Naombeni Ushauri kuhusu hii simu!

Naombeni Ushauri kuhusu hii simu!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,146
Reaction score
7,685
Habarini....Najua hapa nitapata ushauri wa kuaminika ambao ni msaada mkubwa sana kwangu!

Mimi sijawahi kutumia IPHONE lakini hivi karibuni niliamua kutumia iphone nikamuagiza mtu aninunulie iphone 6 plus (6+) lakini iwe na 64GB nikampa pesa sasa amekuja kuniletea IPHONE 6 PLUS lakini SIO 64GB ni 16GB sasa mimi sijawa na amani kabisa ni kama sipo sawa anasema yenye 64GB ilizidi elfu 70 kutoka kwenye hela niliyo mpa! Alishindwa kujiongeza yaani

Sasa mnao tumia IPHONE je 16GB itakuwa sawa au ndio itaanza kunisumbua sijui imejaa sijui nini? Au nibadilishe kwa mtu mwenye 64GB nimuongeze na pesa yaani sielewi nini nifanye au nibaki nayo hivyo hivyoo?

Msaada tafadhari

Cc:Chief Mkwawa
 
Kivipi mkuu
Kwanza kama matumizi yako ni kawaida unaweza kukaa masaa 48 bila kuicharge, JF na Instagram ndiyo vinamaliza charger yangu lakini niwaweza kwenda masaa 12 bila kuicharge.
 
kwa iphone storage ni kitu muhimu tena sana, tofauti ya 16gb inaweza pelekea ongezeko la bei hadi $100.

16gb ni ndogo sana matumizi ya sasa, wiki kadhaa whatsapp tu inajaza hio storage, na ukumbuke 16gb hio huitumii yote free storage ya kutumia itakuwa kama 9gb hivi.
 
Sasa chief kwa ushauri wako unashauri nini? Nipate 64GB? nibadirishane na mtu au niuze au niurudishe kule nisubiri Tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kama matumizi yako ni kawaida unaweza kukaa masaa 48 bila kuicharge, JF na Instagram ndiyo vinamaliza charger yangu lakini niwaweza kwenda masaa 12 bila kuicharge.
Hata katecno kangu tangu nikacharge usiku hadi sasa ndio nimeanza kukacharge tena.

In short nakacharge mara moja kwa siku na online nadunda kama kawaida.
 
Back
Top Bottom