Naombeni msaada wa haraka niokoe maisha ya baba yangu Hospitali ya Muhimbili

Yani manesi wananyanyasa sana sema mtu ukishauguliwa unakua tu mpole sababu hata kama mtu wanamwona hawezi kupona bado unatakiwa umhudumie tena kwa upendo jamani Sisi kuna nesi nahisi alijua ndugu yetu haponi maana kisukari kilipanda na kupumua shida akawa anatufukuza mgonjwa akisikia joto anatuonesha ishara hata tumpepee nesi anatufukuza jaman mtu hata kama unamwona anakufa mhudumie vizuri uache hata na ndugu zake aongee nao wampepee dahh maisha haya
 
Hamna watu wanaopitia maisha magumu kipindi hiki cha Corona kama wagonjwa wa Kisukari

Mungu awasaidie, maana Madaktari wengi kwasasa wanawakimbia, kwa kuhofia kua shida yao ya kupumua,imetokana na Corona, kumbe unakuta, Sukari imepanda, mgonjwa kapatwa na komplikesheni.

Hatimaye Anaga Dunia.

Jambo lako, halitopishana na la huyu mama, kama na endapo tu, Hutochukua Hatua madhubuti

View attachment 1699572

Dah! Inauma sana. Uko sahihi kwa 100%
Hata mimi nilimpoteza mpendwa wangu mapema mwaka wa jana kwa uzembe tu wa hawa watu.

Baadhi wako shallow sana kwenye matibabu kwa wagonjwa wa kisukari na walio zidiwa ghafla. Huwa napandwa na hasira sana kila nikumbukapo lile tukio.
 
Mkuu kwa changamoto ya upumuaji mtafutie nimricaf mumpe na almit au menthol zinauzwa maduka ya dawa za asili nzuri mnooooo.pia ni bora utumie nafas yako kumsaidia baba hawata mfanya vibaya instead wataongeza umakini
Kaka hii Almit na menthol zinatumikaje katik hii changamotp
 
Mkuu maamuzi mengine ni ya kutumia once in a life time, sasa mzee yakimtokea mabaya zaidi bila wewe kutumia mamlaka si nafsi itakusuta mpaka uende kaburini?
 
Dah! Inauma sana. Uko sahihi kwa 100%
Hata mimi nilimpoteza mpendwa wangu mapema mwaka wa jana kwa uzembe tu wa hawa watu.

Baadhi wako shallow sana kwenye matibabu kwa wagonjwa wa kisukari na walio zidiwa ghafla. Huwa napandwa na hasira sana kila nikumbukapo lile tukio.
Kumbuka hata madaktari nao wako kwenye kipindi kigumu. Serikali imeshasema hakuna corona hivyo gears za kujikinga wengi hawana. Kungekuwepo na utaratibu wa kutenga hospital au majengo ya kupimia na wafanyakazi wake wakapewa vifaa kinga hali ingekuwa nafuu zaidi.
 
Dah..mwaka jana nilimpoteza mdogo wangu kwa uzembe wa manesi wa amana mpaka emergency room nilimuingiza kwa kumbeba mwenyewe manesi wananiangalia tu...dah then wananiambia nilipie fedha kwanza...Ma pesa nilikuwa nazo ila niliitaji huduma kwanza.Ndugu zangu manesi pamoja na Chang a moto mnazopitia tafadhari jaribuni kuwa na ubinadamu...
 
Pale hospital ya Hindu Mandal, posta mpya kuna Natural therapies centre, nenda pale watakupatia dawa zitakazomsaidia mgonjwa hasa kwenye upumuaji, pia unaweza ukawaomba wakakupa na ya kinga...wanauza Tzs 7,000/= hivyo vidonge vinatosha wiki 2,
20210211_173549_mfnr.jpg
20210211_173514.jpg
 
Daaah mkuu jilipue umuokoe Mzee nothing to wait , atakuja afe alaf wenye uwezo wa kukusaidia ukiwaambia ulivyosita kuwajulisha watakulaumu Kwa nini hukuwaambia na inabaki neno NINGEJUA....usiogope fanya kitu mkuu liwalo na liwe
Pole sana mkuu, Tumia nafasi yako mkuu
Huwa nasema wabongo wana roho ya kuku
Woga
Woga
Woga
Mimi huwa najilipua hata kama nasaidia mtu baki sasa mzazi si ndio watanikoma?
 
Sasa kama uko kwenye taasisi nyeti ya serikali halafu mwoga hivyo sie wakulima wa huku nanjilinji itakuwaje.

Yaani unakuja kuomba msaada JF wakati watu wanacheza na uhai wa babako mzazi na unaona taratibu zinakiukwa halafu unawaogopa hao madaktari na manesi.

Natamani nikufahami ili nikuchongee ufukuzwe kwenye hiyo taasisi maana huna msaada kwa jamii.

Kama umeshindwa kujisaidia menyewe utaweza kumsaidia mwenzako kweli?

Yiiiiiiiiiiiii, eheeeeeeee!
 
Hapana usitumie nafasi yako kwenye office ya mtu atafanya negative soon ugeukapo na mzee tunaweza mpoteza wewe jaribu kumwita huyo muhudumu mwambie akipona mzee nitakupa kiwanja changu cha mbezi atafanya kwa upendo na akipona mzee mwite huyu mwana Mama mwambie hata Mimi mtumishi wa Bibi na beans kwenda
 
Mgonjwa wa Corona ni rahisi sana kupona kabla hajafikia hiyo stage ya kuwekewa oxygen.Kwa nini umekaa kimya hadi amewekewa oxygen halafu ndiyo unataka ushauri?Ingekuwa alikuwa bado hajawekewa oxygen ningekuambia cha kufanya.

Tuambie mkuu nini cha kufanya ‍♀️
 
Back
Top Bottom