Naombeni ushauri nimekuwa mlevi kupindukia, nimejaribu kuacha nimeshndwa

Naombeni ushauri nimekuwa mlevi kupindukia msaada wa mawazo nimejaribu kuacha nimeshindwa

Gharama za Pombe:

Matumizi ya kununua pombe ni mojawapo ya gharama kubwa katika familia yenye wanywaji wa pombe. Wanywaji hutumia wastani wa saa moja mpaka tisa (Zaidi ya robo siku) katika unywaji wa pombe na hunywa wastani wa bia 3 mpaka 20 kulingana na uwezo kifedha na uhimili.

Nchini Tanzania wastani wa bei ya bia moja ni sh 2,000.

Bia 3=2,000x 3=6,000/= (Shilingi Elfu Sita za Tanzania)

Bia 10 =2,000×10= 20,000/= (Shilingi Elfu Ishirini za Tanzania)

Bia 20= 2,000×20=40,000/= (Shilingi Elfu Arobaini za Tanzania)

Matumizi Kwa Mwezi: Hutumia kati ya shilingi 180,000, 600,000 na 1,200,000

Hizi ni fedha nyingi sana.

Lakini pombe haiendi peke yake,kuna chakula na vitafunwa (Nyama choma,samaki,supu n.k) hivi vinaleta gharama nyingine karibu sawa na hesabu za bia.

Unaweza ukazidisha mara mbili katika gharama za awali na utapata matumizi ya kati ya shilingi za kitanzania 360,000,1,200,000 mpaka 2,400,000 kwa mwezi.
 
Naombeni ushauri nimekuwa mlevi kupindukia msaada wa mawazo nimejaribu kuacha nimeshindwa

Madhara ya Unywaji wa Pombe Kijamii

Madhara ya Unywaji wa pombe yako wazi kabisa katika jamii. Majumbani,sehemu za kazi na hata mitaani. Madhara haya ni kama ifuatavyo:
  • Ukosefu wa staha na maadili– Katika ulevi watu wanakosa kujiheshimu, mfano matumizi ya lugha za matusi,ugomvi na hata kujisaidia hadharani ni vitu vinavyotokea.
  • Ubakaji na Ukatili– Katika hali ya ulevi matukio ya ubakaji na ukatili yamelipotiwa majumbani na mitaani
  • Kuvunjika kwa Mahusiano na Familia- Familia nyingi zinavunjika kutokana na ulevi wa wenza wote au mmojawapo
  • Kushuka kwa Heshima: Heshima toka kwa jamii inayokuzunguka toka katika familia yako hadi nje itashuka kutokana na mambo unayoyafanya ukiwa umelewa.
  • Kukosa Muda na Familia: Walevi wanatumia muda mwingi katika unywaji na hivyo kuwa na muda kidogo na familia zao na hivyo kukosa mshikamano na wenza wao na watoto.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom