mchajikobe
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 2,661
- 1,267
Jamani mwenzenu nina jiko nimenunua la kuchomea nyama, lakini kila nikichoma mishkaki haina ladha na ni migumu,wenye utaalam juu ya hili nisaidieni please.
Andaa nyama yako kwa kukatakata vipande size ya kawaida.Hifadhi kwenye bakuli ama sufuria.Andaa viungo Kama tangawizi,kitunguu swaum na limao /ndimu /vinegar changanya kwenye nyama uliyoandaa kisha ifunike kwa dk45 hadi saa nzima.Jamani mwenzenu nina jiko nimenunua la kuchomea nyama,lkn kila nikichoma mishkaki haina ladha na ni migumu,wenye utaalam juu ya hili nisaidieni plz
Asante kwa darasaAndaa nyama yako kwa kukatakata vipande size ya kawaida.Hifadhi kwenye bakuli ama sufuria.Andaa viungo Kama tangawizi,kitunguu swaum na limao /ndimu /vinegar changanya kwenye nyama uliyoandaa kisha ifunike kwa dk45 hadi saa nzima.Kabla ya kuchoma unaweza pia ongeza viungo Kama soy sauce ama berbercue sauce na chumvi kiasi.Natumaini utakua umeandaa jiko. Choma mishkaki yako kwa moto wa kiasi ili iive vizuri. Serve kwa chachandu na salad na chakula upendacho Kama chips,ndizi Choma ama ugali.Enjoy
Nadhani hakuuliza kuwa Nyama gani inafaa kwa mishikaki?inategemeana na aina ya nyama unayotumia.si kila nyama inafaa kuchoma mishkaki.ongea na alwatan wa bucha akuelekeze nyama ipi inafaa
Anko mbona unataka kuanza ligi asubuhi namna hii.Amesema nyama haina ladha na inakuwa ngumu.logicaly inamaana kuna kitu anakosea.eidha kwenye kuandaa,kwenye kuchoma,ama aina ya nyama anayotumia.mimi sio mjuaji nimetoa tu angalizo hapoNadhani hakuuliza kuwa Nyama gani inafaa kwa mishikaki?
Nilidhani ungeanza kumuelekeza kuwa nini afanye ili mishikaki yake iwe raini na yenye radha,, then mwishoni ndo umpe angalizo lako, coz Nyama inayofaa kwa Mishikaki haiwezi Tu kuwa raini na yenye radha bila kuweka viungo kama Mdau alivyosema hapo juu post # 3.Anko mbona unataka kuanza ligi asubuhi namna hii.Amesema nyama haina ladha na inakuwa ngumu.logicaly inamaana kuna kitu anakosea.eidha kwenye kuandaa,kwenye kuchoma,ama aina ya nyama anayotumia.mimi sio mjuaji nimetoa tu angalizo hapo
Ukiweka viungo kiasi cha kutosha na kuiacha ikae kwenye viungo (marinated) inapata ladha na kuwa laini... viungo vya kutengeneza ladha tamu ya mishikaki ni vinegar au limao au ndimu, kitunguu saumu, kitunguu maji unakata vicube vidogo vidogo, chumvi kiasi, tangawizi, pili pili manga ya unga, mafuta ya maji (ya alizeti, au olive,) huu mchanganyiko ndo unachanganya na nyama kisha unaifunika viungo vifanye kazi yake kwa saa moja hivi. Wengine huweka na papai bichibichi lilipondwa ili kulainisha nyama mana yanakuwa na enzyme fulani ya kulainisha protein/nyama.Jamani mwenzenu nina jiko nimenunua la kuchomea nyama,lkn kila nikichoma mishkaki haina ladha na ni migumu,wenye utaalam juu ya hili nisaidieni plz