Naombeni ushauri nimekuwa mlevi kupindukia msaada wa mawazo nimejaribu kuacha nimeshindwa
Gharama za Pombe:
Matumizi ya kununua pombe ni mojawapo ya gharama kubwa katika familia yenye wanywaji wa pombe. Wanywaji hutumia wastani wa saa moja mpaka tisa (Zaidi ya robo siku) katika unywaji wa pombe na hunywa wastani wa bia 3 mpaka 20 kulingana na uwezo kifedha na uhimili.
Nchini Tanzania wastani wa bei ya bia moja ni sh 2,000.
Bia 3=2,000x 3=6,000/= (Shilingi Elfu Sita za Tanzania)
Bia 10 =2,000×10= 20,000/= (Shilingi Elfu Ishirini za Tanzania)
Bia 20= 2,000×20=40,000/= (Shilingi Elfu Arobaini za Tanzania)
Matumizi Kwa Mwezi: Hutumia kati ya shilingi 180,000, 600,000 na 1,200,000
Hizi ni fedha nyingi sana.
Lakini pombe haiendi peke yake,kuna chakula na vitafunwa (Nyama choma,samaki,supu n.k) hivi vinaleta gharama nyingine karibu sawa na hesabu za bia.
Unaweza ukazidisha mara mbili katika gharama za awali na utapata matumizi ya kati ya shilingi za kitanzania 360,000,1,200,000 mpaka 2,400,000 kwa mwezi.