Naombeni ushauri

Nahic kule kuitwa itwa dia,honey,swit etc ndo kume ku inspire bro,hebu ipe kamati yako ya kichwa ifanye tathmn,hayo maneno cku hz ni ya kawaida sn unaweza ukaitwa na houz gel wako...
 
Mie kamwe skushauri, mpaka uziseme kwanza hizo sababu unazozificha. Halafu, mi naona huyu wa hapa umemtamani na huenda ulisa-do naye.
 
kuna baya lipo mbele ya TT kama ataamua kumuacha dada wa Mbeya na kujibanza kwa yule dar maana huyu wa dar yupo kimaslahi zaidi
 
Kuwa muwazizaidi ili tujue pa kuanzia
VInginevyo unamtamani huyo dada wa dar na unatafuta kujustfy


Heshima kwenu wana jamvi.

Nina mpenzi wangu ambaye kweli tuna pendana sana na kwa kweli ni msichana anayeniheshimu na kujiheshimu kuliko wasichana wote niliowajua, lakini kuna sababu ambazo kwa sasa sijaamua kuziweka wazi jamvini zinazopelekea nifikirie kuachana nae.

Lakini ukiachilia hizo sababu ambazo sijaona ni busara kuzimwaga jamvini ni kwamba tunafanya kazi mikoa tofauti, mimi niko dsm na yeye yupo mbeya, na wote tumemaliza chuo kikuu mzumbe, yeye mwaka jana, mimi mwaka juzi.

Sasa wakati nafikiria kuachana naye, huku dsm nako kuna msichana ambaye ni rafiki yangu wa kawaida tu, na ana mazoea nami hadi kufikia kuniita sweet, honey, love etc, ingawa ukweli ni kwamba hatuna uhusiano wowote na hata hivyo aliniambia ana mtu wake na anampenda sana, na mimi pia nilishamwambia kuwa nina mtu wangu, japo tuko mbali.

Sasa jana huyu msichana wa hapa dsm, kaniambia kwamba boyfriend yake sio mwaminifu, na kaamua kuachana nae japo anaumia coz anampenda sana so ameamua kunishirikisha ili nimshauri.

Kwa kweli wana jamvi nipo njia panda, kwa sababu na mimi nimejikuta natamani kum approach huyu dem aliyeachwa na jamaa yake kwa sababu dem wangu kwanza siko naye, so naweza kaa hata zaidi ya miezi miwili nikiwa naugulia hamu ya kufanya mapenzi, na hapa dsm niko more than lonely, nishaurini wakuu, nimtokee huyu dem aliyezinguliwa na mtu wake, then niachane na dem wangu wa kitambo as wanasema fimbo ya mbali haiuwi nyoka, niachane nae kwa style gani, coz naogopa kuumiza moyo wa mwenzangu, isitoshe she is so innocent and decent?

Wakatabahu.

Tt
 
na wasiwasi na wewe utakuwa unapenda wajane tu.yani unakimbilia wajane...labda ndo kipaji chako.mana unataka kumwacha mpenzi wa kwa ajili ya mang'aa flani.

daaaah, bro kweli nimeamini hata maneno ya watu yanaweza fanya umpende/usimpende mtu hata kama mara ya kwanza ilikuwa kinyume chake.

Yaan now kila ninapomuwaza huyu dem neno mjane linanijia kichwani.

Kwa kifupi umenifanya nianze kumwona hafai kwa kiwango kikubwa sana.
 
Tatizo lako hat kabla hujalileta humu inaonyesha tayari kichwani ulishaamua kupiga chini Mbeya ili u dominate Dar,,mbaya zaidi bila sababu za msingi!ulileta humu ili upate "simphathy"ya jamvi ku "legalize"hiyo "mission"achana na Dar maana huna sababu za msingi bana!hofu yangu ni kwamba hiyo weekness yako ya kukosa msimamo inaweza kuja kukutesa huko mbele,,jaribu kuidhibiti
 
We unafuata unapopendwa kweli au hiyo dick yako inavyojisikia, maana unasema hamu ya mapenzi, usipende kufuata tamaa ya mwili, utajuta bro, kama mmoja kati yenu, kazi yake inafaa kuhamia mkoa wa mwenzake, jitahidi mfanye hivyo, mapenzi ya kweli watu wanayalilia, we unatamani starehe ya nusu saa, ni vizuri mpenzi wako atambue tatizo la umbali linavyokukwaza ili mtafute suluhisho pamoja na kama itashindikana kila mmoja aridhie kama ni suala la kuachana, dah, haya mapenzi ya siku hizi kiboko, ni tamaa tu inayoyaongoza, tutakuja kweli thubutu kuwauliza binti zetu kama hao wanaotaka kuwaoa wanawapenda kwa dhati wakati hayo mapenzi ya dhati kwa wake zetu tulikuwa hatuna!, mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, tupunguzeni tabia mbaya jamani.
 
Nafurahi kuona kila kukicha JF michangi yenu ina msaada na hekima ndani yake kwani nimesoma mawazo ya wachangiaji mmoja mmoja hapa na nimeweza ona busara zenu hata kwenye maandishi,
mmemshauri vyema huyu kaka na ninaamin TT kama utafuata ushauri humu ndani usimuache dada wa mbeya kwani yatakuwa majuto maisha yako yote ...
jitahidi kutatua tatizo na siyo kulifunuka kwa sababu zisizo na msing,
je unadhani yeye huyo dada akiamua kutafuta mapungufu yako na kuyafanya yawe sababu ya kukuacha atashidwa?
i mean hata wewe yapo unayomkera ila anajua umuhimu wa kukuheshimu na kujiheshimu kwa kukurekebisha ili mtengeneze family bora..
be a REAL MEN make up your mind today achana na dada wa dar maana na wewe atakuwcha muda si mrefu,
huna lolote la kumuacha dda wa mbeya ni tamaa yako tu ,
jitahdid uishindde hiyo tamaa na utakuwa salama ...kumbuka ubora wa kitu hauuoni ukiwa nacho mpaka kitakapotoweka..

ushauri:fanyia kazi mawazo ya JF
 
Nawashukuruni saaaaana ndugu zangu wana j.f kwa jinsi ambavyo mmenishauri kwa hekima na busara kubwa sana, kwa kweli kwa mara ya kwanza wakati nawaandikia hii thread sikutarajia kama ningeweza shauriwa kwa busara kwa kiwango mlichofanya.

Na ni mawazo yenu haya yamefanya niongeze upendo mara dufu kwa mpenzi wangu aliyeko mbeya.

Nitaendelea kufanyia kazi na kama nilivyowaambia kuwa kuna ishu nyingine ambayo sikutaka kuiweka jukwaani kwa sasa, so nitaendelea kuitafutia ufumbuzi, then natumai baadae nitawafahamisha tena hapa jukwaani kwamba ni wapi nimefikia na uamuzi wa mwisho ni nini.

God bless you all.
 
Sasa sababu za kutaka kumwacha hutaki kusema halafu unataka sisi tukushauri nini? Hebu peleka utoto wako hukooooo...na inaonyesha huna akili so huyo binti hatokufaa unampotezea muda tu kwani anaakili na uelewa mkubwa kukushinda.
 
aisee hapo utavurunda na utamkumbua wa mbeya ukimwacha!Kama unakiri wa mkoani yuko vema,nakuapia utajuta kumuacha!kinachokusumbua ni upweke tu na wengi wanaishi katika hali hiyo,mbeya tu hapo?khaaa....me nshawahi kaa bukoba na galfriend (sasa mke) yuko songea,miaka 3 still tulivumiliana na tukaoana!huyo wa dar,kamalaya tu hako!hebu waza,ok ukiwa nae akahamishwa,utafanyaje?kweli tamaa mbaya.....hata hilo jina lako halikufai tena na ndio maana karibu watu wote waliokushauri humu sijui kama kuna mtu amekusifu kwa madudu unayotaka kuyafanya.....shinda majaribu,futa hayo mawazo mabaya
 
aisee hapo utavurunda na utamkumbua wa mbeya ukimwacha!Kama unakiri wa mkoani yuko vema,nakuapia utajuta kumuacha!kinachokusumbua ni upweke tu na wengi wanaishi katika hali hiyo,mbeya tu hapo?khaaa....me nshawahi kaa bukoba na galfriend (sasa mke) yuko songea,miaka 3 still tulivumiliana na tukaoana!huyo wa dar,kamalaya tu hako!hebu waza,ok ukiwa nae akahamishwa,utafanyaje?kweli tamaa mbaya.....hata hilo jina lako halikufai tena na ndio maana karibu watu wote waliokushauri humu sijui kama kuna mtu amekusifu kwa madudu unayotaka kuyafanya.....shinda majaribu,futa hayo mawazo mabaya

com dwn najua ameelewa maana kwa hasira hizo kuna baadhi ya watu wanatamani wamchape vibao humu lol ila najua he s is the real men atafanya maamuzi sahihi ...
 
Huna sababu ya msingi ya kumuacha mliependana siku nyingi. Usipende kuchukuwa walioachika na inawezekana huyo unayefikiria anamuacha mwenzake kwa kukosa uaminifu anaweza kuwa yeye ndio sio muaminifu. Chunga sana UKIMWI UPO UTAKUMALIZA. BORESHA UHUSIANO WAKO NA HUYO ALIYEKO MBALI NA MTAFUTE UWEZEKANO WA KUWA PAMOJA NA MKAMILISHE TARATIBU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom