Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,056
- 1,868
- Thread starter
- #41
huenda tatizo lipo kwako.
- unajisikia wewe ni mtoto wa kiume ndio maana baba yako anakupenda zaidi ya wengine.
- unaamini baba yako hana maamuzi yake pasipo kushawishiwa na "mama wa kambo"
- unadhani kwa vile umesoma kuliko wengine basi mambo yako yatanyoka kuliko wao.
kama niko sahihi kwa hayo niliyosema hapo juu nakushauri uanze kufanyia kazi yafuatayo
- amini kwamba baba yako anakupenda kwa vile ni mwanae na si kwa sababu wewe ni mtoto wa kiume
- mdhihirishie baba yako kwamba unawapenda nduguzo na utashirikiana nao siku zote. hii inaweza mfanya abadili
mawazo yake kuhusu mgawanyo wa mali zake
- tambua kwamba kusoma ni muhimu japokuwa sio uhakika wa mambo kukunyokea maishani. wapende nduguzo
bila kujali elimu yao.
hata hivyo nikupe pole kwa changamoto ulizopitia. nakuombea baraka na mola akuonyeshe pale ulipokosea ili uweze kupanyosha na pale ulipokosewa ili paweze rekebishwa.
Naomba nieleweke Mimi sina shida ya mali ninachotaka ni kupata ushirikiano na familia.