Nape Ajikana

Nape Ajikana

wikolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
800
Reaction score
271
LICHA ya tambo za kuwaondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baadhi ya vigogo wa chama hicho wenye tuhuma za ufisadi kwa kutumia falsafa ya kujivua gamba, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amekana mkakati huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Nape alisema suala la kuwafukuza uanachama wanachama wake wenye tuhuma za ufisadi si la msingi bali chama kinajikita kuweka miundombinu itakayozuia masuala hayo kutokea.

Alisema kuwa chama kimejikita kwenye mkakati wa kuzuia mambo mabaya yasiendelea kutokea ndani.
"Hili ni chama kubwa linakaribia kuwa na wanachama milioni sita…wanakuwapo watu wana hamu ya kutoa rushwa, kununua uongozi, wanakuwapo watu wana hamu ya kupora rasilimali za nchi...hii ni sawa na kumchoma moto kibaka, unamchoma leo lakini kesho anatokea mwingine," alisema.

Nape aliongeza kuwa njia sahihi ni kuweka miundombinu ya kuhakikisha watuhumiwa hao hawafanikiwi kufanya mambo hayo. Kwamba mjadala mkubwa usijikite kwenye kufukuza.

"Kufukuza pia inaweza kuwa njia mojawapo lakini adhabu peke yake inatosha? Leo nchi inayoongoza kwa adhabu kali ya rushwa ni China, lakini bado wala rushwa wapo," aliongeza.

Akizungumzia tuhuma za chama hicho kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya wapinzani kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi mkuu mwaka 2015, alisema madai hayo ni uongo uliokubuhu.

Source: Tanzania Daima Leo

My Take: Haya ndo matatizo ya viongozi wetu kukurupuka. Nikikumbuka jinsi huyu jamaa alivyokuwa anatamba majukwaani na ajenda yake ya siku 90 kwa mapacha watatu nashindwa kuamini kwamba leo anaweza akakana.
 
Kwa Nape wala sishangai, namfahamu kwa hata wadogo zake na baadhi ya ndugu zake huwakana hadharani!
 
Nape kazoea kukana,hukumbuki alishakana kuhusika na CCj,nashauri kumpuuza maana hajitambui.
 
Anaona fahari sana kula matapishi yake!
 
Jamani pamoja na Nape kuweka picha ya kumwagilia kaburi la baba yake inaonyesha alikwenda peke yake bila ndugu zake...ndani ya ukoo wa Nnauye hatambuliki....!!
 
"Hili ni chama kubwa linakaribia kuwa na wanachama milioni sita…wanakuwapo watu wana hamu ya kutoa rushwa, kununua uongozi, wanakuwapo watu wana hamu ya kupora rasilimali za nchi...hii ni sawa na kumchoma moto kibaka, unamchoma leo lakini kesho anatokea mwingine," alisema.
Source: Tanzania Daima Leo

My Take: Haya ndo matatizo ya viongozi wetu kukurupuka. Nikikumbuka jinsi huyu jamaa alivyokuwa anatamba majukwaani na ajenda yake ya siku 90 kwa mapacha watatu nashindwa kuamini kwamba leo anaweza akakana.

Talking of QUANTINTY and not QUALITY
 
Kwa Nape wala sishangai, namfahamu kwa hata wadogo zake na baadhi ya ndugu zake huwakana hadharani!

Kukana imo kwenye GENES zake na ndio maana hata hao watoto wa Mwanaisha wanamkana kuwa yeye sio mtoto wa Moses Mnauye!!
 
:confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:

Nabotama na suki elingaka ngai te mino nazui na mokili ya nzambe nasala nini bafuti ngai ngai na monnaie?
 
Kumbe unaonjelea habari za Nape,mimi nilifikiri unaongelea habari za mtu ambaye ana akili timamu!
 
Dah! Hii nafasi aliyepo NAPE ni muhimu sana katika chama, sasa kama anavuluga mambo atakua anajimaliza yeye pamoja na chama pia.
 
:confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:

nabotama na suki elingaka ngai te mino nazui na mokili ya nzambe nasala nini bafuti ngai ngai na monnaie?

sei proprio figlio di mignota!!!!
 
Alisema seku ile kwenye mkasi kuwa zamani alikuwa anapenda kuongea ukweli ila wenzie wakamwambia siasa haziwi hivyo so now amejingiza kwenye mtandao wa waongo ambao ni pamoja na wazindiki na mafisadi. so keshaharibika huyu kijana.
 
Naomba kuuliza,Je kuna mwanasiasa Mkweli? Au ili uwe mwanasiasa lazima uwe na degree moja au mbili za kujua kusema uongo? Inatisha
 
Back
Top Bottom