Naombeni msaada wa haraka, maumivu makali ya kichwa

jjs2017

Senior Member
May 25, 2019
162
250
Habari za wakati huu ndugu zangu..

Mke wangu (miaka 29) anasumbuliwa sana na maumivu ya kichwa, kichwa kinamuuma sana mpaka anasikia kinazunguka kwa ndani na anahisi kinakuwa kizito alienda hospitali akapimwa akaambiwa ana typhoid na ana damu ya 10.5 ila hawakuona tatizo lingine amemaliza dawa yapata mwezi sasa bado hali ipo pale nimemrudisha hospital ila hawajaona tatizo lingine.. Naombeni msaada wenu kwa anaejua tiba au tatizo ni nini hasa linalomsumbua mpaka kupelekea kusikia maumivu makali ya kichwa hadi kuhisi kinazunguka kwa ndani

Asanteni
 

Cryptographer

Senior Member
Aug 2, 2021
115
250
Hii ilimtokea mke wangu wiki kadhaa baada ya kujifungua aliambiwa anywe chai ya majani mengi kisha alale chali bila kugeukageuaka ndo akapona mazima
 

Punnisher

JF-Expert Member
Jul 28, 2014
885
1,000
Hamna kilicho ongezeka mkuu
....hiyo damu kidogo....
Ila maumivu ya kichwa yanaweza kusababishwa na msukumo mkubwa wa damu(hypertension).kipanda uso,damu kidogo mwilini,matatizo ya macho haya ndiyo mara nyingi yatasababisha maumivu makali ya kichwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom