Naombeni msaada, mwenzenu napitia kipindi kigumu sana cha Msongo wa Mawazo

Njoo tujumuike humu unaona wenzako sahv tunaingia humu
Kupiga ulabu huku ni kama ibadan

Ova
20230718_165825.jpg
 

Attachments

  • 20230718_165822.jpg
    20230718_165822.jpg
    99.2 KB · Views: 9
mimi ni mpole sana hivyo mimi kutokua mtu wa kujichanganya sana na watu (watu wangu wa karibu nakosa nguvu ya kuongea nao kwa sababu nisiwaumize).
Hiki kisingizio hakina mantiki, sasa upole na kuchangamana wapi na wapi? Unaweza kuchangamana vizuri na bado ukawa mpole
 
Habari za jioni wana jamii wenzangu.

Naombeni msaada mwenzenu napitia kipindi kigumu sana cha msongo wa mawazo, nahitaji mtu wa kukaa tukaongea tu nimechoka na sasa naogopa kukaa ndani peke yangu. Nilijitahidi nibadilishe mazingira lakini bado hali imegoma kukaa sawa.

Kusali nasali sana na biblia pia nasoma ila baada ya muda mawazo yananirudia, hali hii pia inachagizwa na hulka yangu mimi ni mpole sana hivyo mimi kutokua mtu wa kujichanganya sana na watu (watu wangu wa karibu nakosa nguvu ya kuongea nao kwa sababu nisiwaumize).

Naomba Msaada wa mawazo tafadhali, asanteni sana Mungu awabariki.
Bro, nilishapitia vipindi vigumu balaa....kumpoteza mtoto wangu, kumpoteza baba, kumpoteza mama..na wote walifuatana....ndugu wakainuka kwenye Mali... lakini muda huponya...niliamua kumuachia Mwenyezi Mungu tu, niliamua kurelax na kuanza kuishi simple sana..no complications wala nini..huwezi amini nilivuka salama..na life linasonga fresh tu
 
Kusali nasali sana na biblia pia nasoma ila baada ya muda mawazo yananirudia, hali hii pia inachagizwa na hulka yangu mimi ni mpole sana hivyo mimi kutokua mtu wa kujichanganya sana na watu (watu wangu wa karibu nakosa nguvu ya kuongea nao kwa sababu nisiwaumize).
Mapenzi noma una stress za mapenzi ? Tuanze hapo kwanza
✍️
 
Watu amabao hawana kampani au close friends mara nyingi ni wabinafsi,wajivuni,wasiotaka kusikiliza wengine yaani hawana empathy ,wajuaji na nk
Kwa kujifanya at ni introvert
Kujulikana sana pia sio issue sometimes Bora uishi maisha ya low profile underground chini chini wakikujua sana hawachelewi kukudharau
✍️
 
Watu amabao hawana kampani au close friends mara nyingi ni wabinafsi,wajivuni,wasiotaka kusikiliza wengine yaani hawana empathy ,wajuaji na nk
Kwa kujifanya at ni introvert


Watu wanaokufamu ndio wanajua namna ya kudeal na wewe sisi stranger labda tukufanyie motivation tu.

Amani iwe nawe
Mkuu kama huna uelewa wa jambo kimya ni busara zaidi. Tumeumbwa tofauti, ukiweza kushauri sawa huwezi mute. Situation anayopitia mkuu inahitaji faraja na si kubeza
 
Cha kwanza nakushauri usishinde sana ndani..jitahidi asubuhi na jioni ufanye mazoezi ya kukimbia au kutembea...utaimarisha afya ya akili na mwili pia..
ELEWA pia unayopotia kama ni kuanguka kwenye biashara imetukuta wengi sana ..yaani unafail kila kitu mbele huoni na nyuma huoni..ELEWA HILI SUALA NI LA MUDA TU sio la milele..utadharaulika, utaona aibu kuishi maisha mapya tofauti na Jamii ilivokuwa inakuona, watu watakukimbia etc hayo mambo ndio yatokea sana....
Ushauri jiangalie wewe binafsi ANZA MOJA KUBALI UMEANGUKA....toka ndani ingia chaka lolote usione aibu fanya lolote la kuanzia kupata kipato chochote..ikiwezekana toka hata huo mji nenda mwingine .....kubwa zaidi kuwa karibu n Mungu wako maana Mungu atakuinulia watu watakusaidia...
 
Mkuu kama huna uelewa wa jambo kimya ni busara zaidi. Tumeumbwa tofauti, ukiweza kushauri sawa huwezi mute. Situation anayopitia mkuu inahitaji faraja na si kubeza
Usimsemee muache aseme mwenyewe ndo maana Ni mesema mara nyingi sio mara zote
Elewa kwanza

Yeye ndo anajua sio wewe anyway umeshatuma iyo million 5 maana tatizo hapo ni pesa
 
Mkuu pole sana,nenda shalom kanisani kaloleni, omba kukutana na mtumishi wa Mungu Akyo atakusaidia sana na hiyo hali itaisha.
 
Dhulima na mambo ya kifamilia
Pole sana, jipe.moyo wa kusonga mbele, hizo dhulma ulizofanyiwa zisikufanye urudi nyuma, bali zikufanye usonge mbrle kwa nguvu ili ujikwamue

Kuhusu familia, kila familia ina changamoto, ishi maisha yako maana hapa duniani huwezi mridhisha kiumb3 yeyote, jipende kwanza wewe abd be a priority before making others priority, kula vizuri, jichanganye na watu, tembelea maeneo mazuri kama hali inaruhusu na upate muda mzuri wa kulala
 
Mkuu nenda ata stendi pale tembea tembea , Hali ya msongo WA mawazo ikipungua ndo ufikirie nini cha kufanya ,

Usichukue Maamuzi yoyote ukiwa na mawazo ,
Take it easy Mkuu changamoto za maisha ni kawaida kikubwa Uhai
 
Back
Top Bottom