Naomba utaalam wa kupika chai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba utaalam wa kupika chai

Discussion in 'JF Chef' started by figganigga, Oct 24, 2012.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  Naomba nifundishwe kupika chai. nahita nijuie kupika kila aina ya chai. iwe ya rangi au maziwa. vilevile nahitaji kujua viungo vinavyo hitajika. ni hayo tu. mia
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  chai haipikwi ina chemshwa kama unataka kuchemsha chai ya rangi:-

  Maji 1/2 lita
  Sukari saizi unayotaka
  Michaichai kiasi unachohitaji wewe
  Tangawizi iliyokwanguliwa vijiko vya chakula 3
  Iriki vijiko vya kula 2

  Jinsi ya kuandaa

  Chemsha maji kisha tia vitu vyote isipokuwa sukari kwani kila mtu anatumia anavyojisikia mtumiaji. Chemsha kwa dk 15 tayari kwa kunywa..

  Cheers :coffee:
   
 3. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Chai ya rangi: Chemsha maji kwa kiasi utakacho. Wkt maji yanachemka, tia viungo [(h)iliki, mdalasini, tangawizi -- angalia maelezo hapa chini]. Acha viungo vichanganyike na maji yachemkayo kwa km dkk 10-15. Sasa unaweza kuweka sukari ukipenda. Tia majani ya chai kidogo na acha yachanganyike na maji yachemkayo kwa km dkk 10 -- usiwache majani yachemkie kwa muda mrefu; chai inaweza kuwa chungu. Chai yako iko tayari kunywewa.

  Chai ya maziwa: Ni vema kuanza kwa maji kiasi kidogo, km ktk chai ya rangi. Tia maziwa baada ya viungo kuchemkia ktk maji. Hatua nyingine ni km ktk chai ya rangi hapo juu.

  Maelezo Khs Viungo:

  (h)iliki - Menya maganda. Weka mbegu ktk kipande cha karatasi/kitambaa safi kisha zitwange.

  tangawizi - Mbichi ni bora kuliko ya unga. Isafishe tangawizi, menya maganda kwa wembamba au para kwa kisu. Isage tangawizi ktk kiparuzio (grater). Kiasi cha tangawizi unachoweka ktk maji yachemkayo kinategemea kiasi cha ukali unachokihitaji -- kiasi kikubwa, ukali zaidi. Kumbuka pia, muda mrefu wa kuchemkia tangawizi huchangia kuongeza ukali.

  mdalasini - Ni vema kuutwanga kuliko kuuweka mzima mzima. Mdalasini mzima ni bora kuliko wa uliokwishatwangwa -- Ni vema uutwange wewe mwenyewe.

  Nasubiri feedback.
   
 4. k

  kisilo Senior Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe chai naho inautalam wacha nijaribu kumpikia my wife kesho.
  jf ni kilakitu nizaidi ya darasa.mia
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  But angalia asije akazoea tu ila kumsaidia ni poa sana na sisi wanaume tukipika tu ujue utasifiwa miaka mia..
   
 6. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,161
  Likes Received: 10,507
  Trophy Points: 280
  Chemsha maji yapate moto kisha weka kwenye kikombe halafu chukua majani ya pakti tia ndani ya kikombe chako chenye maji moto, ongeza sukari saizi yako kisha koroga..
  Kwisha.....
   
 7. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umenichekesha kwa hiyo "Kwisha". Hii ni chai ya maofisini.
   
 8. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mimi nanywa uji na maji chai nyama ya hamu.
   
 9. Zurie

  Zurie JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2016
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 962
  Likes Received: 1,621
  Trophy Points: 180
  Nilidhani chips tu...kumbe hata chai:eek::eek:
   
 10. Freelancer Wakala

  Freelancer Wakala JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2016
  Joined: Feb 6, 2016
  Messages: 1,061
  Likes Received: 679
  Trophy Points: 280
  Nikioa mwaka wake huo Wife atazidi ku-love you.
   
 11. Evelyn Salt

  Evelyn Salt JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2016
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 45,126
  Likes Received: 32,004
  Trophy Points: 280
  Usiweke viungo kwenye chai wakati ipo jikoni harufu inapungua, fanya hivi.....
  Twanga viungo vyako, inaweza kuwa iliki na mdalasini, vitwange vizuri kisha viweke kwenye chupa ya chai, chai ikichemka weka kwenye chupa funika.... Aseee inanukia hatareee
   
Loading...