Nyamuleha jr
Senior Member
- Feb 20, 2013
- 185
- 65
Chasha wherever you are tafadhali naomba uje umsaidie kijana mwenzetu huku.
Mimi nahisi nitaandika hapa hadi vidole vitauma sidhani kama mdau atanielewa.
kijana mbona hata ujamaliza mwaka tokea umalize,,suala la ajira rasmi linahitaji uvumilivu,,na kusoma siyo kigezo cha wew kuchagua kazi wakati kazi unayoichagua wenzako wanalelea nayo familia,,kua na subira na uvumilifu,,na usichague kazi alimradi tu unajua unafanya kwa madhumuni gani,,Nimemaliza digri 2013 Baada ya kukaa dar mda mrefu kusaka ajira bila mafanikio nimeamua kurudi home, nimewakuta wale tulio soma nao lasaba wametoka kimaisha wamejenga, wanauhakika wa maisha tofauti na mimi ambaye sinahata ela ya vocha, nimekuta watu wamejiingiza sana kwenye biashara ndogo ndogo mbao, ufugaji wakuku, mwezi sasa umekatika watu wananishauri jiingize kwenye hizi biashara ndogo sasa naona noma kweli inshu ambazo ningefanya nikiwa la saba sasa nizifanye nikiwa nimemaliza chuo kikuu, kwanza nahisi nitawakatisha hawa madogo tamaa ya kusoma, nikama nilisha kuwa juu sasa nimerudishwa chini kwenye matope kabisa. Hapa naona bora niende mbali ambapo sijulikani nikafanye izo inshu, au nifanyaje?
mkuu, ushapata initial capital...?Naona hii post watu wameipenda kweli na ushauri wenu umenipeleka level nyingine, bora zaidi.
Nataka ni wambie hii ni day one yakuanza kutekeleza.:-
kwanzia nifike home nimekuwa mtu wa kujificha tu home nikitoka naenda town tu mara moja nachukuwa gazeti narudi home, ila bado kuna changamoto ya maneno hasa sisi tulio soma social sciences, utasikia sasa umesoma kozi gani hiyo, sosholoji, pltc science, ndiyo maana hupati ajira . Kuna wadau wameniambia fahari ndiyo baba waujinga watafute haohao walasaba ambao wamefanikiwa ukubali wawe walimu wako, nasema asante kwahilo., ngoja nianze kutafuta slide za enterprenueship nipate elimu zaidi.