Naombeni ushauri mie nina huruma sana

Naombeni ushauri mie nina huruma sana

Wasaidie wazazi pekee over.. Utapiga marktime mpk basi ndugu marafiki wengi uangalie wale ambao mnasaidiana tu wengine potezea
Sijawahi kuwa na rafiki wa kunisaidia mimi kwa kweli wengi wao ndo wanileteao shida na kujifanya wakaribu yangu
 
Kutoa ni moyo kama unacho watu wa kariba yako walishakufa kwenye vita ya pili ya dunia
 
Kama unatoa hela toa hela kidogo ambayo usiipigie mahesabu kama inarudi, mtu amekuja kukukopa laki, unamwambia saivi nimebanwa sana sina ela chukua hii ten itakusaidia
 
Jifunze kusema hapana ,sina ,siko vizuri
 
Jifunze kusema hapana ,sina ,siko vizuri
 
Usitoneshe vidonda mkuu wengine tuna maumivu sugu.

Nawaachia wahusika wakuhukumu tu mimi siwezi kitu.
 
Huruma ikizidi sana dhambi aisee

Kuna paka niliikopesha hadi Leo haikumbuki kulipa
 
Ndugu zanguni nimefika mbele yenu hapa kwa lengo la kuomba ushauri wenu .Ni kijana mwenye umri wa miaka 24 sina mke wala mtoto . Ninajituma kwa juhudi zangu kuhakikisha natengeneza maisha yenye unafuu kidogo .huwa napita mengi lakini sijawahi kushikwa mkono hata niombapo msaada,

Lakini mimi ninapojituma kwa juhudi zangu basi marafiki zangu hutafuta sababu mara niwaazime pesa mara nimsaidie ,inafika sehemu naingiwa na huruma kabisa najitaidi kutoa kulingana na uwezo wangu, ila mm nikijaribu kuomba nikiwa na shida huwa sipati zaidi ya kwa mzee wangu au mama yangu wa kambo pekee ndo wenye misaada tosha ila wengine wanakana nikiwaomba ,lkn wao wanahitaji msaada wa hali na mali mpk nafikia stage naona kama msalaba vile .. mpaka inafika sehemu nawaza kwann mimi ni mtu wa kutoa tu lkn kupokea ni ngumu ?

MUDA MWINGINE NDUGU ZANGU, JAMAA ZANGU HUNIANGUSHA KWA ASILIMIA KUBWA KABISA UNAMKOPA NA UKISHAMKOPA BASI NDO HATIMA YA WW NA YY KUONANA WABAYA ILA YOTE KWA YOTE MIE NAJALI UTU ZAIDI .

ILA MPAKA SASA UZALENDO UMENISHINDA YAAI MSHAHARA WANGU 300K KWA MWEZI UNAKUTA WALIONIOMBA NIWAKOPE SI CHINI YA 2 MFANO HUYU HAPA

Kaka nlikwepo na shida na kiasi cha pesa man, nataka nitangulze kwenye kodi please niazime elfu hamsini ntairudisha chuo kikifunguliwa mzeee ,Naomba unipe majbu broooo ntafte namna kma ikshindkana.

Na bado kuna wengine .. huwa najiuliza au umasikini unanitafuna mie .

USHAURI WENU NI MUHIMU SANA
Sasa iyo ni huruma,ungekuwa na huruma ungesamehe watu madhambi yao,au ungesaidia yatima na wazee na wasiojiweza,,,,,huo mchezo unaitwa kujipendekeza na kukosa mpangilio wa fedha istoshe hela yako haina matumizi
 
Yaani haya mambo yanakera sana, wengine ukiwapa ndio wanajenga mazoea ya kukuomba kila wiki, hadi unajuta kumpa
 
Sasa iyo ni huruma,ungekuwa na huruma ungesamehe watu madhambi yao,au ungesaidia yatima na wazee na wasiojiweza,,,,,huo mchezo unaitwa kujipendekeza na kukosa mpangilio wa fedha istoshe hela yako haina matumizi
Yaani Mimi nimekuwa MTU wa kuumizwa sana na marafiki sijui mashost, sasahivi sitaki upumbavu, nitamsaidia ndugu yangu wa damu, au mtoto na mume wangu.... Sitaki ushambenga!
 
kama umeshabaini tatizo lako basi lifanyie kazi bora lipi umwambie mtu pesa huna mbakie kuwa marafiki daima au umkopeshe pesa zako hlf asikulipe na mgeuke kuwa maadui????

Tafakali chukua hatua. msaidie anayekusaidia.
 
Sasa iyo ni huruma,ungekuwa na huruma ungesamehe watu madhambi yao,au ungesaidia yatima na wazee na wasiojiweza,,,,,huo mchezo unaitwa kujipendekeza na kukosa mpangilio wa fedha istoshe hela yako haina matumizi
Asante kwa ushauri
 
Back
Top Bottom