Naombeni msaada wa mawazo au ushauri kuhusu Tablet PC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni msaada wa mawazo au ushauri kuhusu Tablet PC

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Michael Amon, Jan 3, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Habari yenu members wote wa jamii forums. Ninaomba msaada wenu wa mawazo au kuhusu tablet PC. Mimi na kampuni yangu ya Young Master Supplies and General Enterprises tuna mpango wa kuleta Tablet PC's na kuziuza hapa Tanzania kwa bei nafuu kabisa kama hiyo hapo inayoonekana hapo chini.
  71jAp4Li-KL._AA1500_.jpg

  Ila tatizo sina uhakika kama zina soko hapa Tanzania. Ninaomba kama kuna mtu yoyote mwenye ufahamu zaidi kuhusu hizi Tablet PC aniambie kama zina soko hapa Tanzania au la ili nisije nikaleta zikashidwa kuuzika na matokeo yake nikapata hasara. Natanguliza shukrani za dhati kwa yeyote ambaye atajitolea kunisaidia katika hili.

  Pia unaweza kutoa maoni yako, mawazo au ushauri kupitia anwani zetu hapa chini
  Mobile: +255789 884 221
  E-mail: youngmasterent@gmail.com
   
 2. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  nipe moja niitest then ntakwambia!
   
 3. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  ungeweka specification ya hizo tablet PC unazotegemea kuzileta na price afu tuone km ni affordable!
   
 4. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Samahani dada yangu. hapa naongelea kuhusu market na sio ubora wa bidhaa. Asante
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Samahani mkuu. hapa siongelei kuhusu swala la kuuza ila ninaongelea kuhusu swala la soko. Nauliza kama zina soko hapa Tanzania au la.
   
 6. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hivi SOKO na KUUZA tofauti yake nini? Kitu chenye soko manake ni kwamba kinauzika bro. Weka specs, brand, initial pricing n.k. then tukwambie

  Kama hutaki kuuza unataka soko la nini?
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Nadhani kaka haujanielewa. Mimi bado siajaanza kuuza hizo Tablet PC ila nina mpango wa kuuza. Ila kabla sijaanza kuziuza nilikuwa nauliza wadau kama zina soko hapa Tanzania kwa maana ya kwamba kama zinauzika au la.
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180

  Young Master
  Katika moja ya vigezo vya kujua kama soko lipo ama la ni specs za hizo tablet zako
  kumbuka siku hizi dunia ni kijiji na tz tablets zipo za samsung kama aina mbili ,ZTE na ipad 1&2
  hivyo funguka waeza pata wateja humuhumu
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa mkuu kwani wewe unadhani ni Tablet PC zipi zinauzika hapa Tanzania kutokana na uzoefu wako katikati ya Tablet PC za kawaida na ipad? na Tablet Specification gani ambazo wewe unadhani zitawafaa watanzania?
   
 10. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280

  Tablets PC kama bidhaa zingine inanunuliwa kwa kuthaminisha ubora na uwezo.

  Hata vitumbua na maandazi huwa tunaangalia mpishi kuepuka kulishwa vitu visivyofaa! Otherwise jipange upya ulete uzi uliosheheni marketing strategies!

  Karibu tena!
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,607
  Trophy Points: 280
  Young Master,
  Kwa haraka haraka sana....soko liko wazi sana na brand zinazofanya vizuri sana kwa sasa ni ipad2,samsung na ZTE.

  Sasa kazi kwako kama utaleta hizo upambane na bei za sokoni,ipad2 1.5m,samsung 1m na ZTE laki 8.

  Pia angalizo makampuni yote ya simu nao wanaziuza kwa wateja wa kulipia mwisho wa mwezi....kwa hiyo soko ni pana na ushindani pia mkali!!
   
 12. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Asante sana kwa ushauri wako mkuu. Nimekuelewa.
   
Loading...