Naombeni ushauri wenu katika hili jambo la kazini wanaJF

Naombeni ushauri wenu katika hili jambo la kazini wanaJF

Sarayevo

Senior Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
117
Reaction score
42
Natumai mumeshinda salama ndugu zangu, kama kichwa cha habari kinaposema naomba ushauri kwenye hili jambo:

Baada ya kuajiriwa kwa muda mrefu niliona nitafute njia ya kujiajiri basi nikapanga mwisho wa 2019 nitaacha kazi lakini mfanyakazi mwenzangu akaniambia nisaini tu mkataba alafu baadae nitafanya maarifa nivunje huo mkataba kitu ambacho nilifanya na mpaka sasa hivi napoandika nilishakamilisha utaratibu wa kuacha kazi mwisho wa mwezi Jumamosi.

Lakini sasa kulikuwa na mabadiliko kwenye uongozi wakaleta kiongozi mpya na mimi ndio niliempokea lakini sasa jamaa kanibadilikia na kuwa adui kabisa hata nimsalimie wakati mwingine anaona tabu kuitikia kuna siku alifika asubuhi bila kujua kwamba mimi nilifika mapema na kuingia kwenye kazi aliponiona ofisini akataka kuanza ugomvi mimi nikamwambia mimi nipo kwenye kazi yangu ndio nimetokea kuja hapa ofisini.

Sasa ndugu zangu huyo jamaa nimwambie waziwazi liwe naliwe au ninyamaze mpaka hiyo Jumamosi ili nimuone atafanya nini?

Karibuni sana kwa ushauri wenu.
 
Fanya kuachana naye songa mbele boss hamna haja ya kukwazana baina yenu. Tafuta furaha kwenye maisha mambo mengine achana nayo yapite tu
 
Kama uko kwenye process za kuacha kazi na kujiajiri ushauri wa nini tena hapo mkuu
 
Kama uko kwenye process za kuhama ushauri wa nini tena hapo mkuu
Yani hizi week kama tatu hivi ninafanya kazi kwa wakati mgumu sana na huyo jama wakati anajua mimi naondoka lkn lazima anajenga bifu.
 
Hebu kumbuka vizuri ktk pitapita zako hujawahi kula demu wa jamaa kweli maana sio bure
 
Duh!! Haya maisha ni fumbo kubwa Sana, unatamani kuajiriwa aliyeajiriwa nae anatamani kuacha kazi, unatamani kuolewa aliyeolewa nae anatamani angeachika, unalilia afya mwenye afya njema anakunywa sumu!!

Mkuu Mimi ni graduate nipo mtaani maisha kwangu ni magumu, naomba unielekeze hiyo ofisi nami nipeleke maombi yangu kama nipo qualified lakini!!!

Nitakushukru sana mkuu wangu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom