Naomba Ushauri

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
213
Hi

Habari zako

Nafikiri wewe ni mzima au sio

Mimi pia ni mzima sana hapa nilipo maisha yangu ni kawaida tu ila kwa sasa hivi naiona dunia sasa hivi kama chungu hivi , nilizoea kuwa na furaha na kujinafasi lakini ghafla naona mambo yanakuwa mchanganyiko

MAMBO YENYEWE

Tumekuwa tukigombana na mambo kama hayo ambayo ni ya kawaida lakini haswa zaidi ni kuhusu yeye mwenyewe kuwa msiri katika mambo yake na vitu vyake vingine ambavyo mimi kama mpenzi wake nilitakiwa kujua lakini hakupenda kuniambia wala nini ingawa nilikuwa namsaidia na kujaribu kuwa nae karibu zaidi .

Sasa hivi amegraduate ameniambia tuachane sababu kubwa ni kwamba yeye ni muisilamu na wazazi wake hawapendi mtoto wao awe na mpenzi ambaye sio muisilamu wakati mimi nachojua yeye ni mkristo na wadogo zake wote ni wakristo hata kwa majina na kadhalika .

Balaa zaidi jana usiku niliambiwa kwamba yeye ana mtoto ambaye yuko mkoani mbeya mwaka kesho ndio anaanza masomo hapo ndio nilichanganyikiwa kabisa kwa sababu hakuwahi kuniambia kuhusu kisa hichi

Ndio nikakumbuka kumbe pesa alizokuwa anatak kwangu kupeleka kwa bibi yake kumbe ni kwa ajili ya mtoto wake ambaye mimi simjui na sijawahi kupewa taarifa , kumbe anavyoniambia niwe mbali na ndugu zake ni kwa kuogopa wataniambia ukweli wake kuhusu mtoto wake na vijimambo vyake vingine

Unaonaje hapa kaka je niachane nae au nifanye nini manake niko nae kwa mwaka mzima sasa , nimepigania nae maisha mpaka sasa hivi na tumekuwa tukifurahi na hata wazazi wangu wanamjua

What should i do ¿

Naomba ushauri
 
mmmh anaweza kuwa na mke na mtoto. Penzi halilazimishwi. kama unaona haelekei tafuta mwingine. Wakina sisi ambao hatujaoa na tunatafuta wachumba tupo wengi.

Muite faraga muongea hata kama ni usiku kucha basi muonge bila hasira na kama ni kuachana muachane pia bila kugombana.

Jinsi ya kufanya ni kuelezea maisha yenu tangu day 1, maudhi yooooote, Raha zoteeeeeeeeeee, na nini msimamo wako wa sasa(pamoja na tetesi ulizosikia) na ungependa kusikia nini kutoka kwa kila mmoja wenu.
Kila mtu akieleza feelings zake bila hasira mtafikia muafaka wa kuendelea au kuachana
 
Hi

Habari zako

Nafikiri wewe ni mzima au sio

Mimi pia ni mzima sana hapa nilipo maisha yangu ni kawaida tu ila kwa sasa hivi naiona dunia sasa hivi kama chungu hivi , nilizoea kuwa na furaha na kujinafasi lakini ghafla naona mambo yanakuwa mchanganyiko

MAMBO YENYEWE

Tumekuwa tukigombana na mambo kama hayo ambayo ni ya kawaida lakini haswa zaidi ni kuhusu yeye mwenyewe kuwa msiri katika mambo yake na vitu vyake vingine ambavyo mimi kama mpenzi wake nilitakiwa kujua lakini hakupenda kuniambia wala nini ingawa nilikuwa namsaidia na kujaribu kuwa nae karibu zaidi .

Sasa hivi amegraduate ameniambia tuachane sababu kubwa ni kwamba yeye ni muisilamu na wazazi wake hawapendi mtoto wao awe na mpenzi ambaye sio muisilamu wakati mimi nachojua yeye ni mkristo na wadogo zake wote ni wakristo hata kwa majina na kadhalika .

Balaa zaidi jana usiku niliambiwa kwamba yeye ana mtoto ambaye yuko mkoani mbeya mwaka kesho ndio anaanza masomo hapo ndio nilichanganyikiwa kabisa kwa sababu hakuwahi kuniambia kuhusu kisa hichi

Ndio nikakumbuka kumbe pesa alizokuwa anatak kwangu kupeleka kwa bibi yake kumbe ni kwa ajili ya mtoto wake ambaye mimi simjui na sijawahi kupewa taarifa , kumbe anavyoniambia niwe mbali na ndugu zake ni kwa kuogopa wataniambia ukweli wake kuhusu mtoto wake na vijimambo vyake vingine

Unaonaje hapa kaka je niachane nae au nifanye nini manake niko nae kwa mwaka mzima sasa , nimepigania nae maisha mpaka sasa hivi na tumekuwa tukifurahi na hata wazazi wangu wanamjua

What should i do ¿

Naomba ushauri

Dada yangu pole kwanza kwa yaliyokukuta!! kwa ushauri wangu wa haraka haraka sikiliza moyo wako, kama jamaa unampenda na unafikiri huenda akabadilika asikurushe roho tena mbeleni ya maishani basi msamehe mfunge pingu za maisha.

Lakini kama ataendelea kuweka msisitizo muachane si busara kumng'ang'ania, achana naye na jitahidi umsahau kabisa. Unajua duniani ni kama baharini, samaki mmoja akiteleza unaendelea kuvua huenda ukapata kingfish wa kukuliza

Ni ushauri tu chekecha akili mukichwa yako

ush
 
Kwanza muongo, pili kakutumia kumtunza mwanawe ambaye hata hakuwa na ustaarabu wa kukwambia.Hata ukiendelea naye jiandae kwa maisha ya matatizo, kuongopewa na kutumiwa.

Achana naye, muogope kama ugonjwa.
 
Unangangania mtu huyo mmoja tu sababu gani? Kama mngekuwa nayo ndoa ningekushauri utunze doa yako na labda watoto! Usihesabu hizo hasara ndogondogo za kuwa ulikuwa ukimpa pesa nk, zimekusaidia kumjua vizuri. Nadhani ni faida zaidi ukiachana nae ukaanza maisha mapya ("good riddance" tunasema), lakini kumbuka msemo huu: "in every loss, don't forget the lesson in it", yaani kumbuka ulichojifunza katika tukio hili na ujitahidi wasije wakakugeuza gunia la mazoezi (punching bag). Kila la heri.
 
Kuna msema usemao

``When one door is closed another one is opened`` Dont waste your time looking at the closed door.
 
In life there is ups and downs. The best way is to talk to him kama kweli he means wot he says au anatikisa kibiriti. Then kama anatikisa kibiriti mweleze sio mahali pake. na kama ana mean business yaani off. Then ANZA mama. dont get hurt yrself. Na hata kama akija na machozi ya mamba don'nt let him in again. Last usijitoe kwa mwanammme cheaply. study them first. Good luck
 
..take some time to see the world!not him/her!

..go out with friends of yours who are single and enjoy your youth!

..concentrate on work and other things in life which are worthwhile!go out and seek the light.

..usigombane nae,usimtusi,usimwambie mnaachana/unamwacha,na wala usi-worry so much about him/her! worry about you!just love yourself!

..after some time you'll see the light!
 
Jamani mimi sio mwanamke kama wengi wanavyochangia mimi ni mwanaume

IMEKUWA BALAA ZAIDI KUNA WATU WAMECHOMOKA KWENDA KUMWAMBIA HUYU DADA
 
SHY!
najua hali inavyokuwa mtu kumpenda, najua inavyouma ukija gundua unadanganywa. Mimi mwenyewe nina experience kama hiyo kutoka kwa demu. Inauma sana hasa kama ulikuwa umempa moyo wako wote na hisia zako zote kiasi cha kuamua kuwa mtakuja oana.

Mimi ninamachache sana ya kukuambia

1.U can not force love (Penzi halilazimishwi mkuu)
2.Hakuna penzi la upande mmoja inaelekea huyo mwenzako hakupendi na hiyo ni hatari sana maana utaumia siku zote za maisha yako kama utalazimisha kuwa nae.
3.Cheater will always be cheater (muongo siku zote ni muongo) Mimi kama kunakitu nakichukia ni uongo bwana.

4. Kaa nae na mmuongee ila usilalamike na kujifanya cheap kwake. Atajua thamani yako mkishaachana nakuambia. Usigombane naye uwe diplomatic tuu

5. Usipende kuumiza hisia zako Shy nakushauri uachane naye itakuuma kwa muda mfupi lakini baadaye hutajutia. Hutakaa ujute kwanini uliachana naye. kama kweli anamtoto na hajakuambia ni wazi atauzalia watoto kibao wakati mkiwa kwenye ndoa.

6. Amini mungu hakukupangia na kuna mtu mwingine who worth ur time and love.
 
Japokuwa uamuzi wa mwisho unao wewe (maana mapenzi ni upofu, ukiandgalia kwa macho makavu hutaona)lakini ningekuwa mimi ningeachana nae. Dunia ya sasa haihitaji mpenzi asiye mkweli, muongo na mpenda maslahi pekee. Huyo hafai japo unampenda lakini kwa yeye kutokuwa muwazi kitakuja kukugharimu.
 
Mkuu sasa unaniangusha kwani ni nini kilichokufanya mpaka umpende huyo?
Kama unampenda kwa dhati sioni sababu ya kumwacha,mtoto si hoja.
Aliamua kukuficha bse anakupenda as kama ujuavyo wanawake ni wengi nowdays.
Take it easy mkuu ambaa nae tuu as long as mwapendana kwa dhati.
Tafuta mda akuambie ukweli wa mambo,na jinsi ilivyokuwa kwa mantiki ya kutaka kujua ukweli.
 
Mkuu sijibu kwa niaba ya SHY bali ni kuwa kama umesoma maelezo vizuri demu hampendi na ndio maana hataki hata kuolewa nae na kuja na visingizio vya dini. Mimi naamini hili ni penzi la upande mmoja tuu mkuu.
 
Pole sana lakini cha muhimu ameshakueleza ukweli kuwa muachane sasa labda kama alivyosema mjumbe mmoja kuwa mtafute ili ujue sababu ya yeye kutaka muachane ili kwamba usije ukapata mwingine ukajikuta umerudia kosa lile, hata hivyo hujasema mlikuwa na malengo gani wakati mnaanza mahusiano yenu na ndo sababu hakuwa amekueleza kama ana mtoto bila shaka kila mtu alikuwa na mawazo yake.

NB:Mapenzi hayalazimishwi using`ang`anize kama hakutaki uta teteseka bure kumpenda asikupenda na atazidi kukutesa muelewe wala usimkasirikie kwa uamuzi wake MUNGU ANA MAMBO MENGI.
 
WEKENI MAJINA SAWASAWA HATA MIMI HAPA NILIDHANIA U DEMU. I am so sory. If you are youngman then all the world is yrs. learn first. dont commit yrself and make early promises. Maua ya kutua yapo kibao!! just Involve God will help to find yr Ubavu. Stay blessed
 
Kweli..

Lakini Shy Mbona Inaonekana Haufanani na huyo...Ndoa Ni kuunganisha akili...sasa..atakusumbua sana...!!Nashindwa kukushauri uachane nae..japo that is a solution..
 
Kwanza samahani sana maana mimi nami nilielewa vibaya na nilikuwa wa kwanza kucomment.

Naikistika kusema hivi lakini hao ndugu zetu wa Mbeya Mwa..s naona wanashida kidogo kwa hilo maaana nianazo cases 9 za namna hiyo na 7 kati ya tisa zilitokea bado nipo hapo Mlimani. Achana na zinazotokea sehemu ingine. So sijuui why huko Mbeya?

Naamini kila mtu ni unique na kila binadam hupotoka kwa mawazo,maneno au vitendo hivyo angalia tofauti zenu mzitatue ikishindikana achaneni
 
QUALITY OF PERFECT COUPLE

With the divorce rate over 50%, too many are apparently making a
serious mistake in deciding whom to spend the rest of their life with. To avoid becoming a "statistic," try to internalize 10 insights.

1. You pick the wrong person because you expect him/her to change after you're married. The classic mistake, never marries potential. The golden rule is, if you can't be happy with the person the way he or she is now, don't get married. As a colleague of mine so wisely put it, "You actually can expect people to change after their married...for the worst!" So when it comes to the other person's spirituality, character, personal hygiene, communication skills, and personal habits, make sure you can live with these as they are now.

2. You pick the wrong person because you focus more on chemistry than on character. Chemistry ignites the fire, but good character keeps it burning. Beware of the "I'm in love" syndrome. "I'm in love often means, "I'm in lust." Attraction is there, but have you carefully checked out this person's character? Here are four characteristics to definitely check for: a. Humility: Does this person believe that "doing the right thing" is more important than personal comfort? b. Kindness: Does this person enjoy giving pleasure to other people? How does s/he treat people s/he doesn't have to be nice to? Does s/he do volunteer work? Give to charity? c. Responsibility: Can I depend on this person to do what s/he says? What s/he's going to do? d. Happiness: Does this person like himself? Does s/he enjoy life? Is s/he emotionally stable? Then ask yourself: Do I want to be more like this person? Do I want to have a child with this person? Would I like my child to turn out like him or her?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom