Naondoaje vinyongo/hasira moyoni mwangu?

Chuki ni huleta mawazo ya kishetani yanayoweza kuleta maafa makubwa jambo la msingi ni kupiga goti kwa Mungu mueleze unavyojisikia na jinsi binadamu mwenzio alivyokutenda sio ngumu kuamini Mungu anajua kesho yako na ya huyo unaemuona ni adui wa furaha na amani moyoni mwako..msamehe msogeze karibu usijali mapungufu yake anaeza kusema umejipeleka lakin wakati huo wewe unatibu majeraha yako Mungu atakusaidia katika hilo na utarudishiwa amani na upendo kwa huyo ndugu yako!!!!
 
Pole sana Bro. Its happens.

Hasara ya kwanza... KUTOKUSAMEHE ni sumu unayokunywa wewe huku ukitegemea fulani afe? Who is going to die anyway?

Napendekeza yafuatayo:
1.
Kaa utafakari.. All these years umembeba dadayako, Ni nini umepata, au utapata nini? na usipomsamehe utapata nini au utalipwa nini na nani na lini na kitaweza kurudisha maumivu yote unayopitia.. japo hamna faida yeyote.
2. Mtafute ukae naye umueleze A-Z na namna ilivyokuumiza na namna unavyotamani atambue kosa lake myamalize.
3. Nenda kaa sehemu private yenye utulivu hata kama ni chumbani kwako, Then mwandikie barua ukieleza mwanzo mwisho na ukimtangazia msamaha.. ukimaliza chukua hio barua uichome kama ishara ya kuachilia. Ukijisikia kulia lia, vyovyote vile usijizuie.. linapokuja swala la moyo kuna mengi.
4. Kwa muda wote huu unapomuweka moyoni.. unafikiri yeye anaathirika kiaje? naye akiathirika unafaidika na nini au umeshafaidika na nini so far?
5. je ukimsamehe unafaidika na kipi? (Furaha, Amani, upendo, udugu etc) Kumbuka hivi visa vya kusingiziwa uchawi n.k ni vya kawaida sana huku africa.. na ni familia chache sana ambazo hakuna muathirika wa hili jambo.. na sikweli.. bali ni hisia tu au shetani anawatumia kuvuruga mji/familia... (My best guese)

All the Best kaka.
 
kama wewe huwa unasamehewa basi kumbuka na wewe una jukumu la kusamehe wengine.
Unachotakiwa kufanya muite ongea nae jinsi unavyoumia kwa yale aliyoyatenda. halafu
mwambie kuanzia sasa umemsamehe. hakika utakuwa umeonyesha ukomavu. achana na
mipango ya kulipa kisasi kwa kuchoma na pasi, maana utajiongezea matatizo halafu kila
mtu atakucheka kwa uamuz wa kijinga uliofanya.
 

Thanx for tha advice. Umesema yaliyo kweli. Be Blessed.
 

Nimesoma ur post machozi yananitoka...... Thanx a lot for ur advice. Hamna kitu kinauma kama uenezewe maneno machafu ambayo si ya kweli nd people just keep pushing u down....much less anayefanyiwa hvyo ni mzazi wako unaye mjali sanaa. Anyway Mungu atalipa.
 

Mkuu honest me ni siwe muongo, kwa upande wangu ni bora ucheze na mzee wangu ila si mama nw nina miaka zaidi ya 30 ila huyo kama angekuwa ndugu yangu hakuna rangi angeacha ona kwa kweli.
 
Mkuu honest me ni siwe muongo, kwa upande wangu ni bora ucheze na mzee wangu ila si mama nw nina miaka zaidi ya 30 ila huyo kama angekuwa ndugu yangu hakuna rangi angeacha ona kwa kweli.

Nlishawahi mtia kibano hatosahau maishani mwake...since then najiepusha nae. Kimya jibu la mjinga.
 
Samehe mara sabini.
Mshirikishe Mungu kwa njia ya sala.
 
Haaaa mie ni muhanga pia ila nachofanya ni kukuepuka na kutokusemesha kwa lolote na siku ukijileta utafrai na shoo na bado sitaki kuchangamana naye. Adui wa baba yako (baba as mzazi) ni adui yako kamwe hawezi kuwa mwema kwako na kizazi chako.
 

Mkuu I had the same case nilipokuwa mdogo mpaka Leo simtamani kumuona alienifanyia ingawa ni miaka 15, sikulelewa na wazazi wangu tokea 6 yrs na nilikua mbali nao, kama miaka 8 kupita, ukatokea msiba wa mtoto wa baba yangu mkubwa aliekuwa ananilea kipindi hicho, so tukasafirisha msiba back to home, tumemaliza so tukarudi home ( kwa wazazi wangu) hapo nina 13 yrs, tuliondoka ndugu wengi tukaja nyumbani, nilikua na furaha ya kuonana na ndugu zangu nilowaacha na wale walokuja kuzaliwa baadae. Wakapika home tunajiandaa kula chakula as a family,( mama na baba hawakuwepo) baba yangu mdogo alinivaa ghafla na kunichapa na waya mgongoni bila kosa akanifukuza nisile na chakula ( kumbuka hapo ni home ni Mara ya kwanza baada ya kutokuwepo miaka 8) kile kitu kiliniuma hadi kesho nilimchukia! Ninamchukia! Nitamchukia! Baada ya hapo sijawahi onana nae tena miaka kama 16 ivi, kipindi hiki chote nimejitajidi nimsamehe lakini roho inakuwa ngumu coz hajawahi nieleza, kwa nini alinichapa bila kosa, alininyima kula jasho LA wazazi wangu, angeniacha japo nizoee kidogo, why 1st time home anifanyie vile, hapendwi hadi na ndugu zangu kwa sasa! Hope kumsamehe hadi anicomfont ye mwenyewe, anijibu hayo maswali kwa ufasaha labda ninaweza nikamwelewa, otherwise tuonane patakapostahili!!!
 

Nakuelewa sanaaa....Yan kuna watu wana mambo ya ajabu kweli. Mi sikufichi na ukubwa huu mtu akinitibua kihivyo awe mjomba au baba mdogo walahi nakwambia mbona tutazichapa, ntamvumilia kwa mara kadhaa akizingua nalianzisha wasinichoshe....namuogopa nani ??

The only people siwez argue nao ni my parents only, Heshima kwa mzazi wako aliyekuzaa ni kitu muhimu sanaaa they are the only ones who give a f*ck about me.

Sitambui ndugu mwingine mm. Kuna baba yangu mdogo flan alikua na tabia ya kuja home na ku command command wakati wazee hawapo tukiwa watoto....kwa akili zangu nikiona jambo ni la ki fal.a fal.a nlikua simuheshimu au kumsikiliza atapiga atatukana lakini sifanyi.

Nikamwambia utapiga utaniua lakini sifanyi.... Mpaka leo na utu uzima huu anajua kabisa sim feel au kumheshim kivile na hawez nifanya chochote ni salamu tu mazoea na watu wa ajabu ajabu sitaki.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…