Naona aibu jamani, nisaidieni

nyengo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
454
184
Tuna watoto wawili ktk famlia yetu, binti na wa mwisho ni mvulana. Mvulana ana mwaka mmoja na miezi sita. Sasa kinachonitia aibu ni kwamba huyu mtoto wa kiume tunapombadili nepi hua anashika nyeti zake na kuanza kucheka cheka kitu mbacho huwa naona aibu mbele ya mama mkwe ambae amekuja kututembela hivi karibuni.
Sijui ni kwa nini anafanya hiyvo na mnanis
hauri nifanyeje wanajamii
 
usijali hayo ni mambo ya kawaida kwa watoto unapombadilisha nepi huwa hewa inaingia hivyo hujisikia vizuri sana, muda mwingine uwe unamzoesha kukaa na chupi tu, unajua nepi huwa zinajoto sana? mimi mwenyewe nina mtoto nikimbadilisha huwa anafurahi sana, tena wakati mwingine anarusha na mikojo mara baada ya kumvua, hivyo jifunze kumuacha mtoto apate hewa mara kwa mara!
 
nyengo usione aibu! hiyo ni kawaida sana Mwanasaikolojia SIGMUND FREUD kaeleza mengi sana ebu ingia mtandaoni ( sigmund Freud psychosexual stages) utacheki ni hatua mojawapo tu ktk ukuaji, ya kwanza inaitwa ORAL stage yaani wewe mpatie mtoto chini ya mwaka 1 utakuta kila kitu akikishika anaweka MDOMONI ..........na kuna stage akifika kama wa kiume anamtamani mama yake mzazi na wa kike anamtamani babayake kimapenzi!
 
duuuu! hiyo kali nilikuwa sijui lol! kumbe watoto huwa wanatamani wazazi wao kimapenzi kaaaaaaaaaaaaaa! mpya hiyo..
 
Heeeeeh! Kwa kweli hiyo kali! Kumtamani mzazi kimapenziiiii??????!!!!! Mh, au unamaanisha ule upendo wa jinsia tofauti kwa watoto na wazazi, but sidhani ni wa kimepenzi jamani! Duuuh!
 
Kwani kuna ulazima wa kumbadili nepi mbele ya mama mkwe wako? acha kumbadili mtoto nepi mbele za watu, mengine acha nature ijishughulikie.
 
nyengo usione aibu! hiyo ni kawaida sana Mwanasaikolojia SIGMUND FREUD kaeleza mengi sana ebu ingia mtandaoni ( sigmund Freud psychosexual stages) utacheki ni hatua mojawapo tu ktk ukuaji, ya kwanza inaitwa ORAL stage yaani wewe mpatie mtoto chini ya mwaka 1 utakuta kila kitu akikishika anaweka MDOMONI ..........na kuna stage akifika kama wa kiume anamtamani mama yake mzazi na wa kike anamtamani babayake kimapenzi!

ASANTE NIMEISOMA NA NTAENDELA KUSOMA VIZURI.NASHUKURU KWA USHAURI WAKO qamunga goyyo
 
huyo kama mnalala naye chumba kimoja mhamisheni,angekua anaongea angewaumbua kwa sababu ile shughuli anashudia kweupe kama anatzama video.halafu niona unamikasa mingi?
 
NYENGO USIOGOPE NI JAMBO LA KAWAIDA, NI ISHARA YA KUFURAHIA KUPATA HEWA KWENYE MAENEO HAYO.
PIA FAHAMU MAMA MKWE ANAIJUA HIYO HALI ANAYOIONESHA HUYO MTOTO KSB NI MLEZI WA MUMEO...lol.

PIA NI KWELI KUWA MPENZI WA KWANZA WA MTOTO WA KIUME NI MAMA YAKE MZAZI AU YULE ANAYEMLEA/MLEZI.
NA UPANDE WA MTOTO WA KIKE MPENZI WAKE WA KWANZA NI BABA YAKE MZAZI/MLEZI NI KWA MUJIBU WA WANASAIKOLOJIA.
 
Inawezekana kuwa kuna kitu kinamwasha, usibweteke na wanaokuambia eti jogoo anawika.

Mie naona km sio hali ya kawaida jaribu kuwaona wataalam wamchukue vipimo sahihi.

huyu ni mtoto mdogo, hana sababu ya kumchezea mzee kila mara chukua hatua
 
Inawezekana unamuacha na mkojo kwa muda mrefu sana mpaka anaona tabu na pengine kuwashwa, so unapomvua anajisikia raha sana kama ametoka kifungoni. Jitahidi kumcheki mara kwa mara na kama amekojoa ili abadilishwe kwa wakati.

Halafu mwaka mmoja na miezi sita ni mkubwa anatakiwa aanze kuvalishwa vichupi, vikaptura au suruali nyepesi msimkabe kabe sana na manepi yanampa tabu tu.

Lingine kama walivyoshauri watu hapo juu mkiwa kwenye raha zenu hakikisheni hawaoni kwani watoto wa sasa wanapata akili mapema sana. Miaka miwili anaelewa kila kitu
 
Inawezekana kuwa kuna kitu kinamwasha, usibweteke na wanaokuambia eti jogoo anawika.

Mie naona km sio hali ya kawaida jaribu kuwaona wataalam wamchukue vipimo sahihi.

huyu ni mtoto mdogo, hana sababu ya kumchezea mzee kila mara chukua hatua

Na hii ina ukweli dada, ameshapata tohara?
 
Kwani kuna ulazima wa kumbadili nepi mbele ya mama mkwe wako? acha kumbadili mtoto nepi mbele za watu, mengine acha nature ijishughulikie.
Wakati nambadilisha nepi wakati mwingine mama mkwe yuko hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom