hayo ni uongo uliokubuhu.

Source: Tanzania Daima Leo

My Take: Haya ndo matatizo ya viongozi wetu kukurupuka. Nikikumbuka jinsi huyu jamaa alivyokuwa anatamba majukwaani na ajenda yake ya siku 90 kwa mapacha watatu nashindwa kuamini kwamba leo anaweza akakana.

DUH,KWA HIYO CCM WANATAKA KUTUAMINISHA KWAMBA YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO?[KIZAZI HIKI CHA DIGITAL?],NA KWAMBA GAMBALIZATION IMEKUWA CD ZILIPENDWA?HIVYO CD MPYA NI KUNUNUA MASALIA?KWA MAANA HIYO NDIYO NGIJANGIJA? Mtoto hana Baba.
 
Kwa hili Nepi amadhihirisha CCM na Ufisadi ni Damudamu pia Rushwa na CCM ni kama Baba na mtoto Kweli pesa ni noma alitoa siku 90 akasema 120 sasa hivi anakana kudadadeki 2015 ndo mtajikana vizuri
 
Alisema migogoro iliyopo ndani ya cdm inatosha kabisa kwa wao ccm kupata siri za ndani hivyo hawana haja ya kuwa na hiyo mitambo
 
Nape ni mwiba mchungu sana kwa chadema ndio mana anasakamwa
 
Ukitaka thred yako iwe na wachangiaji wengi hapa jf, taja jina la nape au mwigulu
 
Na bado tunamsubiri huyo katibu mkuu wake atueleze wla rushwa aliowaondoa chamani ikifika hiyo miezi sita
 
huyu mbulula kila akiongea ni afadhali ya jana.... PUMBA TUPU.NTAMUONA NAPE ANA BUSARA KAMA AKIKAA KIMYA..
 
​lowasa anachukua chama kwa ccm nape katafute wazazi wako hususan baba kuna utata na dna ninajitolea kukulipia kwa ajili ya dna yako pole sana kwa kukurupuka.
 
Back
Top Bottom