Naombeni njia wadau, nimekwama

Meridah Tough

Senior Member
Nov 27, 2017
136
363
Habari za jioni?

Mpaka nafika hapa wadau mjue nimekwama. Naombeni ushauri juu ya haya mahusiano. Kiukweli nilikuwa nashangaa nikisikia kuwa mpaka watu wanafikia kufunga ndoa, wamepitia mambo mengi sana ya kukatisha tamaa na mengine ya furahaa.

Kwa ishu yangu mimi iko hivi, nina jamaa ambaye ni mpenzi wangu kwa sasa. Tulidate naye tangu miaka kadhaa iliyopita, akanitenda tukaachana.

Sasa baada ya mwezi akaniomba msamaha kuwa amebadilika. Kwa kweli nilikuwa nampenda hivyo nikamsamehe na maisha yakaendelea.

Baada ya kama wiki tatu tangu turudiane, nikaona mwenzangu ameanza kubadilika. Simu password kama zote, usiku wanapigiana simu na mwanamke ambaye waliachana lakini inavyoonekana wamerudiana.

Niliongea na mwenzangu akabisha kuwa hayo ni mawasiliano ya kawaida tu hakuna kitu. Majuzi alisahau simu yake, kwa kuwa ninamjua sikupata tabu kufahamu password yake. Kweli nimekuta chat zao humo wanaitana mke na mume and so forth.

Yan kiufupi jumbe nilizozikuta humo zinaonyesha kuwa mwanaume ndiye anampenda mwanamke kutokana na kuconfess penzi lake kwa huyo mwanamke kila mara.

Lakini at the same time, mimi hata nimwambie kiasi gani nampenda hawezi kujibu hiyo msg. Hivyo nilichukua maamuzi ya kumface na kumwambia kuwa ni heri achague huyo mwanafunzi wa chuo (21 yrs) ambaye wapo mikoa tofauti au anichague mie mzee mwenzake (28 yrs) mwanaume ana 31 yrs.

Bado hana msimamo.

Ninaombeni ushauri wadau maana kuna sauti inaniambia niondoke, nyingine inaniambia nivumilie.
 
Utang'ang'ania Mchakato Mpaka Lini, Hata Kama Ni Samaki Unachakata Itaozea Mkononi

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Awamu Ya Tano


Tuliza Mawazo Anza Upya Huyo Jamaa Hajitambui, Ukiondoka Usigeuke Nyuma

Hamna Mtoto, Hivyo Wahi Mapema, Naweka Clip Hapa Chini

 
kama sauti inayokuambia ondoka ndo inatangulia then inafuata ya vumilia basi ondoka bt kama saut ya vumilia ndo inaanza basi baki, katika mioyo yetu kuna po+ & ne- reaction ambazo hutuongoza juu ya jambo lolote, reaction inayotangulia huashiria "YES" bt inayofuatia huashiria "NO"

hii kanuni itumie katika kila jambo unaloliendea hakika hutojuta.
 
Unapoteza muda, achana naye fanya yako angekuwa anakupenda angekuwa na jibu la moja kwa moja huyo hakupendi.
 
Unataka uvumilie ujinga uko desperate kiasi gani na ndoa mpaka unataka ujitumbukize mtaroni, The guy is not a right person to you, Wake up move on
 
I said yessss! i said noooo!
i wanna stay but ma heart says goooo.

Haya ni mashairi ya wimbo flani hivi wa reggae, jina la muimbaji na jina la wimbo wenyewe sijawahi kujua
 
Habari za jioni?
Mpaka nafika hapa wadau mjue nimekwama. Naombeni ushauri juu ya haya mahusiano.
Kiukweli nilikuwa nashangaa nikisikia kuwa mpaka watu wanafikia kufunga ndoa, wamepitia mambo mengi sana ya kukatisha tamaa na mengine ya furahaa.
Kwa ishu yangu mimi iko hivi, nina jamaa ambaye ni mpenzi wangu kwa sasa. Tulidate naye tangu miaka kadhaa iliyopita, akanitenda tukaachana.
Sasa baada ya mwezi akaniomba msamaha kuwa amebadilika. Kwa kweli nilikuwa nampenda hivyo nikamsamehe na maisha yakaendelea.
Baada ya kama wiki tatu tangu turudiane, nikaona mwenzangu ameanza kubadilika. Simu password kama zote, usiku wanapigiana simu na mwanamke ambaye waliachana lakini inavyoonekana wamerudiana.
Niliongea na mwenzangu akabisha kuwa hayo ni mawasiliano ya kawaida tu hakuna kitu.
Majuzi alisahau simu yake, kwa kuwa ninamjua sikupata tabu kufahamu password yake. Kweli nimekuta chat zao humo wanaitana mke na mume and so forth.
Yan kiufupi jumbe nilizozikuta humo zinaonyesha kuwa mwanaume ndiye anampenda mwanamke kutokana na kuconfess penzi lake kwa huyo mwanamke kila mara.
Lakini at the same time, mimi hata nimwambie kiasi gani nampenda hawezi kujibu hiyo msg.
Hivyo nilichukua maamuzi ya kumface na kumwambia kuwa ni heri achague huyo mwanafunzi wa chuo (21 yrs) ambaye wapo mikoa tofauti au anichague mie mzee mwenzake (28 yrs) mwanaume ana 31 yrs.
Bado hana msimamo.
Ninaombeni ushauri wadau maana kuna sauti inaniambia niondoke, nyingine inaniambia nivumilie.
Unataka mpaka umkute kitandani wana nyanduana ndio uamini kuwa hao ninwapenzi na hawawezi kuachana?
Jipe.presha mwenyewe ala ala usije ua nafsi ya mtu yeyote!
 
Kwenye ule uzi wa kutuma hela kwa wakwe umelisema hili. Nakuunga mkono.

Tatizo hapa tujue dada anaona umru unasogea zaidi na ukute haoni mbadala wa karibu.

Mkuu, hapo hana chake. Ana machaguzi matatu tu, moja aendelee na jamaa ila akubali matokeo kwamba maisha yao yote jamaa ndivyo alivyo.

Pili aachane nae aendelee kutafuta mtu watakaeendana nae na akampenda na kumheshimu.

Kuhusu huyo jamaa kubadilika haipo. Hapo ndio nikasema haihitaji akili nyingi kwa hizo dalili kujua jamaa hampendi.
 
Japo ume chelewa ila una 2 years za kufanya mambo makubwa.kabla uja fika 30 ..achana na uyo mtu
 
Back
Top Bottom