Naombeni ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by cheusimangala, May 23, 2011.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Amani ya Mungu iwe juu yenu.

  kuna kitu kinaninyima raha kidogo nategemea mawazo yenu yatanifaa.

  Ni hivi,

  Mim ni member wa social club fulani,mkurugenzi wa hiyo club ndo alinishawishi nijiunge nao.Sikua namfahamu ila siku moja mahala fulani nilidodosha card yangu ya club niliyokua mwanachama zamani,ndo huyo baba akaiokota na kuanza kunambia kuwa yeye ni mkurugenzi wa club yenye activities kama za club ya card yangu hivyo akaniomba nijiunge na club yake sbb alijua kuwa club ye card yangu ilishafungwa.

  Kwa vile ni kweli club yangu ya zaman ilifungwa nikaona sio mbaya kutembelea hiyo club nione kama inanifaa,baada ya kuwatembelea mara mbili nikaridhika nao nikajiunga.

  Tatizo ni kwamba,mama mkurugenzi ananinyima amani,siku ya kwanza kabisa nilipofika yule mkurugenzi akaniintroduce kwa mke wake,na kumwambia mkewe kuwa mim ni mzoefu wa zile activities na kwamba nikikubali kujiunga nitaongeza nguvu,hasa ukizingatia my former club ilikua ina jina kubwa.

  Basi mim yule mama nikawa nampa heshima zake,ila tu nilivyojiunga akawa ananionesha chuki ambazo sielewi zinatokana na nini maana mumewe hajawahi kunitongoza na ninamuheshimu sana tu.

  Niko kwenye dilema sababu mama anaonekana hapendi uwepo wangu lkn mumewe/mkurugenzi ananipenda(kikawaida) sbb tokea nimejiunga kuna vitu nimewafundisha ambavyo walikua hawajui.

  Mkurugenzi wetu yuko serious sana na watu wengine lkn mim anapenda kuongea na mim,na kunipongeza kwa zawadi kila nikifanya vizuri,na kunisihi nisihame club.

  Sasa siku moja huyo mkurugenz aliniambia iwapo mtu yeyote ataniudhi nimweleze bila kuogopa,mkewe hakupendezewa na kauli hiyo,akamfokea mumewe eti asipendelee members sababu eti akiniambia vile napata kiburi na kwamba eti sihitaji kunyenyekewa kama nikitaka kutimua nitimue.Basi wao kwa wao wakazozana kidogo pale.

  Sasa mim nishagundua mama hapendi nikiongea na mumewe,lkn sijui nifanyaje maana yule mkurugenzi ni mchangamfu kwangu,siku nisipochangamka ananihoji sana,na pia najisikia vibaya kumjibu dry au mkato mkato mtu anayenichangamkia lkn kama mama yuko karibu natamani niwe bubu sbb jicho analokua analokua ananiangalia nalo lahitaji moyo wapendwa.

  Vile vile kuhama hii club kutaniathiri sana sababu baada ya club yangu ya zamani kufungwa imeniwia shida kupata club ya karibu yenye viwango,hii japo ni changa lkn ina viwango na ninaipenda tatizo ni huyo mama tu,maana kuna saa anaweza kuniangalia juu mpaka chini,chini mpaka juu kama macho yanaua huyu mama angeshaniondoa siku nyingi.

  Naombeni ushauri wa jinsi ya kuuteka moyo wa huyu mama maana sitaki kuhama hapa.
  Nifanyaje huyu mama atulie maana siku zote pamoja na kunionesha chuki sijaacha kumuheshimu wala kumuonesha dharau,huwa najifanyaga sielewi kuwa hanipendi.

  With Love:A S-rose:
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mama anawasiwasi na ukaribu wenu!
  Cha muhimu we mkwepe mumewe tu!
   
 3. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kwa hisia sana.

  Jaribu tu kuwa karibu na huyo mama kama itawezekana na uendelee kumuheshimu hivyo hivyo wala usiache

  Wanawake mna wivu nyie pole dada mpendwa
   
 4. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mh jamani club gani hizo ni hapa bongo au huko nje?
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  cheusi,kwa style hii mwana mke yeyote lazima angehisi
  ana karibia kuibiwa!
  either,...
  1.kua karibu sana na huyo mama,mfanye rafiki yako na mshirikishe mambo
  mengi sana ili awe huru na wewe kama mtoto/mdogo wake,..

  au
  2.ondoka kabisa,ili kutunza ndoa ya hao watu,hii ni option ya mwisho
  baada ya ya kwanza kushindikana!

  Please,usi mdokolee mwenzio mme wake!
  Kama umeolewa unaweza kumtambulisha mmeo kwa wote wawili
  huyo boss na mke wake (au hata mchumba kama unae ni vizuri pia)!!!
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kanitambulishe kwa huyo mama tatizo litaisha akijuwa una mtu,halafu mbona hunielezi haya mambo nyumbani ?
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mmmmmh
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ninachokiona hapa Cheusimangala huyu mama hajiamini kabisa anaona kama mzee wake anaweza akakutokea
  Pia labda huyu Mkurugenzi anatabia za kuwa ana totoz ambazo zinamfanya mkewe kukosa amani.
  na huo ukaribu pia upendo alionao kwako Mkurugenzi..kama ungekuwa uko commited na mtu ungeweza kumtambulisha Mkurugenzi na wife wake angalau ingeweza kumuondolea hofu huyo mamaa.
  Ila ndo matatizo ya kufanya kazi karibu na mme /mke hii ni kasheshe ..usicheke na mtu Gubu
  Ngoja niendelee kuwaza zaidi
   
 9. duda

  duda Senior Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  achana nae fuata kilichokupeleka.
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Cheusimangala najua kabisa na nakubaliana nawewe kua personally huna nia mbaya.

  Naomba uiangalie kwa upande wa huyo mama... kwa maelezo ulotoa hapo juu ningekua huyo mama amaini usiami naamini ningehisi kama wewe ila ninge ku tackle kwa njia tofauti sio obvious hivyo.. Unaweza ukaona sawa but it seems huyo baba kisha kupenda kimapenzi tokana na attention yoote anayo kupa na ile hali ya kusema hi is son in to you mpaka hata mbele ya mkewe anashindwa kujizuia. Huyo ni mke wake ilipaswa aoneshe heshima kua mkiwa wote watatu mko eneo moja awe considerate na feelings za mumewe....

  Cheusi mangala hebu angalia kwa umakini yafuatayo na wewe kama mwanamke mwenzangu jiweke nafasi kidogo ya huyo mkewe...


  • Yeye mwanaume ndo alikutafuta mkawasiliana mpaka mkakubaliana wewe uwe member - na kisha kukutambulisha kwa mkwewe; Ni common knowledge kua mumeo akikutambulisha msichana (tena nahisi wewe ni mrembo saana) - m/ke yeyote unakua makini na kuanza ku pick up signs...
  • Yeye huyo mama yupo toka mda hivyo ina maana anajua dedication ya mumewe iko vipi hapo club - huwezi jua; labda kuja kwa ndo kumemfanya kuongeza bidii zaidi....
  • Anakwambia mbele ya mkewe kua ukiwa na shida yoyote sema na atakusaidia.. mwanaume hata kama si mume ni boyfriend akisema hivyo kwa m/ke mwingine na hali wewe upo ni kwamba he is not considerate of her feelings... mimi mwenyewe siwezi penda.
  Ushauri wangu mimi ni kua hilo tatizo kulimaliza ni rahisi... mwambie huyo baba awe considerate to the wife na kwamba mkewe anaumia.. kueni more formal (mana sidhani kama huyo mama mjinga tu - labda kama katika hio club wewe ndo mdada pekee).. ukifanya hivyo na ukikwepa the husband eventually with time the wife will get to know you and understand.

  Wish you all the best.
   
 11. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  thanks,
  sasa nimkwempaje,mana nilishajaribu kufanya hivyo,kwa kumsalimia then huyo nawafuata wenzangu,lkn nikifanya hivyo ananihoji kama naumwa au kuna tatizo,ukisema no problem sir anasema nadanganya sbb anaona niko tofauti.
  Ningefurahi kusikia ww ungemkwepa vipi ndo mana nikaja kwenu baada ya kujaribu bado naona nashindwa.
   
 12. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  asante sana umegusa point muhimu,umeongea kama mwanamke,umeongea yenye busara.
  kweli hata mim angekua ni mume wangu nisingefurahi
  mm ni mtu mzima naelewa dalili za mwanaume anayenipenda kimapenzi,lkn huyu ananijali sbb anaona umuhimu wangu kwa club yake,chukulia mfano ni club ya mpira si lazima coach atapendelea wale wachezaji anaoona wananyanyua timu.
  Huyo kunambia mbele ya mkewe kuwa mtu akiniudhi nimweleze sioni kama ni tatizo sbb pia alinambia kama yeye hayupo kama kuna jambo nisisite kumshirikisha mkewe.
  Hata mim siku moja nilipanga nimweleze kuwa naona mkewe hafurahii huu ukaribu lkn nikashindwa sbb namuheshimu sana na kama nilivyosema hajanitongoza.
  Kuhusu kama ana tabia ya kutongoza tongoza sijui na wala siwezi kumtetea lkn mm hajanitongoza na wapo wadada wenzangu lkn sijahisi kama anawatongoza sbb yuko serious sana.
  mim sina urembo wowote kama unavyofikiri kua ndo sbb ya huyo baba kupagawa,kinachomvutia kwangu ni uzoefu na mambo ninayocontribute kwa club yake.
  Tena mm naona anampenda sana mkewe sema ndo hivyo tena naona haelewi.
   
 13. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  ini SOCIAL CLUB,sio club za madisco au pombe,activities tunafanya hata mchungaji au sheikh anaweza kufanya,mradi awe anapenda ,awe na uwezo na vigezo.
   
 14. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nilikueleza dear sema siku ile nadhani pombe ilikuzidi kidogo ndo mana hukumbuki.
   
 15. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hiyo roho isije ikaniingia hata siku moja kwa jina la Yesu,
  Sitakaa nifanye hivyo,sio kwa huyo tu hata kwa wengine.
   
 16. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
   
 17. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wewe cheusi ushapoteza maono ya mume wa mtu embu feki mpaka akose raha kama huna mood na huyu mume uone kama mwanaume ataendelea kujifanya ana care your movement au tamaa mbaya tu!
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Basi kazi unayo dear... All the best katika kufika solution..
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  sorry,
  pale kwenye neno NISINGEFURA nilikosea,nilitaka kusema hata ingekua mie NISINGEFURAHI nikasahau HI.
   
 20. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,978
  Likes Received: 6,621
  Trophy Points: 280
  unaonekana mzuri sana kuzidi huyo mama.halafu mbona una mazoea sana na mme wa mtu kwa kivuri cha ukurugenzi?inaonekana ulivyokuja ndo akaanza kutoa zawadi.kwanini unategeka sana na hii mitego yetu?je wewe unafurahia unavyopendelewa bila sababu?huyo mama kastuka.baada ya hapo mtaanza kupelekana lunch.acha kumzoea mumewe.kama unaona jicho lake linakupa tabu muulize akiwa na mmewe kulikono?lakini cha msingi deal na kilichokupeleka tu hayo mambo mengine ya kawaida.kama una faida nao endelea.tumikia kafiri...
   
Loading...