Napangisha Frem yangu na Biashara yake ya Chips

Mjasiriamali M

Senior Member
Jan 15, 2013
142
71
Habari za Leo Wakuu,

Husika na Somo Tajwa Hapo Juu, Nna Biashara yangu Ina Run ipo maeneo ya Tandika Magorofani Karibu na Chuo cha Bandari pamoja na Chuo cha Utalii pembeni Mwa Hospital mpya. Eneo ni Zuri kwa Biashara. Nimekosa Usimamizi mzuri wa hawa Vijana wangu, Hapo mwanzoni tulikuwa tunaenda sawa maana niliwaachia wajiendeshe wenyewe mimi nachukua MALENGO(Hesabu) ya siku, kwa miezi miwili ya Awali hili lilifanikiwa kwani nami nilikuwa sichezi mbali na Eneo la Tukio, sasa kadri muda unavyokwenda nami kubanwa na Shughuli nyingine nakosa Ukaribu nao, hapa sasa Nimeanza Kupigwa Kiswahili, Mara Biashara Ipo ila Hela Hakuna mara CHUMA Ulete n.k.

Kwa sasa nimewaambia wapumzike kama wiki tuone tunafanyaje, swala la kutokuwepo mwenyewe ndo linanipa Head Ache, sasa nimeona niuze Vitu vilivyo katika Eneo langu kuanzia Kabati la Chips(Fut 2x1) , meza za square 3 na viti 10, makarai, meko, n.k. then frem nimkodishe mtu anipe kodi yangu au lah kama mtu ataweza kuiendeleza hii Biashara basi nimuuzie yeye anipooze nimuachie chumba na vifaa vyote.

Baadhi ya Vitu nimevionesha kwenye Picha, Frem Ipo Inatazama Barabara na Kuna Parking Kubwa ya magari na eneo linatumiwa sana na Wanafunzi wa Vyuo Hivi Viwili maana kuna Miti ya Vivuli. Kama Utapenda kununua vitu au kupanga tafadhali tuwasiliane na picha zaid zipo ntakusendia kwa whatsapp.(0719447204)

Kodi ya Pango ni Elfu 85 kwa mwezi, Umeme Huwa ni Around elfu 35-40 kwa mwezi. Access ya maji na usalama ni wa uhakika.

Natanguliza Shukrani.
20150824_143337.jpg 20150824_143351.jpg
 
Orodhesha vitu ulivyonavyo vyote na bei yake, naweza amua kitu.

Viti 10, Meza za Plastic 3, ya Mbao Moja, Kabati la Alminium, makarai mawili, Jiko la Pumba na la Mkaa, Jiko la Mishkaki, sahani, fraying pan 2, ndoo na vitu Vidogo Vidogo.

Jumla ya Vyote Ni 400K.
 
Mkuu laki tatu vip@?, hebu nipe mtazamo wako, kama vip mimi nikufate hapa ulipo.
Mkuu leo wamekuja wadau wawili kupaona wote wameonesha Interest ya Kuendelea na Biashara, 300k ni nyingi ila nahisi hawa majamaa wamekuzidi Dau. Asante kwa Interest zako.
 
unauza au unapangisha
km ni k 4 ndo kodi ya mda gani
Kod ni Miezi 6. waliokujaleo nimewapa option ya kujaribu biashara kwa mwezi mmoja then atakayefanikiwa atasema kama anaendelea au la, so ntachukua kodi ya mwezi plus hela kidogo ya kutumia vifaa vyangu vyote kama 240k hivi per month.
 
Back
Top Bottom