Naombeni maelezo kuhusu ving'amuzi.

maege

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
309
73
Habari wakuu!
Nataka kununua king'amuzi kwa ambaye anavitumia naomba anieleze yafuatayo
1) bei ya king'amuzi
2) malipo kwa mwezi
3) idadi ya chanel nitakazoziona
ni Star times, TING, Zuku na vingine kama vipo. Asanteni.
 
star times wanauza king'amuzi chao 39,000/=(ni offer hadi october) kwa mwezi unalipia 9,000 au 18,000 au 36,000....
 
asante ngoja nisubirie maelezo ya vya aina nyingine nifanye maamuzi.
 
star times wanauza king'amuzi chao 39,000/=(ni offer hadi october) kwa mwezi unalipia 9,000 au 18,000 au 36,000....

Viwango hivyo vyote unalipia kwa mwezi? Kama ni hivyo kwa nini vitofautiane?
 
ila mi ninaswali moja la nyongeza je kunaving'amuzi vya startimes vinavyo kubali umeme wa D.C?
 
Mkuu unajaribu kuuliza nini hapa sijakupa uzuri

Ving'amuzi hivi ukisha nunua wewe unakwenda moja kwa moja kwa nyumba yako unachomeka kwa soketi kitu mwake
 
Habari wakuu!
Nataka kununua king'amuzi kwa ambaye anavitumia naomba anieleze yafuatayo
1) bei ya king'amuzi
2) malipo kwa mwezi
3) idadi ya chanel nitakazoziona
ni Star times, TING, Zuku na vingine kama vipo. Asanteni.

Mkuu karibu kwenye ulimwengu wa maudhi, yaani kama upo njema nakushauri uchukue DSTV

Lakini kama umeamua kuja huku hakuna mwenye nafuu wote michosho tu
Startimes wanaongoza kwa uduanzi kifurushi cha sh elf9 hata usithubutu upuuzi mtu, angalau kiduchu cha 18000 na hicho kingine walau utaambulia movie tu basi, kuhusu michezo ni kichefu chefu no live events

Zuku siwajui vizuri

Easytv nao angalau utaona chaneli karibu zote za bongo lakini za nje ni makapi tu hamnakitu

Ting labda uwe mtu wa dini vinginevyo wale wale tu
 
Mimi natumia startime tangu world cup lakini nina mwaka mmoja nimepaki ndani maana ni upuuzi mtupu kwasasa bora hata dstv.
 
je ikifika mwisho wa mwaka tukiingia kwenye program za digitali vinga'muzi vitakuwaje ?vitaendelea kufanya kazi vizuri?nielewesheni tafadhali
 
Nilianza kutumia GTV kabla hawajafilisiwa walikuwa safi sana chaneli za kutosha huduma bora nikahamia DSTV duh huk poa kwenye sports chanel mpaka movie tatizo hawana channel nyingi za Tanzania pili bei zao ni kwa dola 79*1600= kwa mwezi afu ghari. Kwa sasa nimeweka kando natumia EasyTv wako poa sana chanel nyingi za Tanzania na nje pia bei zao kila mmoja anaweza mudu ni Tsh 9000 kwa mwezi. Nimeona kwa startimes scratching sana afu hakuna channel nyingi za tz bei zao ndo Kama alivyotaja hapo juu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu kama una hela yako ya kutosha DSTV haina mpinzani na picha ziko clear kweli kweli, yaani mtu unaona kwamba Waingereza ni moto wa kuotea mbali katika masuala ya kitekonolojia ya usambazaji wa mawimbi ya TV. We sema tatizo linatokea wakati mvua ikinyesha nyingi mawasiliano yanakatika kwa kuwa mawimbi ya Ku-Band yanazuhiwa na maji kirahisi.

Narudia KUSEMA TENA kwamba, ukiwa na hela yako utasikitika kununua kingamzi na dish la DSTV.
 
9000 mwezi mmoja

18000 miezi miwili

36000 miezi mitatu

Hapana hapa mdada umeingia chaka. Kuna vfurus tofaut na vna majna tofaut. Ukilipia cha 18000 kuna more chanels na 9000 unapata few chanels. Fatilia kwa umakini....
 
Mkuu unajaribu kuuliza nini hapa sijakupa uzuri

Ving'amuzi hivi ukisha nunua wewe unakwenda moja kwa moja kwa nyumba yako unachomeka kwa soketi kitu mwake

yah... Swali ni hili ... Kunaaina mbili za umeme. D.C na A.C . Huu wa majumbani ni A.C but mi vitu kama T.V natumia umeme wa solar D.C so vp ina socket ya D.C?
 
Nilianza kutumia GTV kabla hawajafilisiwa walikuwa safi sana chaneli za kutosha huduma bora nikahamia DSTV duh huk poa kwenye sports chanel mpaka movie tatizo hawana channel nyingi za Tanzania pili bei zao ni kwa dola 79*1600= kwa mwezi afu ghari. Kwa sasa nimeweka kando natumia EasyTv wako poa sana chanel nyingi za Tanzania na nje pia bei zao kila mmoja anaweza mudu ni Tsh 9000 kwa mwezi. Nimeona kwa startimes scratching sana afu hakuna channel nyingi za tz bei zao ndo Kama alivyotaja hapo juu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

kuna package mbali mbali za DSTV kuanzia...elfu 16....30 na kitu....40 na kitu.....80....na premium ni laki na 28 elfu.....
bora kama umeamua kupata burudani ni heri ukachukua DSTV....so much more......
 
kwanza lazima utuambie unakopatikana namaanisha unakoishi ndipo 2tapata urahisi wa kukushauri vizuri.
 
Nilianza kutumia GTV kabla hawajafilisiwa walikuwa safi sana chaneli za kutosha huduma bora nikahamia DSTV duh huk poa kwenye sports chanel mpaka movie tatizo hawana channel nyingi za Tanzania pili bei zao ni kwa dola 79*1600= kwa mwezi afu ghari. Kwa sasa nimeweka kando natumia EasyTv wako poa sana chanel nyingi za Tanzania na nje pia bei zao kila mmoja anaweza mudu ni Tsh 9000 kwa mwezi. Nimeona kwa startimes scratching sana afu hakuna channel nyingi za tz bei zao ndo Kama alivyotaja hapo juu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Easy tv wanapatikana huku mikoani?mf Mwanza. Kwa wapenzi wa HBO na documentary za discovery channel(sipendi mpira!) ninunue king'amuzi gani?
 
Back
Top Bottom