ContinousImprovement
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 290
- 268
Members ya JF Nawasalim.
Mimi ni kijana. Umri wangu haujavuka miaka 30. Naomba Ushauri wenu katika hili....
Kwa kipindi kirefu nimekuwa kwenye jitihada binafsi za kubadilisha sehemu kubwa ya tabia zangu ambazo mimi mwenyewe ninaziita "mbaya" lakini changamoto kubwa ni kuwa sijafanikiwa. Bado najiona nipo vile vile.. bado najiona ni mtu anaehitaji kujifunza mengi na kubadilisha mambo mengi.
Mfano, Nina kazi ambayo namshukuru sana mwenyezi Mungu. Maana naona ni muujiza mimi kuipata. Kazi hii japo nilianzia ngazi ya chini kabisa "Volunteer" niliipata hata bila kuwa na vigezo sahihi kielimu ukiachilia "experience" ambayo nimeipata hapa hapa ofisini na ni majuzi tuu ndio nimefanikiwa kupata cheti sahihi cha shule. Na bado nasoma.
Kama ilivyo ofisini na nyumbani. Changamoto kubwa nayopitia ni kushindwa kwa asilimia kubwa kupanga mambo yangu. Sehemu kubwa ya maisha yangu kwa kila siku imetawalwa na "Frustrations". Iam always late.
Japo ninamshahara Mzuri, lakini nina madeni karibu nusu ya mshahara wangu. Na hii imetokana na ile tabia yangu ya kutaka mabadiliko ya haraka baada ya kujiona nimechelewa na hivyo kuanza kufanya vitu ambavyo naviita vya kimaendeleo kwa haraka na kupelekea kujikuta naingia kwenye madeni ambayo baadae nimekuja kugundua kuwa, nayalipa kwa miezi mingi sana. Kiasi kwamba hata kabla sijamaliza kuyalipa linatokea lingine ambalo kwa kujitizama nafasi yangu na mshahara wangu, naona nilipaswa kuwa nalo miaka mitatu au miwili iliyopita. Hapo nitafanya kila namna nipate pesa ninunue....
Tizama hii. ......
Nimefanya kazi miaka mitano sasa. Lakini sasa ndio nimemaliza mwaka tokea nitoke nyumbani na kwenda kupanga"
Ndani ya mwaka huo huo mmoja ambao hiyo miaka minne nyumbani sikuwahi kuwaza wala kuweka hakiba ya pesa kwaajili ya kujakujitegemea. Niliwaza tuu kisha siku moja nikaamka nikatafuta mahala pakukaa nikalipa kodi na kuhamia. Hata nyumbani siku aga..... habari hii ni ndefu.
Kwa kifupi napata wakati mgumu sana kupanga na kutimiza mipango yangu. Mambo mengi ambayo nayaona ndio ya msingi sifanyi. Tatizo kwangu ni nini? Na ni vipi nitaweza kujitoa hapa nilipo? Kila siku mimi ninaanza. Sijawahi kuendelea. Sijawahi kuyafikia malengo yangu.
Vingi nilivyonavyo naona kama sikuvistahili.... hasa nikijiangalia tabia zangu na matendo. Kwanini najidharau? Kwanini naona kama sikuvistahili? Nje am very respectful lakini ndani najiona ni mtu mwenye changamoto kubwa ya kujibadilisha na kuwa aina ya mtu ambae siku zote nimekuwa nikitamani kuwa.
Napenda kuwa mtu wa mazoezi, napenda kuwa na mwili wa kimazoezi. Napenda sana kuwa msomi hasa niliyebobea kwenye masuala ya manunuzi. Napenda kuwa mcha Mungu wa kweli na sio mnafiki. Nisizini huku nikimsifu Mwenyezi Mungu, niseme uongo, nioe Mke Mmoja. Tujaliwe watoto. Nijenge nyumba ya kuishi na familia yangu. Niwepo kwaajili ya Familia yangu, Ndugu zangu, marafiki na Jamii inayonizunguka. SITAKI KUWA WALA KUSHIRIKI UNAFIKI.
Changamoto kubwa ni vipi nitayaweza haya yote kwa Matendo? Kila napopanga. Asubuhi naamka na kupangua. Ya Msingi nayasogeza "Kesho" ambayo sijawahi kuifikia.
Am breaking down. Am worried. How do I survive this?