Naombeni ushauri mie nina huruma sana

Naombeni ushauri mie nina huruma sana

Yaani Mimi nimekuwa MTU wa kuumizwa sana na marafiki sijui mashost, sasahivi sitaki upumbavu, nitamsaidia ndugu yangu wa damu, au mtoto na mume wangu.... Sitaki ushambenga!
[emoji22][emoji22]pole hata mm vivyo hivyo
 
Kuna dada mmoja alikuwa na ujauzito akawa anakuja kwangu Kila Siku... Siku moja akaniropokea Kwamba Mimi napika mboga za 200!! Kila siku hapo ashakula kwangu km miezi 8 bado kidogo ajifungue
 
Mkuu kwenye maisha ni lazima uvae ukauzu na uwe strict na malengo yako.
Punguza kukopesha watu wasiokujali wewe wakati una shida. Na pili pesa zako zipangie malengo mapema zikitoka unazipeleka huko.Kukaa na pesa kwenye acc ndio chanzo cha ww kugawa.
Asante mkuu maana mie pia mhanga wa jambo hili
 
Ndugu zanguni nimefika mbele yenu hapa kwa lengo la kuomba ushauri wenu .Ni kijana mwenye umri wa miaka 24 sina mke wala mtoto . Ninajituma kwa juhudi zangu kuhakikisha natengeneza maisha yenye unafuu kidogo .huwa napita mengi lakini sijawahi kushikwa mkono hata niombapo msaada,

Lakini mimi ninapojituma kwa juhudi zangu basi marafiki zangu hutafuta sababu mara niwaazime pesa mara nimsaidie ,inafika sehemu naingiwa na huruma kabisa najitaidi kutoa kulingana na uwezo wangu, ila mm nikijaribu kuomba nikiwa na shida huwa sipati zaidi ya kwa mzee wangu au mama yangu wa kambo pekee ndo wenye misaada tosha ila wengine wanakana nikiwaomba ,lkn wao wanahitaji msaada wa hali na mali mpk nafikia stage naona kama msalaba vile .. mpaka inafika sehemu nawaza kwann mimi ni mtu wa kutoa tu lkn kupokea ni ngumu ?

MUDA MWINGINE NDUGU ZANGU, JAMAA ZANGU HUNIANGUSHA KWA ASILIMIA KUBWA KABISA UNAMKOPA NA UKISHAMKOPA BASI NDO HATIMA YA WW NA YY KUONANA WABAYA ILA YOTE KWA YOTE MIE NAJALI UTU ZAIDI .

ILA MPAKA SASA UZALENDO UMENISHINDA YAAI MSHAHARA WANGU 300K KWA MWEZI UNAKUTA WALIONIOMBA NIWAKOPE SI CHINI YA 2 MFANO HUYU HAPA

Kaka nlikwepo na shida na kiasi cha pesa man, nataka nitangulze kwenye kodi please niazime elfu hamsini ntairudisha chuo kikifunguliwa mzeee ,Naomba unipe majbu broooo ntafte namna kma ikshindkana.

Na bado kuna wengine .. huwa najiuliza au umasikini unanitafuna mie .

USHAURI WENU NI MUHIMU SANA
Kijana , siku zote usiwe mwepesi kutoa misada hata iweje, penda kusave sana mtu pekee akikuomba msaada ambae huto sita ni wazazi wako tu. Alafu toa 10% ya unayoombwa, mtu anakuomba umkope 54000/- mwambie nina 5000 tu hapo ndo nayoweza kukuazima na mimi niko tight. Pia usipende kukaa na pesa mvukoni au kutembea sana na ATM card. Umri wako ni mzuri kwa kuanza kusave. Maana ukiwa na familia salary ya 300k unaweza shindwa fanya saving.
 
Kuna dada mmoja alikuwa na ujauzito akawa anakuja kwangu Kila Siku... Siku moja akaniropokea Kwamba Mimi napika mboga za 200!! Kila siku hapo ashakula kwangu km miezi 8 bado kidogo ajifungue
Mimi kuanzia sasa heri lawama kuliko hasara maana kila nikikopa lazima ntadhurumiwa hata nikilipwa huwa nadra sana
 
Kijana , siku zote usiwe mwepesi kutoa misada hata iweje, penda kusave sana mtu pekee akikuomba msaada ambae huto sita ni wazazi wako tu. Alafu toa 10% ya unayoombwa, mtu anakuomba umkope 54000/- mwambie nina 5000 tu hapo ndo nayoweza kukuazima na mimi niko tight. Pia usipende kukaa na pesa mvukoni au kutembea sana na ATM card. Umri wako ni mzuri kwa kuanza kusave. Maana ukiwa na familia salary ya 300k unaweza shindwa fanya saving.
Shukrani mkuu nami nishagundua ugonjwa wangu .
 
Kuna dada mmoja alikuwa na ujauzito akawa anakuja kwangu Kila Siku... Siku moja akaniropokea Kwamba Mimi napika mboga za 200!! Kila siku hapo ashakula kwangu km miezi 8 bado kidogo ajifungue
Tenda wema nenda zako
 
Mnafundishana tabia mbaya za uchoyo na umimi
Sio kweli mkuu. Labda hayajakukuta au labda umejaaliwa sana kiasi kwamba hata ukitoa huoni kupungukiwa.

Tatizo linakuja pale ambapo hali yako ni mbaya hata mwenyewe hujimudu ila kutokana na kuguswa na shida ya mtu mwingine unajitoa kwaajili yake kwa ahadi ya kurejeshewa ila baada ya kutoa inageuka kuwa uadui.

Hapo ndipo mtu unaingiwa na moyo wa kutomwamini mtu maana binadamu tunajijua sisi wenyewe
 
Huo ni woga wa maisha unaogopa kumkatalia MTU kwa ajili ya kudhani atakuonaje au atashindwa kukusaidia ukiwa na matatizo. Toa kitu kwa sababu unanafasi ya kufanya hivyo usitoe kwa sababu ya kutegemea returns yeyote

Numbisa
 
Ndugu zanguni nimefika mbele yenu hapa kwa lengo la kuomba ushauri wenu .Ni kijana mwenye umri wa miaka 24 sina mke wala mtoto . Ninajituma kwa juhudi zangu kuhakikisha natengeneza maisha yenye unafuu kidogo .huwa napita mengi lakini sijawahi kushikwa mkono hata niombapo msaada,

Lakini mimi ninapojituma kwa juhudi zangu basi marafiki zangu hutafuta sababu mara niwaazime pesa mara nimsaidie ,inafika sehemu naingiwa na huruma kabisa najitaidi kutoa kulingana na uwezo wangu, ila mm nikijaribu kuomba nikiwa na shida huwa sipati zaidi ya kwa mzee wangu au mama yangu wa kambo pekee ndo wenye misaada tosha ila wengine wanakana nikiwaomba ,lkn wao wanahitaji msaada wa hali na mali mpk nafikia stage naona kama msalaba vile .. mpaka inafika sehemu nawaza kwann mimi ni mtu wa kutoa tu lkn kupokea ni ngumu ?

MUDA MWINGINE NDUGU ZANGU, JAMAA ZANGU HUNIANGUSHA KWA ASILIMIA KUBWA KABISA UNAMKOPA NA UKISHAMKOPA BASI NDO HATIMA YA WW NA YY KUONANA WABAYA ILA YOTE KWA YOTE MIE NAJALI UTU ZAIDI .

ILA MPAKA SASA UZALENDO UMENISHINDA YAAI MSHAHARA WANGU 300K KWA MWEZI UNAKUTA WALIONIOMBA NIWAKOPE SI CHINI YA 2 MFANO HUYU HAPA

Kaka nlikwepo na shida na kiasi cha pesa man, nataka nitangulze kwenye kodi please niazime elfu hamsini ntairudisha chuo kikifunguliwa mzeee ,Naomba unipe majbu broooo ntafte namna kma ikshindkana.

Na bado kuna wengine .. huwa najiuliza au umasikini unanitafuna mie .

USHAURI WENU NI MUHIMU SANA
Kwanza nakupongeza kwa moyo wa utoaji ubarikiwe.

Pili, naomba ufahamu kuwa unapotoa kitu usitegemee kurudishiwa. Wanasemaga Tenda wema nenda zako usingoje shukurani.

Tatu, ndugu akopeshwi ila anapewa.
Kama unaona una kidogo usimpatie ndugu.
ASANTE
 
Pata chuma ulete kwangu wakopeshe tu hata Millioni Moja moja kwa kila mtu lkn mwisho wa siku zina rudi kwako zote kwa njia ya kichawi!!! hapo ujue wewe bado unawadai tu!!! watakukimbia wenyewe wote hao!

Tena ukitaka komesha bwege ya chuma ulete!! akichukua hela zako. kosa tu akichanganya na zake inakomba na zake zote!! zina kuja kwako uwakomeshe!! unazidi kuwa tajiri!! hata akiaguliwa akajua chuma ulete yako wewe kuwa Bishi tuuu!! halafu mseme sana km hivi...

Yaani kukukopesha hela zangu unani bambika uchuma ulete tena, kweli??? kumbe wew chawi? yaaani uwiiiii!! nyie ndugu hamna wema!! leta pesa yangu kwanza acha utani wa kitoto!! ulishaona wapi huu ujinga wa chuma ulete??? eee!! nakuuliza wewe?

Umeanza lini uganga weee!! chizi weee!!!! ndo unaibia watu kijinga hivo badala ya kufanya kazi? wewe mwizi siku hizi?
 
Back
Top Bottom