Naomba Uzoefu wenu, Umekutana na rafiki yako wa kiume wa zamani, Moyo unapasuka paaaaah

Mpe uchi kwanza ili uangalie viwangovyake,usije ukashangaa kumbe jamaa mkamerun,si unajua mambo ya kusoma nje!!
 
Lol....nimekupiga dongo
hujakata tamaa tu! ...he he he...

Well, kwakuwa wataka kusikia kusikia +ves pekee...
fuata moyo wako! 2012 dunia ni yako, maamuzi ni yako:eyebrows:

Mmmh Mbu hatimaye Moyo umegeuka kuwa kuni Mbichi. Unatoa moshi tu. Hata hauwaki :)
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
images
 
  • Thanks
Reactions: LD
Hebu ni-PM nikufundishe jinsi ya kumbana kwenye angle aje ku-propose na kitu cha tanzanite hapa! yaani unamjua toka mtoto afu unamuogopa?
Afu huo moyo wako tunaufunga kwanza na kamba ya ng'ombe ya katani ile, manake unatakiwa ufunguke kwa stepu kama banana, sawa dada?
 
  • Thanks
Reactions: LD
Mpe uchi kwanza ili uangalie viwangovyake,usije ukashangaa kumbe jamaa mkamerun,si unajua mambo ya kusoma nje!!

Come again.. waliosoma nje? on the other hand i second you kujua viwango vyake lol. .
 
  • Thanks
Reactions: LD
Hata ukifunguka nahisi uhusiano utakuwa wa muda mfupi tu!
 
  • Thanks
Reactions: LD
Sasa ndio tumeonana tena.
Hapa vipi LD, vidole viliteleza au ndio mmeshaonana kweli?
Ninachopenda kukusahuri kama mwanamume, ni hivi - endelea pale ulipoacha, enzi za barua za marashi na kopa lililochomwa mkuki; lakini usipige hatua hata moja mbele baada ya hapo. Umeeleza wasiwasi wako ni kuwa usije kulizwa, kwa hivyo kama unaliogopa hilo, zuwia kamba. Hata kama yeye atafunguka kwako, "wewe usifunguke"kirahisi. Give time to time, if he destined to be yours, he'll be.

Moyo umenipasuka paaaaaaaah! nilipoona umerudi. Karibu tena Eliza [wa Tegeta]

umalaya by nature
Marytina, ndio nini tena hii, Dear?

Mpe uchi kwanza
Songoro, hii lugha sio pahali pake hapa. Heshima kitu cha bure.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Habari za siku nyiki wapendwa kaka na dada, nimejitokeza kwenu, kuomba ushauri na uzoefu wenu katika hali kama hii nayoisikia sasa. Sio lazima nikisema mimi iwe ndio mimi kabisa eeh. Yawezekana namwakilisha mtu ila najiita mimi. Manake wapwa hamchelewi kuunganisha dots hapa.

Mwenzenu kulikuwa na kaka mmoja, alikuaga rafiki yangu wa barua enzi zile primary na sekondari. Si haba tuliwasiliana hadi form six, wakati yeye akiwa anasoma shule tofauti kabisa na mimi. Baada ya kumaliza Form six akaenda kusoma chuo Nje ya nchi. Huko Ughaibuni.

Sasa mie si nikabaki bongo, nikajua ndio nitolee tena, sasa we majuu na mie bongo wapi na wapi. Mmmmh nikamsahau kabisa, nadhani na yeye akanishau kabisa. Nikachukulia kama ilikuwa ni utoto tu wakati huo. Uzuri au ubaya urafiki wetu haukufika mbali sana. Uliishia kwenye karatasi, kuandika kwa kalamu ya kunukia na kupulizia marashi :)

Sasa maisha yakaendelea hivyo, nikawa nimeingia kwenye mtandao mmoja wa kijamii, nikamuona, lakini kwa kuwa nilijua yuko majuu, mie nikaogopa hata kumwandikia. Mmmh mi nikawa nipo na jina lingine, sio jina langu halisi lililozoeleka, kwa hivyo isingekuwa rahisi kunitambua.

Mmmh siku moja nikakutana na marafiki wengine ambao tulikuwa tunasoma pamoja na huyo kaka, tukapiga stori za hapa na pale, tukikumbukia enzi za maisha ya sekondari. Mmh si tukajikuta tunamuongelea na huyu kaka. Basi yale maongezi yakapelea mimi kuamua kumwandikia yule rafiki na kujimbulisha kwake.

Uuuuh, ikawa kama sikukuu, hakuamini, loooh, kumbe alisharudi bongo na anafanya kazi hapa. He! tukapeana namba za simu. Duh roho si ikaanza kunipasuka! Duh tunachat tunapiga stori za zamani na sasa, looh moyo unanipasuka. Nikitoka ofisini nikifika nyumbani, naanza kuandika tena sms tunachat...loooh nikaanza kujistukia.

Mbona moyo unanipasuka hivi? Yani huyu kaka ndio ananipasua moyo kiasi hiki, situlii, nataka kumsikia tu, hata akiandika sms. Duh asubuhi natamani ifike niingie online nimuone.

Jamani hii hali imewahi kukuta? Na je ukiwa kama binti au kaka ulifanya je? Manake sasa najiona nitaanza kumshobokea halafu niumie. Mmmmh nikifungukaa mazima kwake itakuwa je? Duh ataniona je kwanza?

Anasomeka yuko single na mimi niko single kwa maana kwamba hata kama ana mtu sio ndio kashafanya maamuzi :).........dah dah Moyo una kihere here huu. NA SIJUI yeye kama moyo wake una kihere here na mimi kiasi hiki nilicho nacho mimi. Au niendelee tu kukomaa kuwa mgumuuuuuuuuu afu anabadilika anakuwa kaka, au ananipotea tena kabisa.

Manake kwa jinsi moyo unavyonipasuka ni kwamba naweza funguka wajameni, halafu nikifunguka baadaye kitatokea nini? Si nitakuja kulia mie?

Hebu mshaurini dada yenu.

hapo kwenye red ndo patakapo kuponza.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Hapa vipi LD, vidole viliteleza au ndio mmeshaonana kweli?
.

Ni kweli tumeshaonana MAMMAMIA....yani sasa kwa kumuona si ndio moyo ukaanza kupasuka?

Ha ha ha huo wako usipasuke bwana...mie nipo sema nimekuwa msomaji zaidi siku hizi.
 
maana yake mkafungue ule ukurasa ambao hamkuufungua........

Ila ukiingia kichwa kichwa ita -eat kwako......
 
  • Thanks
Reactions: LD
Tii kiu yako. Haya maisha mafupi sana!
Akisepa baadae hatakua wa kwanza nafikiri.
BTW hapa katikati hakuna mengine yaliyoendelea na yanayoendelea upande wako, kuna vitu umeruka ktk maelezo yako.
 
  • Thanks
Reactions: LD
HP, Umelonga

Ukienda mbio unaweza JERUHIWA UKAJUTA

Jipe Muda , Muulize na MUNGU wako ili kukiwa na Kibali juu ya hili ufarijike
 
  • Thanks
Reactions: LD
Back
Top Bottom