Naota navamiwa na majambazi au wachawi

Gily Gru

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
7,802
20,763
Wasalaam

Usiku wa kuamkia leo niliota nimevamiwa na majambazi, nikaamka kuangalia saa ni saa tisa na dakika nne usiku. Nikatoka sebuleni nikaona mtu ananifanyia ssssssssssssshhhh kuashiria nikae kimya nisitoe sauti cha ajabu ila huyu mtu anafanana na Steven Seagal (sura yake) ghafla ile sura ikabadilika ikawa yangu. Mtu Yule (ambae sasa ni kivuli changu) gizani aliniashiria nizime taa nijifiche nisionekane. Kweli nilizima taa nikajikita niko mwenyewe sebuleni nikachukua filimbi nikaipuliza majirani waje kunisaidia. Nikashtuka kutoka usingizini koo kavu sana limekauka nikanywa maji nikarudi kulala nikiwa na simanzi sana. .

Kwa nini nilipata simanzi?
Nimepata simanzi kwa sababu ndoto za aina hii nimeshaota mara nne au tano hivi. Tofauti na jana nilipata kufanya maamuzi, wakati mwingine nafadhaika kwa sababu naona kuna watu nje wanachungulia dirishani ila mwili unakuwa mzito kuamka. Naweza ota majambazi au kuna mchawi anachungulia dirishani ila sasa ili niamke kujihami mwili unakuwa mzito nashindwa kuamka kabisa kitandani (bado niko usingizini). Nikishtuka usingizini nakuwa nimetoka jasho sana. Kuna muda nikiwa ndotoni na sasa nimevamiwa na majambazi unakuta natamani kupiga kelele ila sauti haitoki kabisa. Naweza piga kelele kuomba msaada ila sauti haitotoka kabisa no matter how much I scream. This has gotten to me deeply and it’s affecting my sleep and sanity. Is there a meaning behind this or it is just a nightmare? fYCK

Nahitaji msaada wa ufafanuzi au ushauri I am terrified.

rioboWFA9m6Wzkg3c2ZZBqDL2YS1f7.jpg


Nashindwa hata kula
E9ATx40UUAMMkGr.jpg
 
Kama unalala sehemu ya hivi lazima uote unataka kubakwa

On serious Note:
Angalia ventilation system ya unakolala yaani madirisha na kiwango cha Oxygen kinachoingia.
Angalia godoro unalotumia linaweza kua sababu. Acha kula Ngarerumo, Mseto na makande usiku
Pia uwe una omba kwa imani yako kabla ya kulala
FB_IMG_16669986401277002.jpg
 
Kama unalala sehemu ya hivi lazima uote unataka kubakwa

On serious Note:
Angalia ventilation system ya unakolala yaani madirisha na kiwango cha Oxygen kinachoingia.
Angalia godoro unalotumia linaweza kua sababu. Acha kula Ngarerumo, Mseto na makande usiku
Pia uwe una omba kwa imani yako kabla ya kulala
View attachment 2590890
Nitake radhi nalala nyumba safi sana😃
I could put pictures of my house 🏠 uone ina ventilation system ya kuingiza hewa safi but that's not the issue😃
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom