Napata shaka kwa mambo yanayoendelea ndani ya CCM

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,946
2,929
Wakuu saalam!

Mimi ni mgeni jukwani, naomba ushirikiano.

Niende kwenye mada.

Nikirudi kifikra mpaka mwaka 2015 kwenye uchanguzi mkuu, tuliona utitiri wa watia nia, ikaitwa demokrasia.

Baada ya pale tukaanza ona vituko vingi, vichinjio Mara wengine wakawekwa korokoroni wakati wengine wanaendelea kutembeza vinjio kwenye mkutano mkuu.

Haikutosha mara paap, asiyetarajiwa akaokota dodo chini ya nguzo ya Tanesco.
Tukaona Lowassa kahamia upande wa pili.

Haikutosha, Lowassa akizindua kampeni kule Arusha, tukamuona Msukuma na chopa akishuka kumsaidia Lowassa kuzindua kampeni huku akiwa bado CCM, ilikuwa viini macho na mengine mengi.

Tia maji tia maji 2020 hii hapa, tumeanza ona vituko vingi. Toka mwaka jana mara sauti zimesikika kwenye mtandao wakimsema mkuu, haikutosha baadhi waenda piga magoti kushika miguu ya mkuu.

Wengine wakagoma, waitwa kwenye kamati.

NAPATA SHAKA NA HOFU KUU, isije ikawa vituko vyote hivi ni mapishi ili kuwapoteza wapinzani waone kina Membe, Kinana na Makamba watawapa nguvu za kushinda uchanguzi mwaka huu kama ulivyokuwa kwa Lowassa.

USHAURI KWA WAPINZANI:
Acheni kuchukua wanasiasa toka CCM, watengenezeni watu wapya ili kujenga Imani isiyo tindika kiupinzani.

Vijana wapo wengi Tena wasomi wakubwa.

KARIBU TUJADILI.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂😂 hapo tu ndipo naipendea jf mara paaa katikati ya mstimu mtu anaondoka na embe dodo, ok yote kumi sawa ila kuna hitaji watu makini sana na wenye jicho la mbele zaidi kuyajuwa haya
 
IMG_20200211_204603.jpg
 
Yanayoendelea kwa sasa kwa taifa letu Ni uasi dhidi ya utawala Wa sheria.mbaya zaidi kila MTU anaangalia tu.
 
Mkuu karibu jamvini. Ila haraka ya kuingia jamvini ikakufanya usahau some details. Kwamba King Msukuma alitua kwa chopa kwenye uzinduzi wa kampeni za Mzee Lowassa akiwa ametoka CCM? Ebu fanya editing hapo.
 
Umefikiri mbali,hali ya amani inatoweka taratiibu viongozi wakubwa wastaafu wangali wakiangalia na wasitie neno wakati hawana cha kupoteza.
Chaguzi zimeporwa na chama,hakuna anayesema chochote.

Upinzani unakandamizwa waziwazi,wanaona watanzania hatuelewi.Nchi haiwezi kwenda kibabe kiasi hicho.hiyo miradi mikubwa haiwezi kuwa mwavuli wa kujifichia,kwasababu hata taratibu za kuipata hiyo miradi nayo inahitaji uchunguzi huru,kwakuwa ni mzigo mpya wa madeni kwa walipa kodi.
Muda utasema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom