Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
-
- #121
rafiki salama?Rafiki, tunawaachia hawa wasaidizi nyumba zetu, watoto wetu na mali nyingine chungu nzima ndani ya nyumba zetu. Wanatupikia na kufanya kazi nyingine mbali mbali ili kutusaidia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo inabidi tuwathamini na kuwaona kama ni part and parcel ya familia zetu badala ya kuwaona kama ni watu baki na hivyo kuwawekea sheria lukuki, sheria ambazo kama wangekuwa ni ndugu zetu wa damu zisingekuwepo kabisa.
Kama hutaki kubadilisha wasaidizi wako kila baada ya miezi michache basi wasome kwa makini sana akina Miss Kim, Toria na Eiyer na ufuate ushauri wao. Pia badala ya kusubiri mdada akupigie wewe jitahidi katika kila saa kutafuta dakika tano kumpigia ili kujua hali nyumbani ni shwari. Hawa watu ukiwazingua sana kwa sheria lukuki basi wanaweza kabisa kufanya lolote lile ili kukukomoa na kubaki na majuto ni mjukuu.
Good day 🙂🙂🙂
Mimi nampa sababu huwa simpi hela ya matumizi sababu hakuna matumizi ambayo atayafanya, labda kama nimesafiri.Rafiki that doesnt work....hawa wasichana wa kazi ni kukubaliana tunkwamba vitu vinginr tukubali kuliwa...mfano kwetu anatumia simu yake ila vocha hatumuwekei anatumia hela hizo hizo za matumizi ya kawaida maana huwa tumamwachia hela ya matumizi...ila ndo mpaka tumpigie sisi!
Ndo maana nikasema siwashangai wababa wanaosema hivi........Mke wangu mwenyewe ana itikadi hizohizo...hii tabia inanikera kuliko zote duniani...!
Wanasahau maisha ya wanafamilia yapo mikononi mwa beki 3,anaweza akawapoteza wote wakati wowote...
Lazima tuishi nao kibinadamu...!
Nimerelax rafikiMie huwa sijitii headache na maid hata siku moja. Kwa suala hili uliloleta hapa, nakushauri ununue mobile fone ya mezani. Nenda voda hapo wanakupa lisimu la mkonge, ukiwa nyumbani unawaka halijafutwa vumbi. Hicho kimobile ndo kwanza unampigia yuko mtaa wa tatu na anakujibu niko home, hali shwari!
but anyways, kukaa na msichana ukimfanya comfortable utafaidi wewe. Mpigie wewe, tena mruhusu akutumie msg ya tafadhali nipigie kama ana shida yoyote. Tena jumapili kaa na wanao, muache dada akabarizi kwa maboifrendi. jirani wa kakangu alikuwa mkali hapo UDSM, hgal haruhusiwi kupiga picha hata na mwanae wala wanae hawaruhusiwi kwenda kwa jirani. Siku mwanae alikuwa anaharisha, kina dada wakakaa kimya tu na sie tuko home tunaangalia tv tu. By the time mama mtoto anarudi saa moja usiku, anakamata mwanae kwenda hospitali, mtoto anafariki!
mtoto anaweza kuungua ama kuumia mbele yako na usiweze kumlinda. Relax
hii sasa kiboko........najua kinacho kupa mashaka hasa ni usalama wa nyumbani kwako hasa ukiwa na mtoto, vocha mpe ila kiboko ya njia funga cctv pasipo yeye jua pia gharama yake ni kama laki nne ivi kwa maana ya kwamba utapata full matukio kama yafuatao
1. kama mtoto ana mtrit vibaya utajua
2.kama ana tabia ya kuleta vinjemba na kugeuza nyumba yako lodge utajua haraka
3.utajua matumizi ya simu yake kwa kusikia anaongea nn
4.kama mr anamkamua beki 3 nayo itakusaidia
5.kama anatabia ya upashukuna wa kuleta marafiki kwako utamjua
faida yake hata kama una panga chumba kimoja utapata taarifa za uhakika na kuzichukulia hatua fasta, nimefanya ivo adi beki tatu anaisi mie ni mchawi.....
Usimpe hela weka tu utaratibu wa kupiga kila siku mara mbili au tatu..au weka hela simu ya nyumbani sio yake
Nunua bundle ya wiki nzima. Asipate sababu. Je anajua jinsi ya kutumia hizi bundles au...?
Karibu airtel yatosha package..but Tafuta wataalam simu ifanyiwe settings ipige namba fulani tu...namba zingine haipigi
Hapo hamna usuluhishi zaid ya kukata huduma ya kumuwekea vocha,hata mm wife alilalamika anampa vocha bt inaishia kupigia ndg zake sasa hv huduma tumekata kbs tunapiga sisi kama akitaka vocha anunue mwnyw apige atakavyo....mabeki 3 akili zao wote ni moja.
Habari rafiki.
Asante rafiki......Habari rafiki.
Ku control matumizi ya simu kwa msichana ni magumu,ukimuwekea credit ataitumia tu hata kwa simu binafsi.
Kwangu kuna simu ya mezani,naweka credit hiyo tu na kuhakikisha ina charge ya kutosha ninapotoka. Akija bint mpya cha kwanza ni kumfundisha jinsi ya kuitumia na namba za kupiga ikitokea emergency.
Akija na yake au akinunua ataihudumia mwenyewe.
Asante kwa kutaka muongozo.
Kwa mujibu wa kanuni za busara zinazoongozwa na uungwana ni kuwa;
Ma-boss wengine mna roho ya kutu!
Yaani unaona anapata saaana sio?
Kunya anye Kuku akinya Bata msala,
Jiulize boss wako wewe angekuwa ndio anapanga mikakati ya kukudhibiti kwenye vile vimianya vinavyokuingizia mapene ya ziada mbali ya mshahara ungeanza kulalama tena hapahapa.
Muache ajisikie nayeye yupo kazini bwana,
Mpe limit tu, Salio likifika kiasi fukani labda hakuna kupigia wengine ni wewe tu
Na wao wanahitaji kuwasiliana na dunia sio ukimuajiri ndio basi awasiliane na wewe boss tu.
Tunaendelea...
umeni-judge kwa vitu nisivyovifanya......
hayo maandishi meusi ambayo umeyakimbia ndo nimesema mimi huwa nafanya, hayo mengine ni maelezo tu na nimeweka clear kuwa sifanyi hayo
Kabla haujaliona hilo kama tatizo na kuja kuomba muongozo ulipaswa kwanza kujichunguza ili ugundue kikwazo ni kipi.
Pili yakupasa kuelewa kwamba mdada wakazi na yeye pia ana maisha yake anahitaji kuwa huru kufanya baadhi ya mambo yake ambayo hayatavunja misingi ya kazi yake, katika hili swala lako yapo mambo mengi sana ya kuyatazama kiundani zaidi, umedai mara kwa mara huwa unapiga simu sitaki kuuamini kwamba hizo dharura huwa zinategea na kutokea wakati ambao haupigi simu.
Tatizo liko kwenye mitazamo yenu na jinsi mnavyo wachukulia hao wadogo zetu wanapokuja kuwafanyia kazi huko majumbani kwenu, kwanza kabisa kiasi cha pesa mnachowalipa hakiendani kabisa na majuku mnayowatwisha, na pia hauwezi kugharamia mahitaji yake yote, haiitajiki kuchukua maelezo yako mengi ili mtu akusome jinsi unayoishi na binti yako wakazi, kwa maelezo hayo tu inaonesha na wewe ni mmoja kati ya watu wanaoishi na wadada wandani kwa kuwaendesha kama magari mabovu huku mkiwalipa kiasi kidogo cha pesa.
Nafikiri ungekuwa unamlipa kiasi kizuri cha pesa hata usingekuwa unatoa hiyo 1000 kwaajili ya simu, angeweza kulimudu hili kwa vile na yeye mawasiliano kwake ni muhimu kwa ndugu na jamaa zake. kama kweli kiasi cha pesa unachomlipa kinamtosheleza na hiyo 1000 unayotoa, swali la kujiuliza ni kwamba je, ni mzembe kutoa taarifa inapotokea dharura? kama jibu ni hapana, na sababu ni simu haina vocha basi tunarudi kule kule kwenye malipo unayomlipa ni kidogo.
Kweli pesa ni ngumu, na hakuna pesa ndogo, pia ukidharau mia hauwezi kupata 1000, hivyo bajeti ni muhimu swala la msingi ni je kiasi cha bajeti yako kinatosheleza mahitaji ya dada wa nyumabani?...
Swali la kizushi..
Ikitokea huyo mdada wako wa kazi akawa anakupigia simu mara kwa mara hata kama dharura haijatokea na mara nyingine awe anakurushia salio hata 1500, wakati huo wewe huwa unamuachia 1000 kwa wiki, utajifikiria nini juu ya huyo mdada? na utachukua hatua gani?
CC; kiwatengu , The Boss , Mrigariga, ICHANA , Nokia83 , dyuteromaikota , hips.com , Caroline , danzi , Munambefu , Mashaxizo , everlenk , Joseph , Bulldog , Eiyer, Mr mgeni, stroke, byb sac, gfsonwin, Honey Faith, bornagain, thinky, isha, Miss Kim, frank wa moyo, Chauro, Mbu, Escardo-bird, Natanguliza samahani kwa usumbufu kwa kuwakusanya hapa, kilichonifanya niwakusanye hapa naomba muwe watazamaji atakacho nijibu Fixed Point
Pole kwa changamoto best yangu.
Binafsi naamini sana kwenye kuzungumza na kukumbushana. Inaposhindikana kwenye kuzungumza ndio unatafuta njia nyingine mbadala.
Hawa wadada ni watu wetu wa muhimu sana, na tunawatoa kijijini (sote tunajua ukijiji ulivo na mtu pengine anakuwa hajawahi kutoka nje ya familia kwa muda) kwa hio akiongea kwa simu na nduguze/familia anafurahi kupita maelezo. yaani hata kama umekaa pembeni ukimwangalia... you feel the excitement... kwa mantiki hio sitegemei awe mtunzaji mzuri wa hela kwenye simu. au pengine ukimpa vihela ataenda tu kununulia vocha awasiliane na wa nyumbani... ila baada ya muda wanazoea. au pengine unampa hio hela anaenda kununu vitu vingine kwa maana wengi wao huwa hawapewi hata mia nje ya mshahara wao n.k n.k
Ningekushauri tu wewe mpe hio hela kwa maelezo ya kukutafuta anapokua na dharura, mfundishe pia namna ya kukutumia tafadhali nipigie n.k. Mweleze tu umuhimu wa kukujulisha dharura yeyote anayokua nayo halafu muache huru na kila akikubeep /plz call me, mpigie kwa wakati muoneshe kuapreciate. Next time mpe 2000 (mwambie 1000 atumie kwa matumizi yake ya simu na nyingine akupigie angalau mara moja moja anapokua na kitu cha kukuambia. kila anapokupigia muoneshe furaha yako ya yeye kukupigia ili kuendelea kujenga saikolojia yake kwenye kwa namna unavyojali simu yake etc.. over time she is there. Ukimuwekea sheria ya aina yeyote ndio utamwaribu maana itafika mahali hela imeisha afu kinatokea kitu anasema hela si imeisha... nakaa kimya (na ukiangalia kweli 1000 yote aliitumia kuongea na wewe)
Kingine pia waweza fanya kila akikupigia, kata umpigie wewe... inamjengea kitu kingine japo unampa hio 1000 lkn bado hutaki iishe kwako...
All the best... njia bora ya kukaa na hawa dada zetu ni kucheza na saikolojia zao.. ukiwa mkali ukaweka sheria sheria zako... wanakunasisha wewe mwenyewe bila kujua. Na anapokosea hatakiwe AGOMBEZWE.. inabidi aeleweshe aelewe na inapobidi ndo agombezwe na kuonywa....... Nafahamu mtu sehemu nakoishi (single lady) ameshafukuza wadada zaidi ya sita mwaka huu pekee... labda huyu anataka aletewe malaika.. and am sure hata malaika atamfukuza tu in few weeks.
Hawa tunawatengeneza tutakavyo. hatutegemei umtoe mtu kijijini aje afiti perfectly kwenye mazingira ya umjini kirahisi na kwa muda mfupi.. so uvumilivu, kuelekezana, kuzungumza ni muhimu sana.
Hongra kwa kuwajali. Barikiwa.