Naombeni ushauri wenu

dimple

Senior Member
Dec 6, 2016
100
126
Mimi naishi Dar najihusisha na kilimo na ufugaji

Tuna shamba letu kubwa tu Bagamoyo Fukayose lipo ekari 37
Kuna kipindi tuliweka wafanyakazi tukawa tunalilimia mahindi ila kutokana na changamoto za mvua hailifanya vizuri.

Tukashauriana na mr kujenga banda kubwa la kufugia na nyumba ya vyumba viwili na tukazungushia senyenge kama ekari mbili tukaingiza kuku wa chotara 180 wakubwa miez 5 niliwanzia kuwafugia nyumban ila banda likawa dogo ikabidi ndo tuwahamishie shamba kwanza tukasema tuanzie hapo kwa shamba basi Mr alimuweka ndugu yake akawa anaishi hapo anamlipa mshahara tukalima na nanasi ekari 5.

Kuku wale wakaanza kutaga kidogo kidogo ila huyo msimamizi akaanza kuzingua mnooo ktk kipindi chote hicho mr hakuwahi kula hata sh 100 ila kuku wakaendelea kujilisha kupitia mayai kama unavyojua mayai yakawa yanapungua kadri siku zinavozidi kwenda kijana akaanza kuuza kuku mara anasema wamegongwa na nyoka uongo mwingi tu Tukakubaliana na Mr tuwauze kuku walio baki na mradi wa shamba upande wa kuku ukaishia hapo hadi tunauza hao kuku mr hajawai kula hata cent moja watu wanavyofata mayai anakwambia nimenunua chakula cha kuku.

Mimi nikaanza fuga kuku wa mayai nyumbani na mradi unaenda vyema sasa Mr anataka tuupanue huu mradi hadi shamba sabab una hela mimi nina mgomea sabab ku control mayai ukiwa mbali ni shida tutaingia ktk hasara tena na yeye kakubaliana na hili sasa hivi anataka kufuga tena kuloiler kwa nyama yaani miez 3/4 anawatoa kuwauza anasema usimamiz wa kuku wa nyama ni rahisi hata ukiwa mbali sabab kuku akifa ni rahis kumwambia msimamiz akuonyeshe mzoga wake kinachomuuma Mr ni ametumia pesa nyingi kujenga mabanda na kibanda cha msimamizi na wafanyakaz halafu pakae tu hapamuingizii pesa nimekuja kwenu je nimpe go ahead aendelee au nimkatalie sabab Mr hua anafataga ushaur wangu sana je mnaofugia mbali mna control aje mifugo yenu?

Ni sehem ambayo huwez kwenda kila siku na Mr ni muajiliwa hua weekend tu ndo anaweza kwenda.Msimamiz anaweza badirisha
 
Hakika inawezekana ila muhim kutafuta mtu mwaminifu, ukimpata na ukawa unamsimamia vizuri ni rahisi kucontrol hata ukiwa mbali, mradi ukiwa unaanza hakikisha kuna kitabu cha kutunza records, awe na smartphone kwaajili ya kua unafatilia number ya kuku na maendeleo yake kwa video.

Na mwisho nashauri ajil mtu mwenye taaluma ya mifugo ili kuokoa gharama za kuita madaktar panapotokea uhitaji huo na pia itasaidia kua na usimamizi wa uhakika.

Nimesoma mifugo, ndio nimehitimu mwaka huu diploma, unaweza nipatia nafasi tukaanza pamoja kwa uaminifu
Ahsante!

Namba yangu, 0627544910
 
Mimi naishi Dar najihusisha na kilimo na ufugaji

Tuna shamba letu kubwa tu Bagamoyo Fukayose lipo ekari 37
Kuna kipindi tuliweka wafanyakazi tukawa tunalilimia mahindi ila kutokana na changamoto za mvua hailifanya vizuri.

Tukashauriana na mr kujenga banda kubwa la kufugia na nyumba ya vyumba viwili na tukazungushia senyenge kama ekari mbili tukaingiza kuku wa chotara 180 wakubwa miez 5 niliwanzia kuwafugia nyumban ila banda likawa dogo ikabidi ndo tuwahamishie shamba kwanza tukasema tuanzie hapo kwa shamba basi Mr alimuweka ndugu yake akawa anaishi hapo anamlipa mshahara tukalima na nanasi ekari 5.

Kuku wale wakaanza kutaga kidogo kidogo ila huyo msimamizi akaanza kuzingua mnooo ktk kipindi chote hicho mr hakuwahi kula hata sh 100 ila kuku wakaendelea kujilisha kupitia mayai kama unavyojua mayai yakawa yanapungua kadri siku zinavozidi kwenda kijana akaanza kuuza kuku mara anasema wamegongwa na nyoka uongo mwingi tu Tukakubaliana na Mr tuwauze kuku walio baki na mradi wa shamba upande wa kuku ukaishia hapo hadi tunauza hao kuku mr hajawai kula hata cent moja watu wanavyofata mayai anakwambia nimenunua chakula cha kuku.

Mimi nikaanza fuga kuku wa mayai nyumbani na mradi unaenda vyema sasa Mr anataka tuupanue huu mradi hadi shamba sabab una hela mimi nina mgomea sabab ku control mayai ukiwa mbali ni shida tutaingia ktk hasara tena na yeye kakubaliana na hili sasa hivi anataka kufuga tena kuloiler kwa nyama yaani miez 3/4 anawatoa kuwauza anasema usimamiz wa kuku wa nyama ni rahisi hata ukiwa mbali sabab kuku akifa ni rahis kumwambia msimamiz akuonyeshe mzoga wake kinachomuuma Mr ni ametumia pesa nyingi kujenga mabanda na kibanda cha msimamizi na wafanyakaz halafu pakae tu hapamuingizii pesa nimekuja kwenu je nimpe go ahead aendelee au nimkatalie sabab Mr hua anafataga ushaur wangu sana je mnaofugia mbali mna control aje mifugo yenu?

Ni sehem ambayo huwez kwenda kila siku na Mr ni muajiliwa hua weekend tu ndo anaweza kwenda.Msimamiz anaweza badirisha
Pole sana mkuu. Hongera kwa uthubutu na uvumilivu . Ukweli ni kwamba Mradi/biashara ni kama mtoto, huwezi kuzaa kichanga siku ya kwanza tu umpe mtu akulelee lazima mwanzo upambane nae mwenyewe mpaka atakapofikia hatua flan ndo unaweza kumuachia dada wa kazi na kwa muda flani lakini bado sehem ya uangalizi wako wa karibu unahitajika mpaka atakapoweza kujisimamia. Hakuna mradi ulokuwa kwa maelekezo tu pasi na usimamizi wa karibu toka kwa wahusika.

1:Mwambie Mr atatumia gharama kubwa mno kupata matokeo madogo. Namaanisha hata akipata mtu mwaminifu bado kutokuwepo kwake sehem ya tukio kutamfanya aingie gharama kubwa mno ambazo angeweza kuziepuka kama angekuwepo.

2: Huo mradi wewe ndo ulitakiwa uusimamie coz we ndo ushakuwa na experience kubwa na ufugaji ko una version na mradi kuliko jamaa ambae version yake ni kupata pesa tu.

3: Hakuna kazi ngum kama human resource management. Ku manage watu ni kazi mno kwa7bu everyone has his own interests ko kipindi we unawaza kuulea mradi ili ukue ulete matunda mnufaike wote wenzako wanawaza kuwa na mradi kama wako kwa kupitia mradi wako. So unahitaji usimamizi makini na lazima itaonekana unambana ili mambo yaende.
 
Utafanya yoooote lakini nakupa moja tu ukitaka kufanya mradi wa maana na serious usiweke ndugu narudia usiweke ndugu hayo wanayaweza wahindi na races nyingine lakini sijui mtoto wa mjomba hana kazi nimuweke dukani,sijui meneja guest utafurahi
 
Back
Top Bottom