1985, 1987 na 1991
Pole kwa hilo dhahama. Bro, ukiwa unatafuta ushauri kwa mambo mazito kidogo, upe uandishi wako uzito, sina hakika kama tuna matumizi na X kwenye kiswahili chetu, kidogo inasababisha ukakasi.
Tukirudi kwenye mada, HUNA utakaloweza kufanya kurekebisha hiyo tabia ya bwana mdogo wako. Ni tatizo common kwa kila familia, kuna mmoja kati yenu atakuwa fyatu tu na ndio unakuta anawekwa chini ya mbawa za wazee.
Mnaishi nyumba ya familia au kila mtu ana kwake? Hao watoto wanaletwa kwako kwa kigezo cha kuwapeleka kwa bibi au ndio wanaletwa kwa mlezi wa wana wewe?
Unachoweza kufanya, kama unao moyo huo; huyo bwana kuwa muajiriwa inatosha kusema kila anachofanya ana kielewa. Sasa wewe usielewe anachokifanya.
Aaargh, kila nikijaribu kukushauri cha kufanya, naona kabisa nitakuwa nakudanganya tu kwakuwa tunazo kesi kama hizo kwa kila uzao wa baba zetu, kuna mwingine anaingia 50 Dec, watoto wanalelewa na ma-grand na wadogo zake, ikiwa na yeye mwenyewe pia anakaa kwa mzee. Mwingine naye ana watoto wanane, kila mmoja na mama'ake, mwingine anaingia 4th floor hivi karibuni, hatujui anakoishi, kama ana kazi au hana, anajua kila nyumbani kwa ndugu, ndio jinsi tunavyokutana nae.
Hao wote ni kutoka kwa familia tofauti. Ila ni mara chache kukuta uzao wa pili unakuwa chenga, ama wa kwanza au wa mwisho.
Bro, we fanya unavyoona nafsi yako inakuelekeza kufanya, mi sihangaiki na mijitu ambayo inaweza kujitetea, watoto hawawezi kujitetea, wanakuhitaji ILA pia wema ukizidi uwezo, ni dhambi wanasema waumini.