Naombeni ushauri wenu

Naombeni ushauri wenu

Mijanaume mingine sijui ipoje.ss ww ulivyomzalisha mwenzio alafu nani aje kumuoa?muoe huyo aliekuzalia.huyo unaemuona bora alipata mtu ndo akakuona hufai ndo maana akakwambia msitishe uhusiano.
 
MWENYEZI MUNGU atakuchukia.
mtoto wako atakuchukia.
mama atakuchukia.
ulimwengu utakuchukia.
Ungekuwa mwanangu au mdogo wangu ningekujibu kwa ngumi afu nikakuuliza unajisikiaje then nkakwambia hayo ni maumivu madogo sana kwa moyo wa mama mtoto....
 
Kweli weh! Kilaza sifa moja yamwanaume nikuwa namaamuz acha upuuz bana embu onesha ukidume wako.
 
Huyo dem alipata kibuz kingine akakutema bila sababu ya msingi kirahisirahis 2 we unadhan huyo ana mapenz ya kweli kwako? Imagne baba yako angemuacha maza ako na kuoa mke mwingne,me najua uchungu wa kutelekezwa na mshua.me mwanamke ntakayezaa naye ndo ntayeish naye hata akiwa hous girl
 
hii story itanoga zaidi ukimuacha huyo mwenye mtoto..huyo unayemrudia atakuacha tena,
 
Hivi wewe ni mwanaume gani usiye kuwa na msimamo? Huyo demu wako wakwanza naona alikuwa anatingisha kiberiti alijua hutopenda tena, sasa kaona umependa na mmepata mtoto anajidai kuomba msamaha, mbona msamaha wako wewe yeye hakuusikiliza? Achana naye kaa na huyo demu wako mpya mlee mtoto wenu, huwezijua Mungu anakuepushia nini kwa huyo dada.
 
Huyo mwanamke wa kwanza kama alikupenda kwa dhati mbona alikuacha kwa hatua kubwa mliokuwa mmefikia? Au kuna tatizo lilo kwako ulitenda ndiyo akakutema au yeye alimpata mtu akakutoka ghafla akakuta ni maji marefu kwa hiyo akarudi. Kweli ndoa zenu hizi siku hizi mna kazi kubwa sana. Ningekuwa wewe ningeoa mwenye mtoto.

Fundisho, unapoachana na mpenzi au mchumba wako kama unampenda, usikurupuke, tulia kwanza tafakari maana unaweza angukia hata kwa kima ili mradi unapooza stress. Pia ni kwa nini within two month unakutana na mwanamke mantembea kavukavu? Hata incubation period ya VVU hukusubiri au mpenzi wako wa zamani alirudi baada ya muda gani? All in all ni matokeo ya kutojipa nafasi ya kutafakari pale mahusiano yanapokorofisha. Pole zako, umelikoroga na uamuzi uko kwako na si JF maana hapa tunakupa kila aina ya ushauri, pengine tunakuchanganya zaidi.
 
Nilikuwa na mchumba wangu wa siku nyingi,tukajuana tabia,tukaridhiana akanitambulisha kwao nikamtambulisha kwetu wazazi wetu waliridhia na kutuombea mema ili tujipange tuje tufunge ndoa. baadae tukaja kupishana na huyu mchumba wangu akanitamkia kuwa niwe huru nimtafute tu msichana mwingine.wazazi wake wakadokezwa taflani ya mahusiano yetu wakamkalisha chini na kumwomba afikirie kabla ya kuchukua maamuzi.akasema nabaki na msimamo wangu. baada ya miezi kama miwili nikampata dada mmoja nikaingia nae kweny mahusiano na bahati nzuri hyu msichana akapata ujauzito bila ya kufunga ndoa.baadae yule msichana wa kwanza akaja kuniomba msamaha na ndugu zake wakanisihi sana kuwa tusiachane.kwa kweli nipata wakati mgumu sana kimawazo na ukweli msichana anabusara, hekima,mpole,na mwaminifu sana lakini nikasema itakuwaje na huyu msichana mwenye mimba?kabla sijafanya maamuzi nikawashirikisha wazazi wang ili wanipe ushauri.wazazi wakaniuliza mm mwenyewe nimemwona yupi ni bora zaidi ya hawa wawili? nikawajibu ni huyu wa kwanza hata kama tulipishana.nikapata wakati mgumu sana kumweleza dada mwenye ujauzito ambae baadae akajakujifungua mtoto wa kike. ili nimweke wazi msimamo wangu. ingawa nilijua nimemkosea sana.kama binadamu nilikiri makosa yangu kwake.nilipomweleza kwa mara ya kwanza akakataa akasema hataki kusikia hilo.kwa kweli iliniuma sana roho ya huruma ilinijia hasa baada ya kujua yeye hana makosa ingawa anamapungufu yake ingawa si sawa na ya yule wa kwanza ingawa wote wana mapungufu yao ya kibinadamu.lakini ndugu zangu ukweli toka nafsini mwangu nahitaji na nampenda zaidi na nataka kumwoa mwanamke yule wa kwanza kwani nilikaa nae nikamweleza kila kitu kilichotokea akasema yaliyopita si ndwele tugange yajao.kwa kuwa huyu mwenye mtoto alikuwa yupo nyumbani ili kuangalia ustawi wa mtoto sasa nataka nimrudishe kwao ili nitimize ndoto zangu za kuwa na mke wa nafsi yangu.mwanamke mwenye mtoto hataki kurudi nyumbani.nifanyeje? naombeni mawzo yenu yenye hekima ili amani ipatikane kwake na kwangu pia. WA SALAAM NDUGU ZANGU.
email_open_log_pic.php

Uliyempa mtoto kwani hana ndoto zake alizotaka zitimie?

Endapo imani yako inakuruhusu oa wote

Ndoa ni kuvumiliana katika shida na kharaha basi uliyempa mimba (umpokee awe wako) wewe ungezaliwa nje ya ndoa ungekuwa wapi kwa muda huuu?
 
Ukisikia kulikoroga ndo huku
uko tayari kumtesa mwanao sababu ya 'kumuabudu' huyo mwanamke

kwa akili yake anaamini huyo wa kwanza ni malaika sasa kwamba amejirekebisha.kafanya umalaya wake huko kaona wewe umeseto ameona wivu amerudi na coz anajua jamaa ni zezeta lake atamkubalia tu.mwanamke akishajua huwezi ishi bila yeye atakusumbua sana ktk maisha yenu.akili kumkichwa
 
We jamaa nimekudharau sana stupid.we kwa akili zako unaona huyo mtoto hana thaman sababu ya pumbuja looh.kweli kunawanaume vimeo.sh...e...n...z..i kabisa.
 
Huyo wa kwanza hakupendi
Buzi lake limekata kamba huko alikokuwa.

Mabushoke wengi siku hizi, woman of my life my f**t
 
ukisikia utu uzima jaa ndo hii man....kwa kawaida kama mwanamke alikuacha mara ya kwanza,ukimrudia atakuacha tena joh....
nasema tu kama angalizo:banghead:🙁:banghead:😎😉
 
Unajua ndoa ni mkataba wa maisha yako yote so inakupasa uwe mwangalifu unapotaka kuingia kwenye mkataba huu. Usioe kwa kumhurumia mtu, usioe kisa muda umepita sana na sasa una pressure ya time. Sasa ni vema kuoa unaempenda rafiki lkn kwanini ulikua na haraka hivyo ya kuanzisha mahusiano mapya na mpaka yakakukuta yote haya.

Kumbuka unapozaa kabla ya ndoa kuna challenge nyingi hizo huwezi kuzikwepa utakapoingia kwenye ndoa. Mimi naona muache dada wa watu aende kwa amani kuzaa kabla ya ndoa si tatizo Mungu atampa wa kwake atakaempenda kwa dhati. Oa unaempenda na itakusaidia utaishi na huyo umpendae kwa amani pasipo kumlaumu. Unajua kuna ndoa zingine mtu anasema nilikuoa sababu tu ya huyu mtoto kama si huyu mtoto nisingekuoa pengine mdada anaweza asiwe hata na kasoro nyingi lkn kwa vile hukumpenda utaona kila kosa na kujuta maisha yako yote ie unaishi ktk denial.
Remember marriage is a life time commitment do not mess-up
 
Aghrrrr!
Mungu tusaidie, Ulikuwa unawaza nini wakati unaingia ktk mahusiano mapya,ilikuwa stress ama? Huyo mdada mwenye mtoto nampa pole sana kwan hata ukifunga nae ndoa itakuwa kama funika kombe mwanaharam apite make kwa maelezo yako inaonesha kama humpendi,kila mtu anamapungufu yake hamna aliyekamilika kama umeweza kuwa nae hadi mkampata mtoto kwann unashidwa kuendelea nae, ok lbd sbb ni yule wa kwanza.
Kwann unashidwa kuwa na msimamo wa kusimamia maamuzi yako,je umejiuliza kwa nini huyo dada aliamua kusitisha mahusiano yenu?
Na kimemsibu nn mpaka anaamua kukurudia wakati kipindi anasitisha mahusiano yenu aliulizwa/aliambiwa afikirie maamuzi yake nae akasema ndo keshaamua!
 
Mmmh aise ndo mana nachukia wanaume saa zingine....
 
Back
Top Bottom