Naondoa upendo rasmi kwa mama yangu wa kambo

Naondoa upendo rasmi kwa mama yangu wa kambo

Fanya kazi zako kwa bidii, na usiwe na kinyongo na yaliyotoke. hii dunia tunapita tu mambo ya urithi ni ubatili tu.
 
Hivi vimali vya urithi ndio vinavyowafanya vijana wa DAR kubweteka vijiweni huku wakingojea wazee wao wafe ili warithi hivyo vibanda.....tena vibanda ni vile vya dizaini ya mbavu za mbwa.....miaka inakatika na wazee wanadunda tu.....hatimaye miaka arobaini inamkuta mtu bado anakula ugali wa kengele tu.....hatimaye vijana kutoka mikoa mingine wanaojituma hapa mjini kwa kuyasaka mafanikio wanawabebesha taka na kuwachimbisha mashimo ya vyoo kwenye ujenzi wa majumba yao ya kifahari na kuwanunulia sigara na viroba.....huku wenyewe wakiwa hawana cha kujivunia kwenye maisha yao zaidi ya uzawa......
 
Hizo mali ni za baba anazigawa kadiri anavyoona inafaa.

Piga kazi tafuta zako badae nawe uje uwagawie wanao, waswahili walisema "mtegemea cha ndugu ............"

Nakutakia mafanikio katika harakati zako lakini pia chuki haijengi.
 
kaka uzuri umeshawajua rangi zao zote
nakushauri ishi nao kwa tahadhari sana ndugu zako
tena usijilazimishe wakupende ht kidogo hao wabaya sana
we cha msingi mradi una pakuanzia pigania vya kwako
wasaidie unapoweza hizo mali kitu gani bwana
utapata tu tena za kwako mwenyewe za jasho lako zinanoga hatariii
achana na msaga sumu huyo anajishtukia mana anajua watoto wake sifuri so anajiwahi

kua nae makini huyo israeli bro
 
Jambo lakushukuru huyo mama hajakuua,.chapa lapa fanyayako.
Familia zenye watoto wengi wasio wa mama mmoja hazina upendo wakweli,.narudia tena hazina upendo wakweli,.tena hzo Mali zisingegawiwa mapema huwenda nawewe ungekua miongoni mwa wenye kudai kwa fujo.
 
kaka uzuri umeshawajua rangi zao zote
nakushauri ishi nao kwa tahadhari sana ndugu zako
tena usijilazimishe wakupende ht kidogo hao wabaya sana
we cha msingi mradi una pakuanzia pigania vya kwako
wasaidie unapoweza hizo mali kitu gani bwana
utapata tu tena za kwako mwenyewe za jasho lako zinanoga hatariii
achana na msaga sumu huyo anajishtukia mana anajua watoto wake sifuri so anajiwahi

kua nae makini huyo israeli bro

Asante ndugu
 
Urithi gani tena mkuu wakati umepatiwa elimu, tumia elimu uliyoipata kutafuta mali siyo kuwazia mali za mzazi tena.
 
Asante ndugu
nna situation km yako but i know how to play with their tunes
i dont give a damn about them na ninawasomesha mimi ktk kila hali
but in returns siwezi kuandika all i can say
MUNGU nipe uwezo huu kidogo tusije kutetereka mi na mdogo wangu wa tumbo moja kwa sababu wale najua wako kwangu kimaslahi tu
 
washukuru wazazi wako kwanza maana unajua kusoma na kuandika bila shida, sasa tafuta mali zako mwenyewe achana na za wazazi...
 
hahahahaha ndugu yangu ulitaka urithi gani zaidi ya huo ulionao(kizaz hiki cha DOTCOM urithi wetu elimu)..........bora ukose mali upate akili
 
Mimi ni kijana nina ndugu zangu tunakutana kwa baba ambao ni 7 wakike 5 wanaume ni 2 mimi mama yangu amefariki nikiwa na miaka 5 nimelelewa na ndugu tofauti.

Nilipofikia umri wa kuanza shule baba yangu alinichukua ili niwe nae karibu,lakini mateso niliyokuwa nayapata kwa huyu mama hayaelezeki.

Baba yangu alikuwa ananipenda kuliko watoto wake wote kwa sababu ndio nilikuwa mtoto wake wa kiume mkubwa.Nilipofika darasa la nne baba yangu mdogo alinichukua baada ya kuona mateso yamezidi na pia baada ya mkewe kumshauri kufanya hivyo.

Kwa kweli pale kwa baba yangu mdogo nilikaa kwa raha yule mama yangu mdogo alinilea kwa upendo wote,nimesomeshwa mpaka namaliza chuo,kwa kweli mungu amuweke huyu mama ili afaidi mafanikio.

Lakini nikaamu kurudisha mahusiano kwa mama yangu wa kambo na ndugu zangu si unajua damu nzito.Lakini kitendo alichofanya huyu mama ndicho kinachokata mahusiano rasmi mimi na yeye.

Kwani amemshawishi baba yangu kagawa mali kwa ndugu zangu bila kunishirikisha mimi
.
kwa kweli imeniumiza sana,nimemueleza mama yangu mdogo kwa kweli machozi yamemtoka.

Ushauri je nifanyaje na pia mimi ndo nimepata bahati ya kusoma ndugu zangu wote wamekataa shule.

huenda tatizo lipo kwako.
- unajisikia wewe ni mtoto wa kiume ndio maana baba yako anakupenda zaidi ya wengine.
- unaamini baba yako hana maamuzi yake pasipo kushawishiwa na "mama wa kambo"
- unadhani kwa vile umesoma kuliko wengine basi mambo yako yatanyoka kuliko wao.

kama niko sahihi kwa hayo niliyosema hapo juu nakushauri uanze kufanyia kazi yafuatayo
- amini kwamba baba yako anakupenda kwa vile ni mwanae na si kwa sababu wewe ni mtoto wa kiume
- mdhihirishie baba yako kwamba unawapenda nduguzo na utashirikiana nao siku zote. hii inaweza mfanya abadili
mawazo yake kuhusu mgawanyo wa mali zake
- tambua kwamba kusoma ni muhimu japokuwa sio uhakika wa mambo kukunyokea maishani. wapende nduguzo
bila kujali elimu yao.

hata hivyo nikupe pole kwa changamoto ulizopitia. nakuombea baraka na mola akuonyeshe pale ulipokosea ili uweze kupanyosha na pale ulipokosewa ili paweze rekebishwa.
 
Wala sikupi pole!! Hizo Mali si zako, ni za baba yako na Mkewe. Wewe umeshapewa urithi mkubwa Sana ambao ni Elimu. Tumia urithi huo kupata Mali zako wewe! Achana na Mali za baba, waswahili wanasema 'cha Mtu.......'.
 
Achana na mali za urithi, haziongezi kitu kwenye mafanikio ya mtu!!tafuta za kwako mwenyewe utazienjoy zaidi.
 
Back
Top Bottom