Naombeni ushauri nahisi wasipotoa ajira nitaokota makopo

mwanakijiji lugusi

Senior Member
Apr 13, 2016
128
96
Wanabodi naombeni ushauri Mimi ni mwalimu niliyehitimu masomo yangu mwaka 2016 hakika mpaka sasa sijui hatma yangu na umri unasonga na nilisomea ualimu nikijua huku.

Ajira nje nje lakini cha ajabu mpaka sasa hakuna tamko lolote juu ya ajira zetu na huku kijijini kila anaamn nilifeli paper la chuo na demu wangu ameshanikimbia sasa mpaka sasa sijui cha kufanya na kila nikiwapigia simu ndugu zangu huko mjini ili niende nilawasalimie naa wao pia wananipiga chenga ili nisiende town.

Sasa naona maji yamenifika shingoni naombeni msaada wenu wa kimawazo
 
Pole sana! Jaribu kuomba kazi kwenye shule binafsi. Mbali na hapo jikite kwenye kilimo cha gharama nafuu kama bustani za mbogamboga na mihogo. Lakini pia fuga hata kuku wa kienyeji kwaajili ya mahitaji madogomadogo.
 
Wanabodi naombeni ushauri Mimi ni mwalimu niliyehitimu masomo yangu mwaka 2016 hakika mpk SASA cjui hatma yangu NA umri unasonga NA nilisomea ualimu nikijua huku Ajira nje nje lkn cha ajabu mpk SASA hakuna tamko lolote JUU ya Ajira zetu NA huku kijijini kila MTU anaamn nilifeli paper LA chuo NA demu wangu ameshanikimbia SASA mpk SASA sijui cha kufanya NA kila nikiwapigia cm ndg zangu HUKO mjini ili niende nilawasalimie NA wao pia wananipiga chenga ili nisiende town.

SASA naona Maji yamenifika shingoni naomben msaada wenu WA kimawazo
Kama uko kijijini na vyua zinanyesha basi ww utakua mzembe. achana na habari za kusubiri ajira kwani utakufa kwa mawazo. mimi nimesubiri ajira kuanzia 2015 na nmekonda kwa mawazo. sasa nimefikia umamuzi wa kwenda Morogoro kuanza kilimo cha mahindi. naamini nitatoka, na nikitoka nawaachia ualimu wao wa sayansi yao uchwara ya nadharia.
 
Hahaha sayansi yao uchwara ya nadharia sio duuh hongera mkuu umenikata mbavu
 
Anzisha ka tuition hapo kijijini kwa mda kwanza.. Au chekechea kama wewe ni mwalimu wa msingi, Ukiwa na ajira mojja wapo weka banda la mboga mboga ufanye multi task upate hata tu pesa ka tu bando cha kujifariji huku ukisubiria ajira yako,​
 
Mkuu pole sana Kwa kukosa ajira ya ualimu.
Kama kweli Wewe ulisomea ualimu basi wanafunzi wako watarajiwa watakuwa Na wakati mgumu.
Mwalimu ni Mfano wa kuigwa Na wanafunzi wako.Kutokana Na maandishi yako.Tafuta ajira nyingine.
 
Katafute mbegu za mchicha mahali popote. Otesha. Kwenye mvua hii baada ya wiki chache utauza mchicha. Ukipata hata elfu hamsini endelea. Tafuta mahali penye maji ya kumwagilia. Lima hapo. Otesha mboga mbalimbali. Baada ya miezi 6 kipato chako kitazidi hata mshahara wa ualimu. Kamwe usikate tamaa. Maisha yako hivi: Unapoona changamoto ni nyingi sana baada ya muda kidogo tu maisha yako yatachanua
 
Kiukweli hii serikali imewaonea sana haikuwaandalia mazingira ila hawa wanaowafuatia nyuma wamejifunza
Hasa mliosomea masomo ya art
 
Wanabodi naombeni ushauri Mimi ni mwalimu niliyehitimu masomo yangu mwaka 2016 hakika mpk SASA cjui hatma yangu NA umri unasonga NA nilisomea ualimu nikijua huku Ajira nje nje lkn cha ajabu mpk SASA hakuna tamko lolote JUU ya Ajira zetu NA huku kijijini kila MTU anaamn nilifeli paper LA chuo NA demu wangu ameshanikimbia SASA mpk SASA sijui cha kufanya NA kila nikiwapigia cm ndg zangu HUKO mjini ili niende nilawasalimie NA wao pia wananipiga chenga ili nisiende town.

SASA naona Maji yamenifika shingoni naomben msaada wenu WA kimawazo

komaa maisha ndo hivyo tena.....
 
Kiukweli hii serikali imewaonea sana haikuwaandalia mazingira ila hawa wanaowafuatia nyuma wamejifunza
Hasa mliosomea masomo ya art
Sina uhakika kama kuna wanachojifunza hao vijana maana wengi wao akili zao ni za mwendo kasi!
 
Sina uhakika kama kuna wanachojifunza hao vijana maana wengi wao akili zao ni za mwendo kasi!
Watasumbuka sana wengi kipindi hiki maana Tz bado kuamka elimu bado haina msaada kama mbele hawakuoni tutegemee neno ajira kuzidi kutamkwa muda wote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom