Naona kuna mtu hapa katumbukiza ‘coin’ za laki tatu kwenye kimashine cha mchina na kaliwa zote, haya ni matumizi sahihi ya ubongo?

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
5,267
2,000
Jamaa zangu wajeda ndio wahanga wakubwa wa hizi mashine za kitapeli.
Serikali iko kimya.
Pato la taifa karibu 5% linakwenda China kupitia haya madudu.
Haya madudu yanapuna sana. Kila kona yamewekwa
 

Kirokonya

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
1,713
2,000
Jamaa zangu wajeda ndio wahanga wakubwa wa hizi mashine za kitapeli.
Serikali iko kimya.
Pato la taifa karibu 5% linakwenda China kupitia haya madudu.
Haya madudu yanapuna sana. Kila kona yamewekwa
Mpaka vijijini Mkuu.

Kwangu binafsi, kucheza kamari ni upuuzi uliopitiliza.

Ni utaahira fulani.

Kamari hailipi mpaka mchezeshaji ashibe kwanza!

Jiulize, kuna mtu ashibaye hela?

Mnavurugwa kwa vijisenti mnavyokula ambavyo mnajichangia wenyewe huku mchezeshaji akiondoka na donge nono!

Amkeni.
 

Mirlz B Matthew

JF-Expert Member
Oct 10, 2011
2,034
2,000
Mitaan wanaliita Dubu au Bonanza utahira wakupeleka hela yangu kwenye hilo dude bado haujanipanda kichwani na hautonipanda kamwe...Bora ninywe 🍻 beer niifikirie dunia kwa mapana
 

jr.kiyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
678
1,000
Wamesahau tu kukuomba picha,huyo hapo....
africa_gambling_machines-1024x605.jpg
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,544
2,000
Kamari ina uraibu.

Kuna dada hua anakuja atapaki gari lake kisha atachill na hilo ishu hata masaa mawili.

Kisha kuna mjeshi hua akija anapiga stop woooote kucheza analicheza yeye tu akimaliza anaondoka zake.

Kuna jamaa young tu kupoteza 50K au 60K kwenye hiyo mashine kila baada ya siku mbili au nne ni kawaida. Na kila akiondoka anasema sichezi tena jana kaongea kiingereza 'I swear am not going to play this bonanza again'

Kuna mama ni muuza chakula kwenye toroli. Kila usiku lazima afike hapa na kuanza kulishughulikia hili dude, anasema hili ni bonanza lake la mwisho akiliwa huko koooote ndiyo anamalizia hapa.

Kuna couple hua mke anakuja hapa na mume anaenda bonanza la bondeni huko kila mmoja anaenda kulishughulikia hili ishu.

Katika kitu nimededuce ni kwamba watu wengi wanaocheza hili dude hua hawachezi ili wale ila wanaenjoy tu ile excitement ya kusubiria kuona kama wamepatia kitu ama la.

Eish nimemsahau na muha mmoja hua anakuja anaweka vyombo vyake chini anaingia arena.

Halafu guess what? Mimi ninayewapa hizo 200 hata sijui jinsi ya kulicheza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom