Naondoka,nikionekana Mods nipigeni ban!!!

Naondoka,nikionekana Mods nipigeni ban!!!

Haya mandieta ramadhani kareem!
Ameen!
Nawe pia nenda kamche mola wako na inshaallah allah atakupa afya njema ktk mfungo ili uweze kutimiza nguzo hii muhimu ya dini.
 
Wakati mwingine natamani Allah angekuwa aliagiza miezi mitukufu iwe 7 kwa mwaka. Haijalishi kama hiyo mingine mngeambiwa mle chakula. It seems amani inakuwepo kwa sana miezi hii.
Sio saba, iwe 12 kabisa
 
Tayari mwezi umeandama.
Mwenyezi mungu atupe uhai Inshaallah tutaonana baada ya ramadhan.
 
Nimekuelewa vizuri ndugu Mandieta, it seems uwepo wako humu JF mara nyingi umepelekea wewe kufanya mambo ambayo ni makatazo kwa Mwnyezi Mungu hivyo unaamua kuepuka/kujiepusha na shari. Kama ndivyo basi upo sahihi lakini mimi mzee wa siasa na habari mchanganyiko nitaendelea kuwepo jukwaani Inshallah mwezi mzima huu.

Kila la kheri ndugu yangu na ALLAH atufanyie wepesi katika kutimiza nguzo mojawapo muhimu katika dini yetu.
RAMADHAN KAREEM.
 
Huna kasheshe, funga yako sisi sidhani kama yatuhusu!
 
Ili kuhakikisha kwamba mwezi mtukufu unakua salama kwangu na kwa members wengine wa jukwa hili,naondoka kwenye jukwa hili kwa muda na ntarudi baada ya mwezi wa ramadhani kwisha inshaallah!

Na nikionekana nimerudi naomba Mods mnipige ban ili kuninusuru na kuharibika kwa swaumu yangu na ya member wengine.

Sipo tayari kupata au kumsababishia mtu ban ambapo inawezekana ata swaumu kwa mfunguji ikaharibika kwa sababu za kisiasa.

Wabilah tawfiq.
Aslm aylkm.
1. Ina maana JF kumejaa maovu na dhambi za kila namna!!!!!!
2. Ukifunga mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa minajiri ya kuweka dhambi na maovu yako pembeni, ukijua fika kwamba baada ya mfungo huo utarudia kuenenda/kutenda mambo yako kinyume na maadili basi hapo utakua ujafunga
 
Mbona ukuaga wakati wa vunja jungu??anyway
ramadhan kareem
 
utakatifu wa msimu, kwa hiyo baada ya mfungo kwisha ni full kujiachia hadi mwakani tena???!!! ENYI WANAFIKI MUNGU HADHIHAKIWI.
 
Swaumu huweza kuharibika iwapo mfungaji atafanya yafuatayo:
1: kula ama kunywa kwa makusudi baada ya kuchomoza kwa jua.
2: kuingia ama kuingiliwa kimapenzi kwa makusudi baada ya kuchomoza kwa jua.
3: kutoa mbegu za uzazi/ kwa makusudi baada ya kuchomoza kwa jua.
4: kuharibu funga ya mwingine kwa makusudi.
kwa hiyo ndugu zangu kuingia jamii forum ukiwa na nia njema hakuwezi kuharibu funga ya mwislam awaye yote yule. kawadanganye watoto wenzio.

Sijui kwa nini Uislam unashabikia Uzinzi kwa mlango wa nyuma! Ona namba 2 na 3! Uislam ni Mtihani kwa kweli
 
Back
Top Bottom