Naombeni jina la mtoto wa kike

Nenda iringa pale ruaha mbuyuni na vijiji vya karibu vina majina kama hayo
Shida, Masumbuko, Tatizo, Subira na ajabu yake sasa kuna baadhi yao ndio matajiri wa hapo vijijini.

Jina ni utambulisho tu hauna uhusiajo wowote na mafanikio.
Na vile vijumba vyao choka mbaya ndio unawaita matajiri Kuna nyumba Gani nzuri pale kijijini? Shida tupu pale na madebe Yao ya kuuza vitunguu barabarani hayo majina yanawakilisha shida na masumbuko waliyonayo
 
(1) Nuru = lightness, brightness, shine, Illuminata , Enlightener ,nk.

(2) furaha= happiness, Joyce, Gladness Etc

Rodda, veneranda, Antonia, Agustina, severina, Emanuela, Paulina, Patrisia, Poinsiana, Filipina, Teobista, Febronia, Wilhelmina, marselina, Donatila, Fransiska, Anjelina, Stefania, Atanasia.
ANJELINA ngoja nikatafute maana
 
Masikitiko,,majuto,,shida,,ngumukutoboa,,njaa,, mascania,,katapila,majeneza,hayo ndo majina konki cocasitic hayo yaani ni ya kibabe we ni hiphop inatakiwa watoto wako wawe na majina ya kihip hop
 
Siku hizi bila majina ya kizungu waafrika hatuwezi kuridhika kabisa. Mtoto akipewa jina la kizungu lenye double alphabet na jina liwe y au h mwishoni baasi unaonekana mjanja sana! Mental Slavery is real! Mara Giannah mara Abriannah...tumezaliwa afrika tunaongea kiswahili ila akili zetu zipo Ulaya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom