Sijaelewa vizuri... inamaana wewe unakaa kwenu na mkeo ama hua manalala kwenu mkienda kutembea huko nyumbani?? Alafu mila ya makabila mengi ya hapa Tz sio heshima mwanaume kulala kwa wakwe na Mkewe labda in speacial cases.. mbona kitendawili... mbaya zaidi anaesema hivo na kukupa headache ni rafiki wala hata sio wakwe.... kuna nini hapa Herimini??
tunalala kwetu tukienda kuwasalimia wazazi wetu..naambiwa siku nyingine tulale ukweni!
Ashadii hapo ndio ninapoona kituko. Unaamka asubuhi na mkeo hata kama hamkufanya lolote unakutana na mama mkwe mlangoni au koridoni mnaangalianaje na wanafikiria nini vichwani mwao
Ahh hata kama ni mila hizo nyingine ni balaa bana
mimi nimeoa jirani sana na nyumbani kwetu. tangu nimeoa sijawahi kulala ukweni kwa sababu ni mwendo wa dakika tu kutoka kwetu hadi ukweni. rafiiki yangu anasema kuwa kitendo cha kutolala na mke wangu kwao ni kutomtendea haki kwani yeye analala kwetu. anasema ni vizuri kwa mahusiano kulala ukweni na mkeo eti inakuongezea heshima toka kwa wazazi wa mke wako! mimi kweli sielewi lakini mke wangu anasapoti. naombeni ushauri wenu.