Naombeni ushauri mie nina huruma sana

ashomile

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,625
2,442
Ndugu zanguni nimefika mbele yenu hapa kwa lengo la kuomba ushauri wenu .Ni kijana mwenye umri wa miaka 24 sina mke wala mtoto . Ninajituma kwa juhudi zangu kuhakikisha natengeneza maisha yenye unafuu kidogo .huwa napita mengi lakini sijawahi kushikwa mkono hata niombapo msaada,

Lakini mimi ninapojituma kwa juhudi zangu basi marafiki zangu hutafuta sababu mara niwaazime pesa mara nimsaidie ,inafika sehemu naingiwa na huruma kabisa najitaidi kutoa kulingana na uwezo wangu, ila mm nikijaribu kuomba nikiwa na shida huwa sipati zaidi ya kwa mzee wangu au mama yangu wa kambo pekee ndo wenye misaada tosha ila wengine wanakana nikiwaomba ,lkn wao wanahitaji msaada wa hali na mali mpk nafikia stage naona kama msalaba vile .. mpaka inafika sehemu nawaza kwann mimi ni mtu wa kutoa tu lkn kupokea ni ngumu ?

MUDA MWINGINE NDUGU ZANGU, JAMAA ZANGU HUNIANGUSHA KWA ASILIMIA KUBWA KABISA UNAMKOPA NA UKISHAMKOPA BASI NDO HATIMA YA WW NA YY KUONANA WABAYA ILA YOTE KWA YOTE MIE NAJALI UTU ZAIDI .

ILA MPAKA SASA UZALENDO UMENISHINDA YAAI MSHAHARA WANGU 300K KWA MWEZI UNAKUTA WALIONIOMBA NIWAKOPE SI CHINI YA 2 MFANO HUYU HAPA

Kaka nlikwepo na shida na kiasi cha pesa man, nataka nitangulze kwenye kodi please niazime elfu hamsini ntairudisha chuo kikifunguliwa mzeee ,Naomba unipe majbu broooo ntafte namna kma ikshindkana.

Na bado kuna wengine .. huwa najiuliza au umasikini unanitafuna mie .

USHAURI WENU NI MUHIMU SANA
 
Naomba unisaidie kaka kama 54k hivi...
Acha utani ndugu nielewe nipo serious mie huwa namsaidia kwa ninaefahamiana nae face 2 face tena wale marafiki nilosoma nao pia makaka zangu pamoja na wadogo wangu
 
Ww nisawa nawale walipa deni wazuri wakikopeshwa lkn wao wakikopesha kulipwa ni mbinde .."DUNIA HAINA HURUMA" ila ukianza majukumu yakifamilia (mke na mtt) utarud tu nyuma mwenyewe nautajiuliza ndo mimi kweli nilokuaga shirika la misaada
 
Heri wenye Mioyo safi, Maana ufalme wa Mbinguni ni wao!
Ndio kwanza ana miaka 24 hata maisha ya duniani hajayaanza. Atateseka sana kwa hii tabia mpaka atakapokuja ukipata huo ufalme wa. mbinguni.
 
Hakuna msaada wa upande mmoja kama ukiwa na shida wanakukimbia
na wao wakiwa na shida wakimbie

huwezi kuwa Yesu maisha haya
Shukrani sana kibaya nahofia kupoteza undugu na urafiki wa kudumu
 
Bora kubaki na,marafiki wachache kuliko
kuwa,na marafiki wengi halafu hawana
msaada wowote.

Fyekerea mbali marafiki wasio na faida!!
Barikiwa sana ndugu yangu nami ntajitaidi niwapunguze tu, hata wakinichukia haina namna maana uzalendo umenishinda
 
Ni kheri kukaa mwenyewe kuliko kuishi na rafiki kupe.
Kweli ndugu yangu mpaka kichwa kinauma yaani kujituma kwako unufaishe asiye na manufaa kwako na hata ukikosa msaada hana zaidi ya kusema hana .
 
Ww nisawa nawale walipa deni wazuri wakikopeshwa lkn wao wakikopesha kulipwa ni mbinde .."DUNIA HAINA HURUMA" ila ukianza majukumu yakifamilia (mke na mtt) utarud tu nyuma mwenyewe nautajiuliza ndo mimi kweli nilokuaga shirika la misaada
Ndugu yangu inaniumiza sana sema moyo niliopewa sijui ni moyo gani !! Nikielezwa shida ya mtu huwa naona kama shida yangu na natamani aitatue tu ndo maana naishia kuwa mtu wa kurudishwa nyuma .pesa silipwi hata nikiazima mtu na nikilipwa basi imekaa kwa muda mrefu
 
Ndio kwanza ana miaka 24 hata maisha ya duniani hajayaanza. Atateseka sana kwa hii tabia mpaka atakapokuja ukipata huo ufalme wa. mbinguni.
Daah ndugu yangu mie ni mpambanaji haswa na napambania maisha yangu . Hata nikipita mateso huwa nashukuru sababu sipati msaada wowote zaidi ya kuambiwa hana au ushauri pambana
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Mkuu kwenye maisha ni lazima uvae ukauzu na uwe strict na malengo yako.
Punguza kukopesha watu wasiokujali wewe wakati una shida. Na pili pesa zako zipangie malengo mapema zikitoka unazipeleka huko.Kukaa na pesa kwenye acc ndio chanzo cha ww kugawa.
 
Mkuu kwenye maisha ni lazima uvae ukauzu na uwe strict na malengo yako.
Punguza kukopesha watu wasiokujali wewe wakati una shida. Na pili pesa zako zipangie malengo mapema zikitoka unazipeleka huko.Kukaa na pesa kwenye acc ndio chanzo cha ww kugawa.
Asante sana kwa ushauri
 
Back
Top Bottom