Naombeni ushauri nahisi wasipotoa ajira nitaokota makopo

kweli ajira imekuwa ni changamoto kubwa ifike mahali serikali ifikirie kwa makini hili suala,kama serikalu hawaajiri wafungue milango ya ajira kwa kutumia private sector,wabuni njia mbalimbali za vijana kujiajir,ila kwa mwendo wa awamu hii hata kupata kazi private sector ni ngumu sana kwanza kila kukicha wanapunguza watu,
 
Fungua tution inalipa itakupunguzia wenge.WE LALA UONE KAMA MTU ATAKUJA KUKUAMSHA UTAJIKUTA UNAOKOTA KWELI MAKOPO UTUSAFISHIE JIJI.
 
pole sana ila kunanamna nyigi za kupata ajira usifokirie kwajiriwa naserikali tu. jaribu ata kutoka nje nchi jilani utapata kazi kwamfano Rwanda wanahitaji waalimu wakiswahili nk
 
Pole sana!!

Huwa nawaza kichwani mwangu mwalimu huwa hakosi kazi.

Kama uko kijijini kuna shule basi nenda ujitolee upate japo ya chai tu, kama ni mwalimu wa sayansi utapata tu darasa la kufundisha kuna uhaba mkubwa sana.

Lakini unaweza pia kuanzisha kashule hata kachekea tu

usiwaze sana ajira ya serikali
 
huku town mzee wala usirogwe kuja... kuna kundi kubwa wanataman bora wangekuwa bush angalau wangejua cha kufanya!!!!
hali ni mbaya vibaya haupo peke yako mkuu..!!!!
 
Lakini 2016 mbona hata hujasota sana,hata hivyo mpango uliopo ni wa kuajiri walimu wa sayansi na hisabati wale wa mwaka 2015 na kurudi nyuma japokuwa hili nalo limekuwa kama wimbo kila siku hizo ajira zinatangazwa upya. Sasa mpaka mje mkumbukwe nyie wa 2016 inaweza kuwa 2050.
 
Mwanakijiji Ligusi nenda mtaa wa ufipa pale wanaajiri mkuu
Wanabodi naombeni ushauri Mimi ni mwalimu niliyehitimu masomo yangu mwaka 2016 hakika mpaka sasa sijui hatma yangu na umri unasonga na nilisomea ualimu nikijua huku.

Ajira nje nje lakini cha ajabu mpaka sasa hakuna tamko lolote juu ya ajira zetu na huku kijijini kila anaamn nilifeli paper la chuo na demu wangu ameshanikimbia sasa mpaka sasa sijui cha kufanya na kila nikiwapigia simu ndugu zangu huko mjini ili niende nilawasalimie naa wao pia wananipiga chenga ili nisiende town.

Sasa naona maji yamenifika shingoni naombeni msaada wenu wa kimawazo
Unapewa bando kwa ajili ya kusambaza propaganda.
Haupo kijijin kama unavosema acha zako
 
Katafute mbegu za mchicha mahali popote. Otesha. Kwenye mvua hii baada ya wiki chache utauza mchicha. Ukipata hata elfu hamsini endelea. Tafuta mahali penye maji ya kumwagilia. Lima hapo. Otesha mboga mbalimbali. Baada ya miezi 6 kipato chako kitazidi hata mshahara wa ualimu. Kamwe usikate tamaa. Maisha yako hivi: Unapoona changamoto ni nyingi sana baada ya muda kidogo tu maisha yako yatachanua
Sina neno umelitendea haki jina lako la JF.
 
Back
Top Bottom