Naona bado kuna kuzungumkuti kikubwa sana kuhusu biashara yetu ya ndege na Shirika la ATCL

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,004
2,000
ATCL imeingia katika biashara ya anga kwa spidi kali sana na imenunua ndege za uhakika airbus na dreamliner tumeambiwa Boeing nyingine ipo njiani.

Nina wasiwasi mkubwa sana katika uendeshaji wake kama shirika hili litatengeneza faida na kutufanya tutembee kifua mbele. Biashara ya ndege sio lele mama, hata yale mashirika makubwa ya ndege kama vile Emirates, Qatar yanapata msaada toka Serikalini.

Je, Serikali ya Magufuli itaweza kuibebe ATCL? Kubebwa na Serikali sio mbaya kwa wakati mwingine lakini inabidi usimame mwenyewe.

Nimesoma habari hivi karibuni kuwa South African Airways travel agent hawataki kukatisha tiketi zao kwani muda wowote linaweza kuwa kwenye adminstration.

Mpaka sasa ATCL ina safari moja tuu ya masafa marefu. Mumbai mara 4 kwa wiki. Safari za Africa Kusini tumesitisha. Commercial hub - hii inatugharimu.

Ndege tulizo nazo tunazitumia zadi kwa masafa mafupi, DAR KJO, au DAR -MZA wakati ndege hizi zingepiga safari za masafa marefu ingekuwa vizuri. Rwanda air, Kenya airway, na Ethiopia airlines, hawatumii Air Bus au Boieng kwa safari fupi.

Inabidi tujizatiti zaidi katika safari za masafa marefu kabla ya ndege zetu hazijaanza kuchoka. Ndege aina ya embraer 190 zingetusaidia sana kwa safari za nchi jirani kama vile na za ndani

Hata nchi za Ulaya Safari za saa moja na nusu angani hawatumii haya ma air bus and Boeing 787-8
 
LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
3,532
2,000
kila mahali madeni na kulipa hawataki wataliuwa hilo shirika na ndege zitakufa mapema
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,890
2,000
Naona katika ununuzi wa hizo ndege kubwa Boeing na dreamliner JPM alikurupuka sana Bombadier bili za mwanzo zilikua zinatozha kwa safari za ndani kwa miaka 2 ya kwanza na kuzitumia maximally kwa safari za ndani.

Kama wenzetu Uganda wamefanya wana bobandier mbili lakini zinatumika kwelikweli kuenda Burundi Sudan mombasa Nairobi Kia na Dar wametumia mtaji mdogo kwa safari za nchi jilani. Kwetu tatizo ni kiki za kisiasa katika mambo muhimu
 
TO2004

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
508
250
Inawezakan hujafatilia vizuri mkuu ndege zetu zinaenda safari nyingi tu za nje,kuna safariri tatu kwa kwa wiki za kwenda zimbabwe & zambia.pia kuna safari za Rwanda na uganda kila wiki.Mwanzo huwa huwa ni mgumu ila hata hapa tulipofikia ni hatua nzuri sana
 
msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,635
2,000
tanzania kila mtu mjuaji.
ATCL imeingia katika biashara ya anga kwa spidi kali sana na imenunua ndege za uhakika airbus na dreamliner tumeambiwa Boeing nyingine ipo njiani. Nina wasiwasi mkubwa sana katika uendeshaji wake kama shirika hili litatengeneza faida na kutufanya tutembee kifua mbele. Biashara ya ndege sio lele mama, hata yale mashirika makubwa ya ndege kama vile Emirates, Qatar yanapata msaada toka serikalini.

Je serikali ya MAGUFULI itaweza kuibebe ATCL, Kubebwa na serikali sio mbaya kwa wakati mwingine lakini inabidi usimame mwenyewe. Nimesoma habari hivi karibuni kuwa South AFRICAN AIRWAYS travel agent hawataki kukatisha tiketi zao kwani muda wowote linaweza kuwa kwenye adminstration.

Mpaka sasa ATCL ina safari moja tuu ya masafa marefu. Mumbai mara 4 kwa wiki. Safari za Africa kusini tumesitisha. commercial hub - hii inatugharimu. Ndege tulizo nazo tunazitumia zadi kwa masafa mafupi, DAR KJO, au DAR -MZA wakati ndege hizi zingepiga safari za masafa marefu ingekuwa vizuri. Rwandair, Kenya airway, na Ethiopia airlines, hawatumii AIR BUS au Boieng kwa safari fupi. Inabidi tujizatiti zaidi katika safari za masafa marefu kabla ya ndege zetu hazijaanza kuchoka. Ndege aina ya embraer 190 zingetusaidia sana kwa safari za nchi jirani kama vile na za ndani
Hata nchi za Ulaya safari za saa moja na nusu angani hawatumii haya ma air bus and Boeing 787-8
 
viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,004
2,000
Inawezakan hujafatilia vizuri mkuu ndege zetu zinaenda safari nyingi tu za nje,kuna safariri tatu kwa kwa wiki za kwenda zimbabwe & zambia.pia kuna safari za Rwanda na uganda kila wiki.Mwanzo huwa huwa ni mgumu ila hata hapa tulipofikia ni hatua nzuri sana
Nadhani hujaelewa point.tatizo no kutumia ndege kunwa kwa safar za masaa mafupi.Kenya .Ethiopia n.a. Rwanda zndege zao zinazokujab Dar ni Bombadier na Embraer .Hawatumii Airbus wala Boeing kwa safari za masafa mafupi
 
Juma1967

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
16,820
2,000
ATCL imeingia katika biashara ya anga kwa spidi kali sana na imenunua ndege za uhakika airbus na dreamliner tumeambiwa Boeing nyingine ipo njiani.

Nina wasiwasi mkubwa sana katika uendeshaji wake kama shirika hili litatengeneza faida na kutufanya tutembee kifua mbele. Biashara ya ndege sio lele mama, hata yale mashirika makubwa ya ndege kama vile Emirates, Qatar yanapata msaada toka Serikalini.

Je, Serikali ya Magufuli itaweza kuibebe ATCL? Kubebwa na Serikali sio mbaya kwa wakati mwingine lakini inabidi usimame mwenyewe.

Nimesoma habari hivi karibuni kuwa South African Airways travel agent hawataki kukatisha tiketi zao kwani muda wowote linaweza kuwa kwenye adminstration.

Mpaka sasa ATCL ina safari moja tuu ya masafa marefu. Mumbai mara 4 kwa wiki. Safari za Africa Kusini tumesitisha. Commercial hub - hii inatugharimu.

Ndege tulizo nazo tunazitumia zadi kwa masafa mafupi, DAR KJO, au DAR -MZA wakati ndege hizi zingepiga safari za masafa marefu ingekuwa vizuri. Rwanda air, Kenya airway, na Ethiopia airlines, hawatumii Air Bus au Boieng kwa safari fupi.

Inabidi tujizatiti zaidi katika safari za masafa marefu kabla ya ndege zetu hazijaanza kuchoka. Ndege aina ya embraer 190 zingetusaidia sana kwa safari za nchi jirani kama vile na za ndani

Hata nchi za Ulaya Safari za saa moja na nusu angani hawatumii haya ma air bus and Boeing 787-8
Hujui lolote kuhusu biashara ya mashirika ya ndege. Kaa kimya.
**Kutumia ndege kubwa kwa route fupi wewe unaumia nini? Emirates (hanaga ndege ndogo anatumia hizo hizo kwenda destinations hata za dakika 45 kutoka Dubai-Doha (Qatar), Dubai-Manama (Bahrain)
 
Wewe ndio hujui lolote ,Emirates wanapata msaaada toka serikalini,Je Serikali ya Tanzania itaipa ATCl peas kujiendesha , Ethiopian airline wanatumia ndege ndogo kwa route za Dar,Rwandair wanatumia bombardier kuja Dar, KLM wanatumia Embraer 190 kuja London Hiyo in mifano michache tu
 
Unaongea nn wewe?
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,111
2,000
ATCL imeingia katika biashara ya anga kwa spidi kali sana na imenunua ndege za uhakika airbus na dreamliner tumeambiwa Boeing nyingine ipo njiani.

Nina wasiwasi mkubwa sana katika uendeshaji wake kama shirika hili litatengeneza faida na kutufanya tutembee kifua mbele. Biashara ya ndege sio lele mama, hata yale mashirika makubwa ya ndege kama vile Emirates, Qatar yanapata msaada toka Serikalini.

Je, Serikali ya Magufuli itaweza kuibebe ATCL? Kubebwa na Serikali sio mbaya kwa wakati mwingine lakini inabidi usimame mwenyewe.

Nimesoma habari hivi karibuni kuwa South African Airways travel agent hawataki kukatisha tiketi zao kwani muda wowote linaweza kuwa kwenye adminstration.

Mpaka sasa ATCL ina safari moja tuu ya masafa marefu. Mumbai mara 4 kwa wiki. Safari za Africa Kusini tumesitisha. Commercial hub - hii inatugharimu.

Ndege tulizo nazo tunazitumia zadi kwa masafa mafupi, DAR KJO, au DAR -MZA wakati ndege hizi zingepiga safari za masafa marefu ingekuwa vizuri. Rwanda air, Kenya airway, na Ethiopia airlines, hawatumii Air Bus au Boieng kwa safari fupi.

Inabidi tujizatiti zaidi katika safari za masafa marefu kabla ya ndege zetu hazijaanza kuchoka. Ndege aina ya embraer 190 zingetusaidia sana kwa safari za nchi jirani kama vile na za ndani

Hata nchi za Ulaya Safari za saa moja na nusu angani hawatumii haya ma air bus and Boeing 787-8
Wenzetu matimamu hutengeneza business plan kwanza. Si kazi ya kitoto. Inahitaji utalaamu na kuwa na options kadhaa.
Baadaye hufuata ununuzi wa ndege kulingana na business plan.
Sisi tunakwenda kinyume. Tumeanza kununua ndege kwanza! Kwenye ujenzi wa nyumba tumeanza na kupaua (ndege). Msingi (business plan) tutajenga baadaye.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,523
2,000
ATCL imeingia katika biashara ya anga kwa spidi kali sana na imenunua ndege za uhakika airbus na dreamliner tumeambiwa Boeing nyingine ipo njiani.

Nina wasiwasi mkubwa sana katika uendeshaji wake kama shirika hili litatengeneza faida na kutufanya tutembee kifua mbele. Biashara ya ndege sio lele mama, hata yale mashirika makubwa ya ndege kama vile Emirates, Qatar yanapata msaada toka Serikalini.

Je, Serikali ya Magufuli itaweza kuibebe ATCL? Kubebwa na Serikali sio mbaya kwa wakati mwingine lakini inabidi usimame mwenyewe.

Nimesoma habari hivi karibuni kuwa South African Airways travel agent hawataki kukatisha tiketi zao kwani muda wowote linaweza kuwa kwenye adminstration.

Mpaka sasa ATCL ina safari moja tuu ya masafa marefu. Mumbai mara 4 kwa wiki. Safari za Africa Kusini tumesitisha. Commercial hub - hii inatugharimu.

Ndege tulizo nazo tunazitumia zadi kwa masafa mafupi, DAR KJO, au DAR -MZA wakati ndege hizi zingepiga safari za masafa marefu ingekuwa vizuri. Rwanda air, Kenya airway, na Ethiopia airlines, hawatumii Air Bus au Boieng kwa safari fupi.

Inabidi tujizatiti zaidi katika safari za masafa marefu kabla ya ndege zetu hazijaanza kuchoka. Ndege aina ya embraer 190 zingetusaidia sana kwa safari za nchi jirani kama vile na za ndani

Hata nchi za Ulaya Safari za saa moja na nusu angani hawatumii haya ma air bus and Boeing 787-8
Ni ukwrli kuwa biashara ya usafirishaji kwa ndege ni ya ushindani mkubwa kama ilivyo biashara zote kubwa. Lakini...

Sababu zako/yako ulizo/yotoa ya mwendo wa saa moja au saa moja na nusu angani "hawatumii haya ma airbus na Boeing 787-8" ni batili.

Napenda ufahamu kwa ndege yoyote madafa ya saa moja ni marefu na si mafupi. Kinachotizamwa ni gharama na faida ya hiyo "route". Mahesabu yake yakijumuisha kila kiti au kila tani ya mzigo kwa hiyo safari inaingiza shillingi ngapi na inatumika shillingi ngapi. Mara nyingi kunatizamwa "break-even point" na hesabu zikionesha safari fulani kuivuka "break-even point" kwa asilimia kadhaa ni tosha kuwepo kifaida basi ndege hizo hufanyishwa safari hizo. Haijalishi masafa ya saa moja au masaa kumi.

Mfano, masafa ya saa moja "break-even point" ni 60% basi wakipanda abiria 70% una faida kwa safari hiyo. Halikadhalika masafa marefu zaidi ikiwa "break-even point" ni ndogo tuseme asilimia 35 lakini unabeba abiria asilimia 30 hapo una hasara kwenye hiyo safari.

Binafsi nasema, kikubwa kwenye hizi biashara ni "consistency" na kuwa na wafanyakazi wenye nidhamu ya hali ya juu katika matumizi na wizi. Bila hayo, hata ziwe safari zenye faida zitaishia kuwa ni hasara tu.

Mfano mzuri ni ndege kutakiwa kwenda kuchora nembo nje ya nchi kwa kutumia mamia ya mamilioni wakati kitu hicho kinawezekana kufanyika hapa hapa nchini kwa chini ya robo ya gharama za kuipeleka nje. Wale viongozi sifahamu bado wapo au walishatumbuliwa! Hayo ndiyo yanatuumiza Watanzania kuliko ushindani wa kibiashara, wizi mtupu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom