Naombeni ushauri nifanye nini juu ya watu hawa

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,773
3,471
Habari za wakati huu wana MMU, nimekutana na hili sehemu mbili tofauti. Unakutana na mtu eneo fulani, tangia kupoteana yafika kama miaka 4 hamjaonana, tangia mko kijijini mlipotoka.

Unafurahi, unatabasamu kwa sana lakini mwenzangu wapi, hana hata furaha, sijui hii inakuaje wakati huo mimi niko na kazi yangu sio kwamba nataka kumuomba msaada.

Wenzangu ambao tayari limewakuta/ halijawakuta hili niambieni nifanye nini, pindi nitakapokutana nao tena watu wa design kama hii.
 
Sio kwamba hana furaha ya kukutana na wewe,pengine mwenzako yupo kwenye matatizo ya kimaisha au kiafya au matatizo mengine tu,

Ulitakiwa kumuuliza; "Mbona unaonekana huna furaha?,au una maatatizo yeyote ndugu yangu?"

Sio kuanza kufikiria eti hakuonyesha furaha kwavile alihisi labda ulitaka kumuomba msaada,

Halafu kama vile umepotea jukwaa!! Hili sio jukwaa la MMU
 
Kuna watu mnakosa cha kuandika kabisa! Uzi gani sasa umeweka huo? Yaani mtu kukununia ndo ulete uzi hapa? Aisee JF kwa sasa haina tofauti na facebook.
 
Na pia ukumbuke sio kila tabasamu limebeba upendo ama amani ama furaha, watu Wanna stress zao za maisha hasa msimu huu wa sikukuu.
 
[QUOTECiprofloxacin.;14918350]Kuna watu mnakosa cha kuandika kabisa! Uzi gani sasa umeweka huo? Yaani mtu kukununia ndo ulete uzi hapa? Aisee JF kwa sasa haina tofauti na facebook.[/QUOTE]

Hujalazimishwa kuandika chochote, ukiona inakuboa pita zako, sio kila uzi unaowekwa unataka uonekane unajua. Samahani ikiwa nimekukera.
 
Back
Top Bottom