Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Bwajilo

JF-Expert Member
Dec 5, 2021
345
880
Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu.

Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.

Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.

Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?

Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.

Je, ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa.

Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu
 
Pole kwa changamoto ila kiuhalisia mama anahitaji mtu wa kumpa kampani.

Tatizo ni kwamba huyo mzee anataka ahamie kwenu hili ndio linakupa ukakasi.

Mama yako ndio anae olewa so ni vema akaenda kwa mumewe na sio yeye kumleta senior marioo hapo kwenye mji wa family yenu
 
Pole kwa changamoto ila kiuhalisia mama anahitaji mtu wa kumpa kampani
Tatizo ni kwamba huyo mzee anataka ahamie kwenu hili ndio linakupa ukakasi
Mama yako ndio anae olewa so ni vema akaenda kwa mumewe na sio yeye kumleta senior marioo hapo kwenye mji wa family yenu
Hii ndio hofu yangu kubwa.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ni rahisi sana kuchangia, na kushauri omba usikutane na kadhia ya mzazi asiye na busara mbele ya watotinwake, inaumiza sana, utaanza kufikiria toka mbali labda ili zee.lilikuwa linamuibia baba.

Siku nyingi, sasa kama kuoa kwa.nini.asiwe.resposible.kumbeba mke.wake kumpeleka kwake au kumpangishia.nyumba? Hata hivyo kuna.baadhi ya makabila mwanamke huwa hakubali kuzeeka
 
Pole mkuu sisi katika UISLAM mtoto wa kiume tunaruhusiwa hata kuozesha MAMAAKO

NIkweli kwa umri wake na ukizingatia mumewe amefariki muda si mrefu ilipaswa apumzike

lkn wewe inaonesha wasiwasi wako sio mama ni umasikini wa huyo mzee

Nikuulize angetokea mtu mwenye pesa na kujiweza mwenye magari majumba na biashara zake je ungekubari aolewe ?
 
Mama Kuolewa hilo huwezi kuzuia kama wengi wanavyo sema, ila kuolewa halafu aendelee kuishi na huyo mwanaume hapo nyumbani hilo linaleta ukakasi kwa kweli. Mwanaume aoe aende naye kwake na sio yeye ahamie hapo nyumbani hilo hapana.
 
Back
Top Bottom