Naombeni ushauri wadau, hili ni tatizo gani?

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
762
Reaction score
627
Yaani kifua kinaniuma, kilianza kama miti miwili inanichoma kwa muda fulani halafu inaacha!

Hospitali wamekuwa wakidai nipige x-ray za kifua nazo zinaonyesha hakuna tatizo!

😥😥😥
 
Pole sana, waambie wakupime vipimo zaidi maana kama unaumwa halafu wanakwambia hakuna tatizo kwa hiyo unachoumia sio tatizo?
 
Pima vipimo vingi zaidi. Kama ugonjwa utakuwa bado hauonekani basi tafuta sehemu yoyote ya maombi(ya kikristo) Watasaidia ku solve hilo tatizo chap.
 
Je, ukivuta pumzi unahisi vipi mkuu?, je kuna dalili yoyote unahisi kama ya makohozi au kukwaruza kama kitu kinabana?, je unaumia? Inaumaje ukivuta hiyo pumzi kwa muda mrefu na kuibana?

Huwa unatumia sigara, shisha au bangi?, au huwa upo karibu na moshi hususa wa viwandani?

Au huwa upo karibu na shuhuli za upigaji rangi?, au randa za mbao na wapiga msasa fanicha?.

Basi tueleze kwa kifupi na shughuli yako mkuu, kila tatizo lina historia kulingana na mfumo wa kimaisha.

NB: Mimi sio daktari au mtaalamu wa tiba hapa nimewaza tu kama raia. Wataalamu watasaidia ukifanikisha kujibu hayo maswali sababu utakuwa umetoa mwanga zaidi.

Pole sana ndugu.
 
Asante kwanza kuonyesha kujali! Kuhusu mambo uliyouliza, mimi sivuti sigara wala bangi! Nakumbuka kabla ya yote niliteleza ile kawaida Ila sikuanguka chini nilishika mti! Baadaye nikawa na michomo michomo upande wa tumbo hadi kwenye moyo! Nilipoenda hospital wakanipiga x ray ya kifua na ultrasound ya tumbo!Kila kitu kilikuwa normal!Maumivu yakahamia kifuani nikadhani labda ni magodoro ninayotumia, nikaagiza Tanfom mbili za 5 kwa 6, ndizo ninazolalia lakini wapi! Maumivu kama kawa!
 
Asante kwanza kuonyesha kujali!Kuhusu mambo uliyouliza,mimi sivuti sigara wala bangi!Nakumbuka kabla ya yote niliteleza ile kawaida Ila sikuanguka chini nilishika mti!Baadaye nikawa na michomo michomo upande wa tumbo hadi kwenye moyo!Nilipoenda hospital wakanipiga x ray ya kifua na ultrasound ya tumbo!Kila kitu kilikuwa normal!Maumivu yakahamia kifuani nikadhani labda ni magodoro ninayotumia,nikaagiza Tanfom mbili za 5 kwa 6,ndizo ninazolalia lakini wapi!Maumivu kama kawa!
Pole sana Itakuwa mshtuko pata Mucolin
 
Nenda kàpige xray na ct scan hospital za kueleweka na wenye utaalam wa kuangalia x ray sawa sawa. Ni wazi tatizo lipo ilà watu wanazidiana utaalamu hasa kwenye xray
 
Samahani ninaomba ufafanuzi kidogo kama hutojali!
Kuna mtu walimnyonga wakajua kafa wakamtupia mtaroni kumbe alizimia wasamalia wakampeleka hospital amepona kabisa ila ule mshtuko wa mifupa ya koo anasikiaga maumivu ila akipima hana kitu huu mwaka wa 8 amebaki anakunywa dawa za kutuliza maumivu tu.

So kulingana na ulivoeleza navohisi Itakuwa wa kumeza dawa za kupunguza maumivu.
 
Je, ukivuta pumzi unahisi vipi mkuu?, je kuna dalili yoyote unahisi kama ya makohozi au kukwaruza kama kitu kinabana?, je unaumia? Inaumaje ukivuta hiyo pumzi kwa muda mrefu na kuibana?

Huwa unatumia sigara, shisha au bangi?, au huwa upo karibu na moshi hususa wa viwandani?

Au huwa upo karibu na shuhuli za upigaji rangi?, au randa za mbao na wapiga msasa fanicha?.

Basi tueleze kwa kifupi na shughuli yako mkuu, kila tatizo lina historia kulingana na mfumo wa kimaisha.

NB: Mimi sio daktari au mtaalamu wa tiba hapa nimewaza tu kama raia. Wataalamu watasaidia ukifanikisha kujibu hayo maswali sababu utakuwa umetoa mwanga zaidi.

Pole sana ndugu.
Ahsante kwa maswali yako ingawa sio mtaalamu. Yameibua kitu ambacho hakikuelezwa mwanzo, ila kinaweza kusaidia. Alipata ajali, aliteleza.
 
Yaani kifua kinaniuma ,kilianza kama miti miwili inanichoma kwa muda fulani halafu inaacha!

Hospital wamekuwa wakidai nipige x-ray za kifua nazo zinaonyesha hakuna tatizo!

😥😥😥
CT scan utaonyesha hembu cheki maana lazima ukipoanguka kuna damage ilitokea ndani kwa ndani japo hukuona impact kwa nje, damu itakua ilivia ndani
 
Yaani kifua kinaniuma ,kilianza kama miti miwili inanichoma kwa muda fulani halafu inaacha!

Hospital wamekuwa wakidai nipige x-ray za kifua nazo zinaonyesha hakuna tatizo!

😥😥😥
Vipimo vya ECG umefanya!?
 
Asante kwanza kuonyesha kujali!Kuhusu mambo uliyouliza,mimi sivuti sigara wala bangi!Nakumbuka kabla ya yote niliteleza ile kawaida Ila sikuanguka chini nilishika mti!Baadaye nikawa na michomo michomo upande wa tumbo hadi kwenye moyo!Nilipoenda hospital wakanipiga x ray ya kifua na ultrasound ya tumbo!Kila kitu kilikuwa normal!Maumivu yakahamia kifuani nikadhani labda ni magodoro ninayotumia,nikaagiza Tanfom mbili za 5 kwa 6,ndizo ninazolalia lakini wapi!Maumivu kama kawa!

Pole sana,
Kuna uwezekano, wakati unajiokoa usianguke kwa uzito wako na nguvu ya mwendo, uliumiza kiungo/joint kati ya kifupa cha katikati ya kufua na mbavu.

Kuna maswali ya nini ufanye na kutoa majibu kwa kila swali nimekutumia kwenye private msg.
 
Huenda! Ila hospital nimefanyiwa vipimo vya x-ray, ECG n.k havijaonyesha tatizo labda huenda bado sijapata vipimo sahihi na wataalamu sahihi!
 
Yaani kifua kinaniuma ,kilianza kama miti miwili inanichoma kwa muda fulani halafu inaacha!

Hospital wamekuwa wakidai nipige x-ray za kifua nazo zinaonyesha hakuna tatizo!

😥😥😥
Wadau hili tatizo limenirejea kwa nguvu za ajabu!Kifua kinaniuma katikati mithili ya kidonda!Vipimo vya hospitali havionyeshi ugonjwa😭😭Daktari niliyeonana naye hivi karibuni anadai ni vidonda vya tumboni vimehamia kifuani😭😭!!Msaada wenu tafadhali
 
Back
Top Bottom