Naomba Uzoefu wenu, Umekutana na rafiki yako wa kiume wa zamani, Moyo unapasuka paaaaah | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Uzoefu wenu, Umekutana na rafiki yako wa kiume wa zamani, Moyo unapasuka paaaaah

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by LD, Mar 6, 2012.

 1. LD

  LD JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Habari za siku nyiki wapendwa kaka na dada, nimejitokeza kwenu, kuomba ushauri na uzoefu wenu katika hali kama hii nayoisikia sasa. Sio lazima nikisema mimi iwe ndio mimi kabisa eeh. Yawezekana namwakilisha mtu ila najiita mimi. Manake wapwa hamchelewi kuunganisha dots hapa.

  Mwenzenu kulikuwa na kaka mmoja, alikuaga rafiki yangu wa barua enzi zile primary na sekondari. Si haba tuliwasiliana hadi form six, wakati yeye akiwa anasoma shule tofauti kabisa na mimi. Baada ya kumaliza Form six akaenda kusoma chuo Nje ya nchi. Huko Ughaibuni.

  Sasa mie si nikabaki bongo, nikajua ndio nitolee tena, sasa we majuu na mie bongo wapi na wapi. Mmmmh nikamsahau kabisa, nadhani na yeye akanishau kabisa. Nikachukulia kama ilikuwa ni utoto tu wakati huo. Uzuri au ubaya urafiki wetu haukufika mbali sana. Uliishia kwenye karatasi, kuandika kwa kalamu ya kunukia na kupulizia marashi :)

  Sasa maisha yakaendelea hivyo, nikawa nimeingia kwenye mtandao mmoja wa kijamii, nikamuona, lakini kwa kuwa nilijua yuko majuu, mie nikaogopa hata kumwandikia. Mmmh mi nikawa nipo na jina lingine, sio jina langu halisi lililozoeleka, kwa hivyo isingekuwa rahisi kunitambua.

  Mmmh siku moja nikakutana na marafiki wengine ambao tulikuwa tunasoma pamoja na huyo kaka, tukapiga stori za hapa na pale, tukikumbukia enzi za maisha ya sekondari. Mmh si tukajikuta tunamuongelea na huyu kaka. Basi yale maongezi yakapelea mimi kuamua kumwandikia yule rafiki na kujimbulisha kwake.

  Uuuuh, ikawa kama sikukuu, hakuamini, loooh, kumbe alisharudi bongo na anafanya kazi hapa. He! tukapeana namba za simu. Duh roho si ikaanza kunipasuka! Duh tunachat tunapiga stori za zamani na sasa, looh moyo unanipasuka. Nikitoka ofisini nikifika nyumbani, naanza kuandika tena sms tunachat...loooh nikaanza kujistukia.

  Mbona moyo unanipasuka hivi? Yani huyu kaka ndio ananipasua moyo kiasi hiki, situlii, nataka kumsikia tu, hata akiandika sms. Duh asubuhi natamani ifike niingie online nimuone.

  Jamani hii hali imewahi kukuta? Na je ukiwa kama binti au kaka ulifanya je? Manake sasa najiona nitaanza kumshobokea halafu niumie. Mmmmh nikifungukaa mazima kwake itakuwa je? Duh ataniona je kwanza?

  Anasomeka yuko single na mimi niko single kwa maana kwamba hata kama ana mtu sio ndio kashafanya maamuzi :).........dah dah Moyo una kihere here huu. NA SIJUI yeye kama moyo wake una kihere here na mimi kiasi hiki nilicho nacho mimi. Au niendelee tu kukomaa kuwa mgumuuuuuuuuu afu anabadilika anakuwa kaka, au ananipotea tena kabisa.

  Manake kwa jinsi moyo unavyonipasuka ni kwamba naweza funguka wajameni, halafu nikifunguka baadaye kitatokea nini? Si nitakuja kulia mie?

  Hebu mshaurini dada yenu.
   
 2. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Haba na haba huleta mahaba
  OTIS
   
 3. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 180
  Uandishi wako unaelezea uko kwenye kundi la watu wa umri gani hasa.any way vuta puuuumzi,subira huvuta heri,kama we ndo wake wa maisha Mungu atalifanikisha hilo,na hakuna awezaye kuzuia,Fanya maombi pia ili uongozwe na Roho zaidi kuliko hisia za mwili.
   
 4. LD

  LD JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Duh asa hapa niliewe nini mkuu OTIS
   
 5. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 180
  chelea mwana .........
  Mtaka cha uvunguni......
   
 6. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 180
  uelewe pia haba na haba huleta ukahaba.
   
 7. LD

  LD JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nashukuru kwa maombi, sasa umri ndio unachangia hayo hapo mkuu. Mmmh wa maisha hapo sidhani sana.
   
 8. LD

  LD JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo ni ukahaba?
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,183
  Trophy Points: 280
  Hatimaye LD adondokea mapenzini!

  Usisahau kuniletea kadi ya mchango.
   
 10. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Mmmmh yani wewe una vituko!. Mmmh mimi naona usiendelee kujiumiza moyo funguka kwake tu. Mmmh jamaa anasound vipi wakati mkichat? unaona kafika?. Mmmh mimi naona mualike dinner sehemu fulani nzuri Mpige story za zamani. Mmmmh wakati wa kuonana naye hakikisha unatokelezea kimahaba. Mmmh kama unataka roho isikupasuke siku mkionana hakikisha unambusu kabla hata ya salamu. Mmmh umenifurahisha sana dada yangu.
   
 11. LD

  LD JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Babu huo ushauri kweli huo? Hebu funguka mwenzio nina pasuka moyo.
   
 12. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Yule babu wa ofisini vipi? Ashakuachia?
   
 13. LD

  LD JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dah, tatizo wakaka hamsomeki bwana.....naona yupo vizuri tu. anachat anaanzisha mawasiliano. Yani anaonekana yupo ila mie ndio najistukia tu. Duh natumia akili sana.....kujiuliza kwa nini Moyo unanipasuka?
   
 14. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sema na moyo wako, duniani tunaishi maramoja tu yanini kujipa tabu, mfungukie wewe acha kulemba shauri yako...
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,183
  Trophy Points: 280
  Yaani kwa jinsi ulivyoandika.........

  Yaani mi nakushauri tu mfungukie kama ulivyofunguka hapa......

  Yanini kujitesa bana. Na akikukuta huna bikira mtajiewambie kabisa aliyekubikiri ili akuone ulivyo mwadilifu.

  Waishwa mshiki?
   
 16. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Usifunguke aisee atakuona wangu wangu sana, jikaze mpe muda kama ana nia ya zaidi, ataanza mwenyewe. Sisi wanaume ukijileta huwa hatuna adabu hata kidogo, huwa tunakula hata kama tuna commitment zingine na kusepa. So ni vzr ukaucontrol moyo wako, usije ukajidhalilisha kwa kukosa subra.
   
 17. LD

  LD JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yule nilishamshinda bwana...Baba askofu...Moyo unanipasuka mwenzio.
   
 18. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Duuh umenichosha kusoma wewe, maana hizo Mmmmh... Mmmmh makubwa...
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,183
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha...khaa!

  Askofu hebu mfanyie maombi huyu binti, asije akapondwa moyo wake. Kwa jinsi alivyoandika naona haamini kuwa tangu waachane jamaa atakuwa kashaweka foleni ya kutosha ya vimwaga mkojo vya jinsia pinzani. Huu mshawasha ni wa kutaka kuonja alichokikosa utotoni. Akishakipata huyooooo anarudi kwenye foleni zake kujilia vyake.

  Ushauri: Mfungukie kama ulivyotufungukia.....
   
 20. LD

  LD JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Duh na hicho hapo ndio kinanifanya nashindwa kulala.....khaaaa moyo unapasuka, kufunguka nashindwa. Kisa hayo maswali hapo. Duh
   
Loading...